Je, kuna baadhi ya Familia zimebarikiwa?

Umenikumbusha kuhusu motivation speakers, watu wanapenda kusikia mafanikio ya motivation speakers wakati hawana sifa kumbe km huna sifa hata moja ya ujasiriamali huwezi kufanya biashara yoyote
 
Hebu soma nilichoandika kirefu kidogo kuhusu familia ya Mwapachu utapata kitu hapo
Sawa sawa mkuu ngojea niipitie tena.

Hongereni pia kwa kuthamini elimu hata kufanya harambee kuwasomesha wengine. Haya tumeyaona zaidi kwenye jamii za nchini Kenya, huku kwetu michango ya harusi ndio kipaumbele.
 
Sifahamu tufahamishane ndugu.
Akili ni uwezo wa kutafsiri ulicho kihifadhi kwa kukiona ama kujifunza, uwezo wako wa kutafsiri jambo haraka kwa mulekeo chanya hapo utaambiwa una akili sana, binadamu ana akili sana ila binadamu huyo huyo ni mvivu wa kufikiri na ukitaka kujua binadamu ana akili sana pindi akipata tatizo huamsha ubongo wake na kutatua tatizo Akisha tatua tatizo matako hulia mbwata , kumbe akili zilezile angelikuwa anazitumia kila siku ange fika mbali sana
 
Sawa sawa mkuu ngojea niipitie tena.
Hebu pitia pitia mkuu tujadili hii mada maana kama ni maadili watoto wetu tunawapa mno na kuwalea vizuri yet bado hatukwamuki motivational speakers wanatukoroga sana.
Tukifahamiana vizuri tutafanyiana inbox tuwe tunajadili vizuri hata kufahamiana unaonekana ni mkereketwa mwenzangu
 
Uko sahihi mleta mada kuna famili hata vifo sio vingi watoto baba bibi ba mababu wote wako hai, katika umri mkubwa, na hizo familiya hakuna magonjwa majongwa yaani mpaka unajiuliza, ilikuwaje familiya fulani watu almost wote walikufa ktk umri mdogo na familiya nyingine wako hai mpaka wajukuu nae wanaanza kuzeeka dah
 
Hii ni kweli mkuu nashukuru sana nimejifunza.
 
Wanasaikolojia uchwara ndio wanasema hakuna kitu kama bahati,
Kuzaliwa katika familia ambayo wazazi wako ni Rais, tajiri, watu maarufu au mazingira yenye maendeleo ni bahati ya kwanza kwa sababu sio watu wote wanazaliwa katika familia za aina hiyo n na mazingira ya aina hiyo.

Kuna watu wanafanya maamuzi mabaya ambayo huenda yangewapoteza kabisa muelekeko kimaisha ila kwa sababu ya bahati labda hayo maamuzi hayadhuru sana tofauti na wengine wasio na bahati hiyo.
 
Ni kweli kabisa. Kuna watu hawajui hao motivation speaker ila wame toboa sana.
Hilo la motivation speakers nimelikuta kwangu naandika kitabu cha ujasiriamali kunawatu wataka nieleze Hadithi ya mafanikio yangu,(success story), nikabaki kushangaa mfano Hadithi ya mafanikio niliyoyapata wakati wa awamu ya 3 usingeliweza kuitumia ili ufanikiwe awamu ya 5, ama ninakuwa na Hadithi ya mafanikio ya bidhaa iliyo pigwa maruku kwasasa ama kwa kitu kilichopita na wakati, hili lina tukumbusha kuhusu uvivu wa kufikiri
 
Ni kweli nimepitia vizuri nimelewa, hongereni kwa kuweza kufanya harambee na kusaidia wengine wapate elimu, ni familia au koo chache zinaweza kufanya haya.

Kama ulivyosema ni kweli watu wana jitahidi kwenye malezi ila unakuta bado hawa fanikiwi. Ndio maana nimona tujadiliane juu ya hili ni namna ya kujifunza juu ya jamii zetu.

Hakika wewe ni mkereketwa mwenzangu nitakutafuta inbox.

Mfano wa familia uliyotaja ya Marealle juzi niloona wakimuaga mzee Gasper George Marealle kanisani tena Askofu mkuu alifika, ukisikia historia yake na watoto wake wote wame fanikiwa vyema mpaka una furahia.
 
Shule shule peleka mtoto shule iwe ya kata au vipi mkomalie asome na muaminishe kuwa huu ndio urithi wako onyesha umuhimu wa shule mtoto ajue kuwa elimu ni jambo kubwa si jambo la kuchezea akijua mmoja wengine watajua na watafuta na mafanikio yatafuta ila kama watoto unawaminisha shule si chochote basi umaskini kwenye familia hauwezi ondoka koo nyingi na familia nyingi zenye umaskini wa kupindukia ni familia na koo ambazo zilidharau elimu so komaa na elimu kwani watoto wakielimika watajua jinsi ya kusolve matatizo yao wangine watajiliwa watapata vipato watabadilisha maisha ya nyumbani nk

Ukiwa na elimu utajua upambanie wapi mfano leo hii vijana wenye sifa wanapambana na nafasi ya kazi ya upolisi, haya kijan akienda uko akipata ajira si njaa inapungua huo ni mfano mmoja

Mafanikio ya kweli na ya siyo na longo longo ni kwenye elimu

Angalia jamii unayoishi familia ambayo ina vijana hata watatu walio ajiliwa serikali au secta binafsi jinsi inavyo heshimika hata kama uko walipo hawana vyeo familia inapata status ya kipekee so ujachelewa komaa na kusomesha kama ujabalikiwa watoto saidia wale wenye kuonyesha wanaipenda elimu kwenye ukoo wako jitoe wasiaidie ili mfute laana ya ufukara wa ukoo saidia awe mtoto wa dada nani au nani mpe support watambiana mjomba furani ukimpigia sm masuala ya shule akatai kukupa pesa

Pekeleni wakajifunze ujuzi VETA nk
 
Kwa mtoto kuwa na Akili za shule most of the time Genetics matter, kama wewe ni kutoka familia ya vipanga hata uamue kupuuzia shule , kwenye nekta utapata four tu hata D mbili. Hata kama shule ulienda kwa kutegea. Ukitoka familia ya vilaza digrii huwa msamiati mnaousikia kwa wengine au redioni, shetani anawaandama, inakuwa tu shule hampendi bila sababu mnachukia kukaa darasani naturally, mnachukia kujisomea, mkijisomea ikija pepa mlikosoma ticha hatoi maswali na hata akitoa maswali hamkumbuki majibu sahihi, kusoma shule mnaona ni kituo cha polisi, mnasema bora shule iishe mkaendeshe daladala au boda!

For me, mtoto huchukua akili na maelekezo ya mama wakati wa kusoma shule, mama akikomaa mtoto anaweza kufika hadi chuo kikuu. Hapa of course kuna other factors kama shule unayosoma, the food you eat, the place you live etc.

Mtoto akimaliza shule kuja maisha ya mtaani ya kufanya kazi hapo huchukua maisha ya baba yake kama kioo katika maisha yake kwa kujua au kutokujua, kuna maamuzi atachagua aidha mtoto atamkubali na kumfuata dingi kuuza madafu au kuigiza filamu au atampinga mshua na kukataa kuuza madafu na kuamua kuwa muosha magari.

In most cases if a father is an office guy or civil servant, most of the kids wataangukia kazi za ofisi, baba akiwa mkulima, wanawe wengi watakuwa wakulima pia , baba akiwa polisi hatokosa polisi mmoja kwenye timu yake ya watoto japo huwa kuna exceptional kids ambao watafanya maisha tofauti na ya baba zao. Baba aliepanda ndege ni rahisi kwa wanawe kuja kuzipanda sana hizo ndege tena zaidi ya mshua wao
 
Sawa sawa. Mshike sana elimu usimwache aende zake.
 
Well said, you have nailed it Sir.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…