Je, kuna mtu yeyote aliyewahi kushuhudia na kuthibitisha uchawi? Njoo tuongee hapa!

Je, kuna mtu yeyote aliyewahi kushuhudia na kuthibitisha uchawi? Njoo tuongee hapa!

Me nikiona mtu mzima anaamini kuna uchawi namtoa maana kabisa nakuona hana akili kabisa kasoro labda mshana huyu ndo mtu pekee anayekubali Kuna uchawi ila still nitamuheshimu tu sijui kwa sababu gani
min -me
Heshimu tu wanayoyajua wenzako tofauti na unavyojua wewe, watu hutofautiana experience za maisha mkuu.
 
Mimi nilijaribu sana kutafuta ukweli huu na sikufaniliwa.Kuna wakati niliwahi kuishi Namanyere na niliandika uzi mmoja mrefuu wa maisha yangu huko.Kipindi hicho kulivuma habari kwamba Ali Mabodi na Roki Mwanamyoto ambao walikuwa marafiki mno,kwamba ni wachawi wakubwa na walikuwa wanaogopwa mkoa mzima.Huyo Ali Mabodi wengi mnamfahamu kwa jina la Ali Kessy na aliwahi kuwa mbunge wa Nkasi.Hao watu walikuwa wanaogopwa na kuna hadithi nyingi sana juu yao.Watu walikuwa hawashikani nao mkono.Mimi nilishikana na Ali mkono na mji mzima ikawa gumzo lakini sijaona chochote kuthibitisha uchawi wao
Hapo ni sawa na mtu aamuwe kufanya mapenzi na mtu anayesemekana ana ukimwi halafu akaenda kupima ukimwi majibu yakatoka negative kisha akasema hakunaga ugonjwa wa ukimwi.
 
Ni vitu ambavyo tulivyoshindwa tu kuvieleza tu.. ndio tunaita uchawi

Chukulia utungwaji wa mimba mpaka mtoto anazaliwa.. tusingepata mchanganuo wake tungeita tu uchawi

Unalala na mtu , anapata mimba, baada ya mda anajifungua mtoto

Yaani tusingepata ufafanuzi tungesema ni uchawi.. japokuwa tumepata ufafanuzi lakini bado ni moja kati ya miujiza…

Vimaji maji tu vije kuwa binaadamu au kiumbe mkubwa tu
Yanayoelezwa hapa sehemu kubwa ni zile imani potofu tu, ila masuala ya kuhusu uchawi ni issue pana sana na ndio maana waganga wamekuwa wengi na sio kwamba watu wanaenda huko kwa waganga ili kusimuliwa story za kichawi.
 
Uzuri mmoja maujinga mnayo yaamini yanajitokeza yenywe , aya nasikia mnaibiwa nyeti
Kama unaona uchawi kiujumla ni maujinga, mbona hiyo habari ya kuibiwa nyeti imekushika sana kama kitu cha ajabu wakati ushazowea kusikia maujinga ya uchawi?

Watu wana maujinga wa kubadili jinsia kabisa wewe unashangaa huko kupotea nyeti.
 
Kama uchawi unaweza kutiwa chumvi na hata hao wachwi na waganga wasing'amue kama ni ukweli ujue uchawi ni uongo ,rejea issues za ukimwi kipindi cha nyuma
Kwahiyo sayansi ni uongo kwa sababu watu waliaminishwa uongo kuhusu cholestrol kwa kivuli cha sayansi na uongo huo ukadumu toka miaka ya 60 na wanasayansi hawakujua hadi hivi miaka ya juzi?
 
Uchawi ni hadithi za kutungwa na yale mambo yanayotokea bila kutambulika vizuri na ni kutokana na ignorance tu
Wewe unaishia kuzungumzia tu yale mambo ambayo watu wanayaona na kuyahusisha na uchawi tu, ila watu wanatumia uchawi ili kupata matokeo kwenye mambo mengi kuanzia mapenzi, kesi mahakamani huko, makazini, kwenye maugomvi,biashara n.k

Sasa wewe unazungumzia tofauti na huko kabisa, huko hakuna story ni kufanyika kitu matokeo yaonekane kama ilivyokusudiwa.
 
Kwahiyo sayansi ni uongo kwa sababu watu waliaminishwa uongo kuhusu cholestrol kwa kivuli cha sayansi na uongo huo ukadumu toka miaka ya 60 na wanasayansi hawakujua hadi hivi miaka ya juzi?
Sayansi una uwanja mpana wa kujisahisha wapi ilisema imejifungia kwenye box
 
Kuzaliwa zamani tu hakutoshi, kuna watu wana experience za maisha kushinda hata watu waliyowazidi umri kwa mbali.
Waweke uthibitisho hapa , na kama wewe ni mchawi niloge , kipi kiarabu hapo?
 
Wewe unaishia kuzungumzia tu yale mambo ambayo watu wanayaona na kuyahusisha na uchawi tu, ila watu wanatumia uchawi ili kupata matokeo kwenye mambo mengi kuanzia mapenzi, kesi mahakamani huko, makazini, kwenye maugomvi,biashara n.k

Sasa wewe unazungumzia tofauti na huko kabisa, huko hakuna story ni kufanyika kitu matokeo yaonekane kama ilivyokusudiwa.
Wewe pia unazungumzia tu hapa , weka ushahidi wa uchawi
 
Sayansi una uwanja mpana wa kujisahisha wapi ilisema imejifungia kwenye box
Kwani kuna muongozo wa uchawi ambao ndio huo pekee unafuatwa na watu wote wenye kuamini uchawi?

Watu wanaaminishwa nadharia za upotoshaji kabisa na wanasayansi wapo ila hawakuweza kuzuia huo upotoshaji ambao haukuwa na ushahidi wa kisayansi na huo ni mfano mmoja tu.
 
Uchawi ni bla bla za kijinga tu , sayansi ipo na inajirebisha sio kwamba haikosei , huo uchawi upo wapi thibitisha
 
Uchawi ni bla bla za kijinga tu , sayansi ipo na inajirebisha sio kwamba haikosei , huo uchawi upo wapi thibitisha
Nazungumzia watu kupotoshwa hapa elewa kwanza hilo, watu wanajazwa ujinga kwa kivuli cha sayansi ndio maana nasema upotoshaji na ujinga upo kila sehemu ni tofauti na mnavyotaka kutuaminisha hapa, maana naona mmeshikilia imani potofu za kwenye uchawi wakati hata kwenye sayansi watu hao hao wanaweza kupotoshwa.
 
Uchawi haupo ,miaka ya nyuma tulishuhudia kila Mtanzania akijua Ukimwi ni kulogwa unaelewa maana ya kila?
 
Mbona hata wazungu wanaamini tu uchawi na wana madarasa ya kufundisha kabisa uchawi, kuna mavitabu kibao ya wazungu wakifundisha uchawi.

Halafu afrika uchawi ni zaidi ya hicho ulichoeleza, wewe hapo umeeleza tu watu kuhusisha vitu wasivyovielewa na uchawi ila watu hujihusisha na uchawi kwa mambo mengi sana kuanzi kuhusiana na maradhi, harakati za utafutaji, kesi, kusolve mambo yao, issue za mapenzi, uzazi n.k
Kama uchawi ungekuwepo na unafanya kazi the way kama mnavyouelezea, basi USA, Israel na Iran, zingekuwa bize kutumia huo uchawi kwenye hii vita yao ya 2026.

Pia, Russia na Ukraine, huko ingetumika sana kwenye migogoro yao tangia 2022 mpaka leo 2026.

Wasingepoteza mabilioni, trilioni kwenye ICT (AI), mechanical engineering, aeronautics, rocket science, ballistic missiles, military science, etc.

Mataifa ya ulimwengu wa kwanza yametuzidi hapa (reasoning & systematic study of nature) , sisi bado majority of us africans na Asians bado mitizamo yetu ni ya ancient times. That's generally why tupo dominated na wao.

Kama umekua tangu utoto ukiaminishwa hivyo unavyoamini kwamba uchawi upo, basi ni ngumu kwangu kukuaminisha tofauti. Amini unachoamini. Acha mie nibakie kwenye sayansi.

I repeat, most of Africans na Asians ndo tumebaki na hii mindset za ancient times. Chochote ambacho tunashindwa kukielezea au kukielewa, tunasimplify tu na kusema uchawi.

Nyie ndo dizaini ya hawa watu wanaoamini katika hili swala la "mtu kukugasa bega na kisha sehemu za siri za kiume zikapotea" just like hii issue ya kindezi kabisa inavyotrend Tanzania sasa hivi March-April 2026.
 
Back
Top Bottom