Je, kuna mtu yeyote aliyewahi kushuhudia na kuthibitisha uchawi? Njoo tuongee hapa!

Je, kuna mtu yeyote aliyewahi kushuhudia na kuthibitisha uchawi? Njoo tuongee hapa!

Miaka inavyozidi kwenda ndio watu wajinga wanaongezeka
Na suluhisho kuwapa watu elimu iliyo bora na sio kulaumu wanayoyafanya kwa huko kukosa kwao elimu, unakuta hadi leo bado watu wanampima mtu ukimwi kwa kuangalia muonekano wa mtu.
 
Wewe ndio unaropoka upo, hivyo thibitisha kama upo ,maneno yako ya porojo ni kama hadithi za nyeti kupotea tu , nimekupa njia za kuthibitisha bado unaleta porojo tu
Ndio maana nimesema sawa mkuu ongea wewe mimi nanyamaza maana inaonekana huwa nakukwaza sana.
 
Ndio maana nimesema sawa mkuu ongea wewe mimi nanyamaza maana inaonekana huwa nakukwaza sana.
Haunikwazi popote pale , kwanza sikujui , just mdau kama nilivyo mimi , unadai uchawi upo , thibitisha ukweli huo ili tuweze kutofautisha huu ni uchawi na hizi ni propaganda tu kama zile za nyeti kuibiwa
 
Sio hivyo tu, kwenye miaka ya 1960s watu waliaminishwa nadharia potofu kuhusu cholestrol na hadi kutiwa hofu kula vyakula vyenye cholestrol, ila baadaye ikajulikana watu walijazwa hofu kwa kitu ambacho hakikuwa na ushahidi wa kutosha wa kisayansi.
Pigia mstari ushahidi wa "kutosha wa kisayansi", Sayansi inaenda na ushahidi(facts), pia kuna baadhi ya facts za kisayansi hasa zinazohusiana na biology zinabadilika kwa sababu ya mambo mbalimbali kama vile hali ya hewa, life style, resistance na hata kupanukan kwa elimu na teknolojia.
 
Ungelifahamu hilo suala lilivyokuwa hata usingetoa majibu hayo.
 
Haunikwazi popote pale , kwanza sikujui , just mdau kama nilivyo mimi , unadai uchawi upo , thibitisha ukweli huo ili tuweze kutofautisha huu ni uchawi na hizi ni propaganda tu kama zile za nyeti kuibiwa
Sawa mkuu hakuna uchawi wewe umeshinda, umeweza kuthibitisha kuwa uchawi hakuna kama ilivyothibitika ukimwi haukuwa uchawi.
 
Ungelifahamu hilo suala lilivyokuwa hata usingetoa majibu hayo.
Nafahamu vizuri sana pia kwamba big corporations huwa zinatumia pesa kupindisha na kuchafua tafiti za kisayansi na sera za afya kwa faida zao na maslahi binafsi.
 
Sawa mkuu hakuna uchawi wewe umeshinda, umeweza kuthibitisha kuwa uchawi hakuna kama ilivyothibitika ukimwi haukuwa uchawi.
Kamfano kadogo tu haujaona wa nyeti walivyo umbuliwa ?

Ila madai ya uwepo wa uchawi umeyatoa wewe , ungefanya kuni prove wrong
 
Nafahamu vizuri sana pia kwamba big corporations huwa zinatumia pesa kupindisha na kuchafua tafiti za kisayansi na sera za afya kwa faida zao na maslahi binafsi.
Ndio hivyo mkuu tafiti hazifanywi bure hivyo majibu lazima yamfurahishe aliyetoa pesa zake, hali ndio ipo hivyo.
 
Kamfano kadogo tu haujaona wa nyeti walivyo umbuliwa ?

Ila madai ya uwepo wa uchawi umeyatoa wewe , ungefanya kuni prove wrong
Haina haja mkuu kwenye haya maisha watu wana experience zao tofauti, ndio maana unakuta watu hawaamini Mungu ila wanaamini vitu vyengine kutokana na experience yake na hicho kitu japo hakuna ushahidi wa kisayansi.

Masuala ya imani za kichawi ni mapana sana kuliko hiki kinachobishaniwa humu mitandaoni.
 
Nataka unielezee upana wake , wewe kila siku unadai hivi , tukipinga unalalamika kuna kitu hatuelewi
 
Sayansi ni ujinga tupu, eti tumeona mwezi sehemu ambayo binadamu hawajawahi ona wamejuaje kama ni upande hatujawahi ona?
Kwamba sayansi ni ujinga mtupu? 🤔
okay, unaweza kuwa sawa au usiwe sawa.
It all depends na definition yako ya maneno "ujinga mtupu"

1. "Internet!" nayo ni zao la sayansi ujinga mtupu.
2. "simu unayotumia" ni ujinga mtupu.
3. "magari" ni ujinga mtupu.
"nguo ulizovaa" ni ujinga mtupu.
4. "chanjo zote ulizopatiwa tangia umri wa miaka 0-2 ni ujinga mtupu.
5. " nyumba unayoishi" ni ujinga mtupu sabb cement, bati, nondo, ni fruits za sayansi ujinga mtupu.
6. "petrol, diesel," ni ujinga mtupu.
7. "dawa zote ulizowahi kutumia" ni ujinga mtupu.
8. "bunduki" ni ujinga mtupu.
9. "sabuni unazotumia" ni ujinga mtupu.
10. "umeme unaotumia" ni ujinga mtupu.

and the list goes on and on...

unayoiita "Sayansi ujinga mtupu" , imefanya vyote hivyo. Hebu amua japo wiki tu, uitenge sayansi ujinga mtupu na usiambatane na chochote ambacho ni matunda ya hii sayansi ujinga mtupu.

SAYANSI - systematically unaistudy nature (asili ya vitu) na kisha reasoning kwa critical thinking, ku determine kanuni zinazofanya vitu viwe kama vilivyo, kisha kutengeneza dhanio na intelligence, na kufanya jaribio kwa kuset factors zote kufuata kanuni ulizozibaini, kisha kucheki kama matokeo ili kuprove kama ni kweli au sio kweli.

Neno SAYANSI, lisiku-intimidate sana, uksona sayansi ni Mzungu, au eti ukaona SAYANSI imekuja kushindana na nini sijui, hapana,

SCIENCE - you just study the nature systematically kisha kufanya reasoning na critical thinking, bila hisia, kisha kudetermine the nature na laws zinazogovern vitu, na kanuni ambazo yeyote akifata under the same factors basi jibu litakuwa mule mule.

Again, tukisikia SAYANSI tunawaza mavitu makubwa mno, tuwaza SAYANSI ni mzungu tu, wakati tunasahau kwamba:-
  • hata kutengeneza mkaa tu ni sayansi ile, yes it can be proven.
  • hata kutengeneza pombe tu.

Just rejea definition ya Sayansi ni nini.

So, I will pick and choose science over and over again, countless times. SCIENCE ALL THE WAY!!

Imagine life la binadamu bila sayansi, aisee can't imagine.

Hebu jaribu kuishi japo kwa wiki tu bila kutumia vitu vilivyotokana na sayansi.

Mtu anajitoa fahamu kupinga sayansi, wakati maisha yake yote yana-spin na ku-revolve around science, na we can prove it kama ukibisha.

ila sio mbaya, tutaelewana tu, hata kama sio kwa kizazi hiki, ila miaka 80, 90 ijayo huko wajukuu na vitukuu zetu watakuwa wanacheka sana wakisikiliza au kusoma stori zetu kwamba:-
- "kuna watu walikuwa wanaamini katika uchawi, katika chuma ulete,
-eti kuna watu waliamini nyeti za mwanaume zilipotea kwa kushikwa bega tu" n.k.
na imani zingine za ajab ajab kama hizo, zipo kibao tu.

Most of us africans na asians, kitu tukishindwa kukielewa, tukishindwa kuking'amua, basi tunareset mindset kwenye medieval/ancient mode na tunasema ni "uchawi" hivo tu yaani. Finding a scapegoat.

Life is beautiful jamani msipotoshe watu kuwaaminisha kwamba kuna kuroga na kuna chuma ulete bila kuprove .

Acha mie niendelee kuamini katika Science, Finance, etc. Nyie bakini na uchawi wenu.
 
Nafahamu vizuri sana pia kwamba big corporations huwa zinatumia pesa kupindisha na kuchafua tafiti za kisayansi na sera za afya kwa faida zao na maslahi binafsi.
Yes, wafanyabiashara aggressive will do that just to get pesa. Hata kwenye sayansi watu wanapigwa.

The same tu kama hawa wanaoaminisha wenzao kuna uchawi, kuroga, n.k ili tu wapate wa kupiga pesa.
Penye matatizo ya mtu "A" ndipo penye fursa kwa mtu "B"

Unacreate tatizo, unaleta taharuki, halafu unajitangazia unalo suluhisho, (unapiga pesa)

Jamii ya watu wa hivi wanaowazoa wenzao huwa ni watu smart na very clever.
 
Nataka unielezee upana wake , wewe kila siku unadai hivi , tukipinga unalalamika kuna kitu hatuelewi
Nieleze tena mkuu wakati ushasema unataka uthibitisho na si maneno matupu? Unajua hata nyie mngekuwa mnatoa maelezo yenye kueleweka basi hata sie tungeona hicho mnachodai mmefanya utafiti kuhusu uchawi lakini haipo hivyo tukijaribu kuelezea mnakimbilia kudai uthibitisho.

Nimeeleza humu kuwa uchawi unahusika kwenye mambo mengi kama kesi,mapenzi,maradhi,kwenye maugomvi n.k Lakini sisi hapa hatuyajadili hayo kwa kina hapa tunazungumzia zaidi imani potofu kuliko uchawi wenyewe.

Unamwambia mtu akuroge ili ndio ukubali uchawi upo wakati unajua aina ya uthibitisho ambao mnautaka ni ule wa kisayansi tu kwa sababu tofauti na huo hamuwezi kuukubali.
 
Mapenzi ,kesi ,ugomvi maradhi unathibisha vipi ni uchawi na sio sababu nyingine tu ambazo wewe huenda haujazijua ?
 
Wazee, I'm curious kufahm hili jambo kwa undani zaidi. Nimetembea hadi Sumbawanga nikitafuta uhalisia wa mambo haya, lakini nilichokutana nacho ni simulizi tu hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaothibitisha uwepo wa uchawi.

Inanifanya nione kama hii ni sawa na stori za wanaume kuibiwa nyeti zao zinaenea sana kwa maneno, lakini ukichunguza kwa karibu, unakosa uthibitisho wa wazi na inaonekana ni oketo(ujinga).

Sasa nauliza tena kwa uwazi:
Uchawi upo kweli, au ni simulizi tu zinazojengwa na hofu, imani, au mazingira ya jamii?

Kwa upande wangu binafsi, ninaelekea kuamini kuwa ni stori tu lakini niko tayari kusikia uzoefu au ushahidi kutoka kwa yeyote aliyewahi kushuhudia hili jambo moja kwa moja.

Tafadhali toa hoja sio vitisho!
Naomba ufike Tanga wilaya ya Handeni alafu ujue ulete mrejesho.

Fika hapa
Kwa msisi
Kwadikwazu
Sindeni

Haya ni maeneo baadhi tu.

Hakurogi ufe Ila wanakuroga ujifunze.
 
Naomba ufike Tanga wilaya ya Handeni alafu ujue ulete mrejesho.

Fika hapa
Kwa msisi
Kwadikwazu
Sindeni

Haya ni maeneo baadhi tu.

Hakurogi ufe Ila wanakuroga ujifunze.
Kwa msisi kuna kitu gani hao wazigua tumeishi nao miaka na miaka hakuna kitu, na wao ni stories za kusikia tu
 
Back
Top Bottom