Ndio maana nasema wasabato sio wakristo kwa maana Yesu alishasema sio kimwingiacho mtu ndio kinamtia unajisi bali kimtokacho mtu. Wasabato bado mnaamini mambo ya Agano la kale kuhusu unajisi wa vyakula?!
Tatizo mnasoma BIBLIA Kama Gazeti, ndio maana mtaendelea kuibiwa na kuuziwa Maji, Mafuta ,udongo na matapeli kina Mwamposa Hadi mnaingia kaburini maana Hamchunguzi Maandiko
BIBLIA HUMAANISHA NINI INAPOSEMA KIMUINGIACHO MTU AKIMTII UNAJISI BALI KIMTOKACHO?
Ni jambo gani ambalo Biblia inasema katika Marko 7:15-23?
Biblia Inasema
"Hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, bali vile vimtokavyo, ndivyo vimtiavyo unajisi yule mtu. [Mtu akiwa na masikio ya kusikilia, na asikie.]
Hata alipoingia nyumbani, ameuacha mkutano, wanafunzi wake wakamwuliza habari za ule mfano.
Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi;
kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote.
Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi.
Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,
wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.
Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi."(Marko 7:15-23).
Sasa shida inayokuja hapa watu wameshikilia kula vyakula najisi kuwa ni halali kama vile kitimoto na kambare na wanasema inahusisha mwili tu, wanasahau Kuwa kukaidi agizo la Mungu ni matokeo ya uasi ambao uanzia kwenye maamuzi, Lakini pia wanasahau kuwa Yesu ametaja na mambo mengine yanayoweza kumtia mtu unajisi, kama vile ufisadi, uuaji, uzinzi, wivi, je hivi vinausisha roho tu? Je havina matokeo yoyote kwenye mwili kiasi cha mwili kuhusishwa? Inabidi wafikilie upya.
Katika Marko 7:15-23, Yesu hatamki kwamba mtu anaweza kula kitu chochote. Baadhi ya vyakula na vinywaji havistahili na pia vinafisha, na vingine ni hatari kabisa kwa afya. Angalia katika (Walawi 11:2-23) kwa ajili ya orodha ya wanyama, ndege, samaki, na wadudu wasiofaa kuliwa.
Anachoelekeza Yesu hapa ni imani kuwa endapo Myahudi mtaua (mcha Mungu kwelikweli) akifuata tu sheria za usafi wa taratibu za kidini atakuwa safi kimaadili/kiroho. Kwa upande mwingine, hakuna chakula ambacho kwa chenyewe kinaweza kuinajisi tabia ya mtu. Kinachonajisi ni mawazo maovu (ambayo hujitokeza kwa ndani na kujidhihirisha katika matendo ya nje). Ndiyo maana Biblia inatuambia, “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.” (Mithali 4:23)
Hapa Yesu hasemi kuwa vyakula vyote vinaruhusiwa au vinafaa kuliwa. Yesu anatumia vitendo vya nje vya kuosha mikono na kula kama kielelezo cha matendo ya nje ili kuweza kutofautisha na hali ya moyoni. Yesu hugeuza mtazamo wa walimu wa sheria, waliingiza mapokeo ambayo hayakuwa agizo la Mungu, miongoni mwa mapokeo hayo ni kunawa hadi kwenye kiwiko Kabla ya kula Biblia Inasema "Kwa maana Mafarisayo na Wayahudi wote wasiponawa mikono mpaka kiwiko, hawali, wakishika mapokeo ya wazee wao;" (Marko 7:3). Kwa hiyo hata kama ungekula chakula ambacho sio najisi kwao walikiita najisi kwa sababu tu haujanawa hadi kwenye kiwiko, na Habari hizi zilizua mjadala baina ya Yesu na mafarisayo na kuamua kuwaambia ukweli, Biblia Inasema "Akawaambia, Isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa,Watu hawa huniheshimu kwa midomoIla mioyo yao iko mbali nami;
Nao waniabudu bure,Wakifundisha mafundishoYaliyo maagizo ya wanadamu," (Marko 7:6-7).
Basi ingekuwa vyema kwa kila msomaji wa maandiko kutambua kuwa mgogoro ulianzia nyuma kwenye kutokunawa hadi kwenye kiwiko mpaka Yesu anafikia hatua ya kusema "kimuingiacho mtu akimtii unajisi, bali kimtokacho" mawazo ya mafarisayo yalishatiwa unajisi,
walikuwa wamejikita katika mambo ya nje, wakati Yesu alisisitiza matendo ya ndani ya roho, hali ya kimaadili/kiroho. Ni rahisi kudumisha hali ya nje ya kuwa Mkristo kwa kile tunachofanya au tusichofanya. Hata hivyo, wakati ambapo wanadamu huangalia nje, Mungu huangalia hadi ndani ya moyo hupima nia ya makusudi yanayosukuma matendo yetu. (Angalia pia Mwanzo 1:29-30; Matendo 10; 1 Wakorintho 10:31).
Roho Mtakatifu akusaidie kuelewa hili.