Je, Kila Mwanasiasa Tajiri ni Fisadi?

Aisee nini kifanyike sasa ili malalamiko yakome
 
wanasiasa hawa wanatoka kwenye jamii hizihizi hivyo wanafahamika kwa maana familia zao na maisha yao yanafahamika na jamii hivyo kunapotokea madiliko makubwa ya ghafla yani kwenda kwenye huo utajiri unaosema kwa mishahara hii ya kwenye siasa hapa kwetu...hapo ndo pakuanzia.
 
Wewe naona umenyooka hauna unafiki
Issue ya kushinda kwenye hela na kuingalia bila kudokoa ni ngumu si ndio

Muhimu udokoe kidogo tu bila kuacha athari kubwa

Kuhusu huyo Samia sijui chochote
 
Upo sahihi tunajuana wenyewe
Ila kuna wana siasa wafanya biashara ina maana wana vyanzo vya mapato zaidi ya kimoja
 
Upo sahihi tunajuana wenyewe
Ila kuna wana siasa wafanya biashara ina maana wana vyanzo vya mapato zaidi ya kimoja
utajiri unaotokana na mwanasiasa anayejishughulisha na biashara unaonekana na unajulikana mbona... Utajiri wa wanasiasa wetu hapa bongo ni kazi sana kuutetea wanapohusishwa na ufisadi.
 
Hao walikua nazo kabla ya udiwani mfano marehemu Manji. Hauwezi kuona mtu mwenye hali ya kawaida halafu baada ya kupata udiwani tu utajiri wake ukwasi wake unaanza kupaa kwa spidi kama Bashite
Anaweza kupata utajiri akiwa kwenye uongozi kwa njia halali. Kwa mfano, anaweza kuwa na biashara iliyokuwepo kabla ya kuingia madarakani ambayo inaendelea kukua, kufanya uwekezaji halali, au kupata mapato yanayoruhusiwa kisheria kutokana na kazi na mali zake.
 
Kwa mtazamo wangu, kugombea uongozi ni haki ya kikatiba na pia ni aina ya utumishi wa umma. Baada ya kuchaguliwa, kiongozi hulipwa mshahara na stahiki zinazotambuliwa kisheria kama ilivyo kwa watumishi wengine wa umma. Kwa hiyo, kuwa na maisha mazuri pekee si ushahidi kwamba mtu amejihusisha na vitendo vya rushwa au ufisadi.

Kilicho muhimu ni chanzo cha mali na uwajibikaji. Ikiwa mali na maisha ya kiongozi yanaendana na kipato chake halali na vinaweza kuelezewa kwa uwazi, hakuna sababu ya kumhukumu. Vivyo hivyo, ikiwa kuna ushahidi wa matumizi mabaya ya madaraka au mali isiyoelezeka, basi vyombo vya uchunguzi na sheria ndivyo vinapaswa kufanya kazi, si hisia au dhana za watu.
 

Ili mtu aitwe TAJIRI huko duniani anatakiwa awe na sifa tatu...
1. Awe na miradi yenye kuingiza pesa za kueleweka
2. Awe ameajiri watu wengi
3. Awe mlipaji mkubwa wa Kodi kutoka kwenye hiyo miradi yake

UKIKOSA HIZO SIFA TATU NA UNA HELA NYINGI WEWE NI FISADI!

Wenzetu huko Duniani huwezi kutajwa kama TAJIRI kama huna hizo sifa tatu hata ungekuwa na hela nyingi; Wana kuona kama muuza unga tu....
 
Kwani hua wanategemea mshahara pekee?
Hawana biashara?
Au mpka watangaze biashara zingine wanazofanya?
KWA MUJIBU WA SHERIA, KUNA LEVEL YA UONGOZI MTU AKIIFIKIA ANATAKIWA KUJAZA FOMU FULANI ZINAZOONESHA KIPATO CHAKE, UWEKEZAJI WAKE NA MALI ALIZONAZO. LAKINI KATIKA KUKWEPA HILO TAKWA LA KISHERIA BAADHI YA VIONGOZI WASIO WAAMINIFU KAMA KUNA MALI WALIZIPATA ISIVYO HALALI HUWA WANAZISAJILI KUWA ZINAMILIKIWA NA NDUGU ZAO.
NAWAFAHAMU WATU KADHAA WALIOWAHI KUFANYA HUO MCHEZO, MMOJAWAO NI HOMEBOY WANGU.
 
Sawa nimeelewa kwamba mwanasiasa ana haki ya kumiliki mali na kua na maisha mazuri kwa sababu mbali na uanasiasa wake yeye ni mtumishi kama watumishi wengine

So kama kuna sntofahamu vyombo vya uchunguzi na sheria ndivyo vinapaswa kufanya kazi na sio dhana ambazo wakati mwingine sio halisi

Asante kwa maoni karibu tena
 
Upo sahihi hapa kwetu ni tajiri yupi katajwa na ni mwanasiasa mi hua nawasikia kina mo na wengineo
 
Wewe naona umenyooka hauna unafiki
Issue ya kushinda kwenye hela na kuingalia bila kudokoa ni ngumu si ndio

Muhimu udokoe kidogo tu bila kuacha athari kubwa

Kuhusu huyo Samia sijui chochote
Siyo kudokoa kidogo au kikubwa sifa ya mdokozi mzalendo hata akidokoa kikubwa basi icho alicho dokoa nacho anakenda kufanyia mambo ya manufaa kwa taifa tofauti na asiye mzalendo..mfano tajiri mzalendo atumii utajiri wake kuujumu nchi yake bali anatumia utajiri wake kwa manufaa ya nchi yake pia ..hivyo UFISADI WA KIZALENDO BADO UPO KUNUFAISHA TAIFA TOFAUTI NA UFISADI USIO WA KIZALENDO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…