Je, kujenga nyumba ya makazi bila kibali ni kosa? Kwanini watu wengi hufanya hivyo bila kusumbuliwa?

OMKEIT 93

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2026
Posts
294
Reaction score
442
Wakuu,
Kuna jambo nimekuwa nikijiuliza kwa muda na naamini kuna watu humu wanaweza kuwa na uzoefu au uelewa mzuri wa sheria za ujenzi Tanzania.

Je, mtu anayejenga nyumba yake ya makazi kwenye kiwanja chake anatakiwa kuwa na kibali cha ujenzi kabla ya kuanza kujenga?

Kwa sababu ukienda mikoani au maeneo ya pembezoni, utaona watu wengi wanajenga nyumba zao bila kibali chochote. Wengine wanajenga mpaka nyumba inakamilika, wanaingia na kuishi humo miaka mingi, lakini hujawahi kusikia mamlaka imewafuata.

Sasa hapa ndipo maswali yangu yanapoanzia:
1. Kisheria, ni lazima kupata kibali cha ujenzi kabla ya kujenga nyumba ya makazi?

2. Kama ni lazima, kwa nini watu wengi hasa mikoani wanajenga bila kibali na wanaendelea kuishi kwenye nyumba hizo bila kuchukuliwa hatua?

3. Je, mamlaka huwa hazijui au huwa zinajua lakini zinaacha kwa sababu mbalimbali?

4. Kuna tofauti kati ya kujenga bila kibali kwenye mji/manispaa na kujenga kijijini au maeneo ambayo hayajawekwa kwenye planning area?

5. Mtu akijenga nyumba bila kibali, madhara yake ni yapi? Je, ni faini tu, au kuna uwezekano wa kuamriwa kubomoa nyumba?

6. Je, kuna mtu hapa ambaye yeye mwenyewe au mtu anayemfahamu amewahi kujenga nyumba kisha mamlaka ikaja na kuamuru ibomolewe kwa sababu ilijengwa bila kibali?

Naomba hasa wale waliowahi kupitia jambo hili watoe uzoefu wao.
Kwa sababu kuna tofauti kati ya kusema:
"Watu wengi wanajenga bila kibali na hakuna kinachotokea"
na kusema:
"Kisheria unaruhusiwa kujenga bila kibali."
Haya ni mambo mawili tofauti kabisa.
Na swali langu kubwa zaidi ni hili:
👉 Kama mtu ana kiwanja chake halali, analipa kodi zake, hana mgogoro na jirani, na anajenga nyumba ya familia yake kwa fedha zake mwenyewe—ni kwa nini bado anatakiwa kupata kibali cha ujenzi?

Kibali hicho kinasaidia nini hasa?
Je, ni kuhakikisha ramani imefuata mipango ya eneo? Usalama wa jengo? Barabara na mifereji? Umbali kutoka kwenye mipaka ya kiwanja? Au ni utaratibu wa serikali tu?

Wajuzi wa sheria za ardhi, mipango miji, halmashauri, mafundi na watu waliowahi kujenga nyumba—karibuni sana.
Tuelezeni ukweli wa mambo ulivyo kwa vitendo na kisheria.

Je, kuna mtu amewahi kuvunjiwa nyumba yake kwa sababu tu alijenga bila kibali?

Omkeit.
 
Ni maswali yanayohitaji mtaalamu wa ardhi, ila ninachojua ukiwa tayari unaishi kwenye hiyo plot hata kama unaishi room 1 ukianzisha ujenzi hakuna atakayekufuatilia kama kiwanja kipo ndani ndani ila kama ni eneo lililo karibu na barabara utapigwa 🔧
 
Nasikia vibali vyenywe kuvipata ni kwa mbinde!
 
Wakuu,
Kuna jambo nimekuwa nikijiuliza kwa muda na naamini kuna watu humu wanaweza kuwa na uzoefu au uelewa mzuri wa sheria za ujenzi Tanzania.

Je, mtu anayejenga nyumba yake ya makazi kwenye kiwanja chake anatakiwa kuwa na kibali cha ujenzi kabla ya kuanza kujenga?

Kwa sababu ukienda mikoani au maeneo ya pembezoni, utaona watu wengi wanajenga nyumba zao bila kibali chochote. Wengine wanajenga mpaka nyumba inakamilika, wanaingia na kuishi humo miaka mingi, lakini hujawahi kusikia mamlaka imewafuata.

Sasa hapa ndipo maswali yangu yanapoanzia:
1. Kisheria, ni lazima kupata kibali cha ujenzi kabla ya kujenga nyumba ya makazi?

2. Kama ni lazima, kwa nini watu wengi hasa mikoani wanajenga bila kibali na wanaendelea kuishi kwenye nyumba hizo bila kuchukuliwa hatua?

3. Je, mamlaka huwa hazijui au huwa zinajua lakini zinaacha kwa sababu mbalimbali?

4. Kuna tofauti kati ya kujenga bila kibali kwenye mji/manispaa na kujenga kijijini au maeneo ambayo hayajawekwa kwenye planning area?

5. Mtu akijenga nyumba bila kibali, madhara yake ni yapi? Je, ni faini tu, au kuna uwezekano wa kuamriwa kubomoa nyumba?

6. Je, kuna mtu hapa ambaye yeye mwenyewe au mtu anayemfahamu amewahi kujenga nyumba kisha mamlaka ikaja na kuamuru ibomolewe kwa sababu ilijengwa bila kibali?

Naomba hasa wale waliowahi kupitia jambo hili watoe uzoefu wao.
Kwa sababu kuna tofauti kati ya kusema:
"Watu wengi wanajenga bila kibali na hakuna kinachotokea"
na kusema:
"Kisheria unaruhusiwa kujenga bila kibali."
Haya ni mambo mawili tofauti kabisa.
Na swali langu kubwa zaidi ni hili:
👉 Kama mtu ana kiwanja chake halali, analipa kodi zake, hana mgogoro na jirani, na anajenga nyumba ya familia yake kwa fedha zake mwenyewe—ni kwa nini bado anatakiwa kupata kibali cha ujenzi?

Kibali hicho kinasaidia nini hasa?
Je, ni kuhakikisha ramani imefuata mipango ya eneo? Usalama wa jengo? Barabara na mifereji? Umbali kutoka kwenye mipaka ya kiwanja? Au ni utaratibu wa serikali tu?

Wajuzi wa sheria za ardhi, mipango miji, halmashauri, mafundi na watu waliowahi kujenga nyumba—karibuni sana.
Tuelezeni ukweli wa mambo ulivyo kwa vitendo na kisheria.

Je, kuna mtu amewahi kuvunjiwa nyumba yake kwa sababu tu alijenga bila kibali?

Omkeit.

Naweza kutolea maelezo ya suala hili binafsi kama ifuatavyo kwa uzoefu wangu:

Kisheria ni lazima na ni muhimu kwa pande zote mbili kutoa na kupata kibali cha ujenzi wa nyumba kwa eneo husika bila kujali limepimwa au halijapimwa na mipango miji au serikali.

Sababu kuu ni kama ifuatavyo:

1: Kuhakikisha ujenzi umefuata mipango ya ardhi ya eneo husika.

Huwa kuna uwezekano mkubwa wa kupata kiwanja ambacho kiko kwenye eneo lenye lengo au malengo tofauti ya matumizi ya kiwanja kwa mujibu wa ramani ya eneoo husika. Unaweza kukuta eneo husika ni shule, barabara, soko nk.

2: Ni sahihi kwa upande wa usalama wa jengo na watumiaji wengine ya ardhi pia.

Hapa huzingatia aina ya ardhi na uwezo wake, ndipo unahitajika kupeleka mchoro wa jengo kuonyesha msingi, kuta, paa, na jinsi mfumo wa maji taka na maji ya mvua yatakavyofanyiwa kazi. Hapa pia utazingatiwa usalama kwa upande wako na jirani zako.

3: Umbali kutoka kwenye mipaka ya viwanja vingine kuepusha migogoro.

Ni kweli, katika hatua za ujenzi ni vyema kuzingatia majirani na nafasi au njia ya majirani kwa pande zote Pamoja na huduma za kijamii kama moto, hospitali nk.

4: Sisi kama wapangaji kwenye ardhi, ni vyema kutambulika na kufanya malipo kwa utambulisho kamili wa eneo husika na matumizi tunayofanya juu ya ardhi husika.

5: Kuipa ardhi thamani na kutumika kama dhamana kwenye vitenngo vya kifedha kama bank ink. Hapo unaweza kutumika kuchukulia mkopo ardhi ikiwa dhamana nk.

6: NK.

Changamoto:

1: Huduma hii haijawa na ufatiliaji mzuri kwa maeneo mbalimbali ya nchi hasa pembezoni mwa miji. Ukamilifu mzuri unasuasua/unashindikana kutokana na maeneo mengi ya nchi kutokuwa yamepimwa kabla ya watu kuyafikia na kuanzisha makazi ya kudumu. Hivyo, serikali kuanza upimaji baada ya watu kuanza kuishi maeneo husika na kuidhinisha.

2: Uchache wa watendaji wa kazi ambao hufanya ufatiliaji wa maeneo kuwa hauna ufanisi hasa nje ya miji.

3: Uchache au kiasi kidogo cha pesa kutengwa ili kukidhi kazi ya upimaji kulingana na spidi ya watu kuku ana miji kupanuka.

4: Ukiritiba ndani ya mfumo wa ardhi katika kutekeleza majukumu yao. Watu wengi kufanya kazi kwa kusukumwa kuliko kutekeleza majuku yao ya msingi.

5: Harufu ya kukifanya kitengo husika kama chanzo cha mapato kuliko uhitaji halisi wa huduma husika kwa mazingira, jamii na serikali.

6: Uwezo mdogo wa wananchi kuweza kulipia zoezi la vibali vya ujenzi na hivyo kupambana na maafisa wa serikali huko mitaani kwa kadriu itakavyowezekana.

7: Elimu duni kwa wananchi kuhusiana na zoezi husika

8: NK.

Kwa sasa unaweza kukuta mtu ana miaka 3 au zaidi tangu afanye malipo ya kuomba kibali, amepeleka ramani na kufanya malipo yote, ila anaishia kupata risiti ya malipo tu na kuendelea na ujenzi badala ya kibali husika.
 
Naweza kutolea maelezo ya suala hili binafsi kama ifuatavyo kwa uzoefu wangu:

Kisheria ni lazima na ni muhimu kwa pande zote mbili kutoa na kupata kibali cha ujenzi wa nyumba kwa eneo husika bila kujali limepimwa au halijapimwa na mipango miji.

Sababu kuu ni kama ifuatavyo:

1: Kuhakikisha ujenzi umefuata mipango ya ardhi ya eneo husika?

Huwa kuna uwezekano mkubwa wa kupata kiwanja ambacho kiko kwenye eneo lenye lengo au malengo tofauti ya matumizi ya kiwanja kwa mujibu wa ramani ya eneoo husika. Unaweza kukuta eneo husika ni shule, barabara, soko nk.

2: Ni sahihi kwa upande wa usalama wa jengo na watumiaji wengine wa ardhi pia.

Hapa huzingatia aina ya ardhi na uwezo wake, ndipo unahitajika kupeleka mchoro wa jengo kuonyesha msingi, kuta, paa, na jinsi mfumo wa maji taka na maji ya mvua yatakavyofanyiwa kazi. Hapa pia utazingatiwa usalama kwa upande wako na jirani zako.

3: Umbali kutoka kwenye mipaka ya viwanja vingine kuepusha migogoro.

Ni kweli, katika hatua za ujenzi ni vyema kuzingatia majirani na nafasi au njia ya majirani kwa pande zote Pamoja na huduma za kijamii kama moto, hospitali nk.

4: Sisi kama wapangaji kwenye ardhi, ni vyema kutambulika na kufanya malipo kwa utambulisho kamili wa eneo husika na matumizi tunayofanya juu ya ardhi husika.

5: Kuipa ardhi thamani na kutumika kama dhamana kwenye vitenngo vya kifedha kama bank ink. Hapo unaweza kutumika kuchukulia mkopo ardhi ikiwa dhamana nk.

6: NK.

Changamoto:

1: Huduma hii haijawa na ufatiliaji mzuri kwa maeneo mbalimbali ya nchi hasa pembezoni mwa miji. Ukamilifu mzuri unasuasua/unashindikana kutokana na maeneo mengi ya nchi kutokuwa yamepimwa kabla ya watu kuyafikia na kuanzisha makazi ya kudumu. Hivyo, serikali kuanza upimaji baada ya watu kuanza kuishi maeneo husika na kuidhinisha.

2: Uchache wa watendaji wa kazi ambao hufanya ufatiliaji wa maeneo kuwa hauna ufanisi hasa nje ya miji.

3: Uchache au kiasi au kidogo cha pesa kutengwa ili kukidhi kazi ya upimaji kulingana na spidi ya watu kuku ana miji kupanuka.

4: Ukiritiba ndani ya mfumo wa ardhi katika kutekeleza majukumu yao. Watu wengi kufanya kazi kwa kusukumwa kuliko kutekeleza majuku yao ya msingi.

5: Harufu ya kukifanya kitengo husika kama chanzo cha mapato kuliko uhitaji halisi wa huduma husika kwa mazingira, jamii na serikali.

6: Nk.

Kwa sasa unaweza kukuta mtu ana miaka 3 au zaidi tangu afanye malipo ya kuomba kibali, amepeleka ramani na kufanya malipo yote, ila anaishia kupata risiti ya malipo tu na kuendelea na ujenzi badala ya kibali husika.
Sasa kwa mazingira hayo kupata kibali si usumbufu mkubwa na hayo masharti ya ramani wenye vipato vya chini wanao unga unga wanaweza! Wakati mwengine ukifikilia kibali unachoka🤔
 
Kuna vitu ambavyo halmashauri zetu zinafanya na kuviweka, ukiangalia uhalisia na kipato cha wanachi ni vigumu kutekelezeka kwa ufanisi na ni maumivu makali. Na UKIZINGATIA kibali husika kinakuwa hai ndani ya mwaka mmoja tu. Ina maana uwe umekamilisha ujenzi, sina uhakika kama walishabadili hili. Mtanzania wa kawaida awe na chanzo cha mapato cha kuwa amemaliza ujenzi ndani ya mwaka mmoja!!!?? Hapa ni mtego, ndo maana watu wanaona ni vyema kupozana mtaani huko kuliko kulipa kinachotakiwa.
 
Kuna vitu ambavyo halmashauri zetu zinafanya na kuviweka, ukiangalia uhalisis na kipato cha wanachi ni vigumu kutekelezeka kwa ufanisi na ni maumivu makali. Na UKIZINGATIA kibali husika kinakuwa hai ndani ya mwaka mmoja tu. Ina maana uwe umekamilisha ujenzi, sina uhakika kama wakishabadili hili. Mtanzania wa kawaida awe amemaliza ujenzi ndani ya mwaka mmoja!!!??
Umeeleza vizuri mkuu.Bila kusahau, ujenzi unapoendelea ukaguzi unatakiwa ufanyike kwa kila hatua na masharti ya ujenzi kama kuacha mita kadhaa kutoka kwenye "bikoni",upandaji wa miti,nafasi ya nyumba/uwanja na uwanja/kichochoro kuachwa kutimizwa.
Bila kusahau, nyumba ikimalizwa kujengwa,mwenye nyumba anapaswa kupewa kibali/leseni ya kuhamia kwake n.k.
 
Nyumba itaandika stop by ....kwa spray nyekundu. Utawafuata ofisini wakakupe maelekezo, kisha utaendelea na ujenzi wako. Kama umejenga hifadhi ya barabara utaandikiwa bomoa
 
Kwa uzoefu wangu ni huu:-

Viwanja vilivyopimwa :- Hii hauwezi kujenga nyumba bila kuwapelekea ramani halmashauri/manispaa husika ili maengineer wa mipango miji waangalie kama imekidhi vigezo na msharti...Ukijenga nyumba ya chini utapeleka architecutural design tu ila ukijenga ghorofa utapeleka both architectural and structural designs then wakishaona ipo sawa ndipo watakuapa kibali cha ujenzi ,usipofanya hivyo wakija kujua watakupiga fine ya 2% ya gharama ya jengo ulipofikia.

Kwa viwanja ambavyo havijapimwa(skwata):- Hapa mara nyingi wanaopiga pesa ni watendaji na wenyeviti tu wa mtaa kwa kujifanya wanatoa vibali ,hivyo vibali vyao havitambuliki manispaa wala halmashauri.
 
Nyumba itaandika stop by ....kwa spray nyekundu. Utawafuata ofisini wakakupe maelekezo, kisha utaendelea na ujenzi wako. Kama umejenga hifadhi ya barabara utaandikiwa bomoa
Kwahiyo hakuna ulazima wa kibali kama sijengi eneo ambalo haliruhusiwi?
 
Back
Top Bottom