Sasa inawezekana vp mkuu kuwepo kwa uchawi ilhali kuna watu ndani ya miaka 40+ Tanzania hii hii hajaona huo uchawi?
Mbona kuna watu wengi tu wamefariki nchi hii bila kuona maji ya bomba au kitu simple kama umeme. Je, inaondoa ukweli kuwa vitu hivyo vipo
Yani kwa sababu kuna mtu hajui kama internet ya Starlink ipo duniani na hajawahi kuitumia. Ina manisha hicho kitu hakipo?...
Kwa hiyo existence ya kitu ni sahihi ikiwa tu itathibitishwa na kila mtu kuwa kipo.
Je, kabla ya Isaac Newton kugundua gravity, je inamaanisha gravity haikuwepo
Vipi kwa waliogundua electrons, au hata micro organisms ambazo leo hii huwezi kuziona pasipo kutumia microscope. Je kwa sababu wewe hujawahi kumuona protozoa lakini ukiwa diagnosed kutokana na impact ya hicho kitu. Ukapewa dawa na ukapona.. Japo hujui hata process ya hiyo dawa inafanyaje kazi mwilini hadi unapona "Ignorance" Yet kutokana na kupona "unaamini"
Sasa wewe Una tofauti gani na mtu ambaye hajawahi uona uchawi kwa macho ila akienda kwa mganga, anaafushwa anaaguliwa na kupona japo hajui hata huo uchawi unafanye kazi "ignorance" Ila bado "anaamini".
Je ignorance yako kuhusu spiritual world ndio sababu kuu ya kuthibitisha kuwa spiritual world haipo??...
Na ukitaka uthibitisho wa kisayansi. Je, hiyo sayansi ni kitu perfect cha kuthibitisha kila kitu ikiwa yenyewe tu kila siku inakuwa improved. Imagine 2023 ndio tunaanza kuachana na kutumia internet ambayo haitegemi fibers kwenye infrastructures sababu ya kutumia satellite.
What if level ya sayansi ya leo haijawa kubwa kiasi cha kuingiliana na spiritual world. Sasa vipi kama kesho ikifikia hatya hiyo, utaamini kama wale walioamini dunia ipo flat kama meza hadi pale walipothibitishiwa na sayansi kuwa ipo spherical??...
Je ignorance yako binafsi na incapacity ya sayansi iliyopo ndio conclusion ya kuwa kitu flani kipo ama hakipo??...