Je, kuna mtu yeyote aliyewahi kushuhudia na kuthibitisha uchawi? Njoo tuongee hapa!

Ukija kwenye sayansi inakataa ufafanuzi bila ushahidi
 
Hakuna wazungu wanaoamini uchawi, ulozi au kulogana karne hii, kama wapo ni sawa na Waislamu wachache wanaokula kitimoto.
Wazungu kiasi wamebaki na imani superstitious za bahati mbaya na nzuri pamoja na nyota(astrology).

Uchawi ni broad term.
Sio kulogana tu.

Wazungu ndio wastaarabu,
Je wanaamini kuwa kuna supernatural power na ambazo hazitoki kwa Mungu?.
 
Kwa nini unaamini uchawi upo 100% ?
 
Ukija kwenye sayansi inakataa ufafanuzi bila ushahidi

ni kweli. Kila ambacho hakina ufafanuzi tunaweza kuita uchawi.

Kwahiyo Uchawi upo.

Kigoma kuna wale wanaitwa Kamchape. Wanapita na kutoa mavitu ndan. Na wanapiga ramli zao na wakisema nyumba hii ina vitu. Wakiingia wanakuta vitu kweli. Na watu wote wanaviona.
Uliiona hii?.

Kuna yule Bibi alianguka na Ungo Arusha. Kama mwez mmoja nyuma, alikuwa anatoka karagwe na mume wake. Sijui walikuwa wanaenda wap, Akaanguka pekeyake. Uliiona?.

Kuna wale fisi walikula mtoto, walimvua nguo mtoto , wakamla, nguo hazikukutwa hata na damu.
Uliona?
 
Chuma ulete kuna namna yake ili ifanye kazi. Kuna sehem inadunda.
chuma ulete haifanyi kaz /haipenyi kwenye kitu cha Chuma.
ungeeleza hiyo namna yake ya kufanya kazi mkuu ili maswali yawe machache, maana ukisema chuma ulete haipenyi kwenye chuma nakua sielewi chuma gani unayozungumzia, maana karibu kila duka lina nodno nje na ni dhahiri nondo ni chuma.

Kuna hadithi kuwa Mababu zetu walikuwa wanatumia Nyuki kufukuza wazungu.
Kuna sehem ngome zao zilikuwa ni ngumu kuingia kwasababu ya mazindiko.
Ila wazungu wajanja wakawalaghai Waafrika wachache ndio wakawaingiza taratibu kwenye jamii husika.
hizi hadithi za maeneo gani na walihold kwa muda gani
 
Yaani watu wanaumiza sana akili na wana deciplne kubwa sana ya Maisha.

Mambo mengi kuhusu uchawi ni hearsay (Alisema Fulani).

Ila no evidence.

Science ipo cleared na akili ya binadamu ni infinite ina uwezo mkubwa wa kusababisha matokeo ambayo ukiwa hauelewi utaamini ni uchawi.
 
Hakuna wazungu wanaoamini witchcraft (uchawi, ulozi au kulogana) karne hii, kama wapo ni sawa na Waislamu wachache wanaokula kitimoto.
Wazungu kiasi wamebaki na imani superstitious za bahati mbaya na nzuri pamoja na nyota(astrology).
mkuu kuna zile documentary ambazo wanaonyesha wnaenda kutafuta mchawi ndani ya nyumba wanaongea nae kutumia vifaa vya frequency, au ni content tu
 
mkuu kuna zile documentary ambazo wanaonyesha wnaenda kutafuta mchawi ndani ya nyumba wanaongea nae kutumia vifaa vya frequency, au ni content tu

Kuna uchawi na kuna Mizimu, ghost, vibwengo, mashetani/maruhani .malaana nk.

Tuweke haya kwenye uchawi?.
Na yenyewe wakuu hamjawah kushuhudia?.
 
Reactions: Lax
Maisha Huwa hayampendelei MTU yeyote waovu na wema wote wanfanikiwa .

Shortly hauwezi ukafanikiwa kwa maombi peke yake au kwa kuroga bila nidhamu .


Uchawi ungekuwa unafanya kazi effectively sisi waafrica tungekuwa ndo tuna run the world ila ni vise versa yake .

Kwahiyo huo uchawi hata kama upo hauna maana yoyote kuufatilia na kutaka kujua upoje is waste of time
 
Jana maeneo ya temeke nimegusa mtu begani reaction yake ilikua ni WW3

😁😁😂
 
Kuna uchawi na kuna Mizimu, ghost, vibwengo, mashetani/maruhani .malaana nk.

Tuweke haya kwenye uchawi?.
Na yenyewe wakuu hamjawah kushuhudia?.
kushuhudia hapo tunduma watu wameshuhudia sakata la nyeti na watu kula kipondo ila mganga mkuu wa hospitali na jeshi lapolisi wamethibitisha nyeti hazijapotea.

wewe elezea namna gani chuma ulete haifanyi kazi benki
 
kushuhudia hapo tunduma watu wameshuhudia sakata la nyeti na watu kula kipondo ila mganga mkuu wa hospitali na jeshi lapolisi wamethibitisha nyeti hazijapotea.

wewe elezea namna gani chuma ulete haifanyi kazi benki

Sehem inayowekwa hela ikiwa imetengenezwa kwa mbao Chuma ulete inafanya kazi.

Sehem inayohifadh hela ikiwa imetengenezwa kwa Chuma . Basi chuma ulete haiingii.
 
Reactions: Lax
Kwahiyo hata shetan hayuko?.
Shetani never exit hajawahi kuwepo

Ni adui wa kubuni imagination enemy.

Ulimwengu unajiendesha fairly haumpendelei MTU ukiweka efforts yoyote Ile ipo siku itakulipa haijalishi wewe ni muovu au mwema

Shetani katengenezwa ili kubalance duality but hakuna shetani
 
Hatupingi uwepo wa uchawi kwa sababu hatujauona kwa macho, tunapinga uwepo wa uchawi kwa sababu ya mkanganyiko (contradictions) na matobo katika story za uchawi.

Kuhusu mfano wako wa maji ya bomba unakosa mashiko kwa sababu maji ni maji tu, kama mtu ameweza kuona mbao au tawi la mpapai likipitisha maji hawezi kushindwa kuelewa chuma au plastic ikipitisha maji.
Zaidi sana Dunia ya Leo Kuna teknolojia ya kunasa picha na sauti.

Pia story za Sayansi za bomba la maji, umeme, gravity, satellite, internet na protozoa ni zile zile, hazibadiliki, ziko constant na replicable miaka yote na sehemu zote duniani sio kama story za uchawi ambazo hata ku define tu uchawi wenye ni tatizo na kila mtu ana experience zake tofauti za uchawi na exceptions kibao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…