Davidmmarista
JF-Expert Member
- Apr 11, 2024
- 3,114
- 6,309
- Thread starter
- #101
Nadhani hili Lina ukweli flani. Na umeeleza vizuri, sayansi haiwezi ku violate laws of physics and biology in a sense watu wamasimulia.Uchawi upo na wachawi wapo ila siyo kwa jinsi ambayo wanasimulia watu.kua mchawi anaweza kupita kwenye pembe ya ukuta au mchawi anaweza kuruka na ungo au mchawi anaweza akakuonyesha mbaya wako kwenye kibuyu Kisha akamchoma kisu akafa la hasha uchawi Auko hivyo.Uchawi ni Elimu ya kuogofya watu ndiyo maana ukienda kwa mchawi lazima kwanza akuweke Ktk mazingira ya kumuogopa na ikiwezekana Dawa na mazindiko lazima mkafanye msituni au kwenye mapango makubwa hayo yote nikujenga mazingira ya kukuibia.Ukisikia mtu anaitwa mchawi ujue fika kabisa huyo mtu ni mtu mwenye Roho mbaya ,kukuwekea sumu kwenye chakula kwake ni kazi ndogo sana.Pia wachawi wanashirikiana wanapotaka kumdhuru mtu wanatumia njia zakimafia kumfikia muhusika nakupanga mipango mbali mbali itakayo weza kumuangamiza muhusika.Kuna wachawi ambao wanauwezo wakufuga Simba na fisi nakuwatuma kwenda kufanya uharibufu na madhara kwa walengwa wao, hiyo ni Elimu na science ya Mila natamaduni za Koo Fulani.Nasikia Kuna wataalamu wakutengeneza Radi ila Hilo sikubaliani nalo ila wapo wataalamu wanaweza kukuletea nyuki nyumbani kwako hao wapo,Mchawi anaweza kuwa mtu wa Dini yoyote au hata asiye na dini.ukiambiwa mtu ni mchawi kama naye mbali kwani anaweza kukudhuru bila sababu yoyote Bali tu nikwasababu ya Roho yake mbaya
Watu wanaojiita wachawi nadhani pia wapo na Wana practice rituals ambazo watu wanaziita uchawi wenyewe. Ingawa nadhani haiwezekani nipo mbali hichi tunacho kiterm kama uchawi kinifikie Iran na US wangekuwa wameshautumia siku nyingi, Tanzania tarh 29 wangekuwa wameshautumia kusimamisha zoezi na kuleta vurugu.
Nadhani ni practice kama practice nyingn either kwa kutrain wanyama may be na kutumia dawa kama sumu ambayo inaweza kuleta effect kwa mwanadamu.