Je, kuna mtu yeyote aliyewahi kushuhudia na kuthibitisha uchawi? Njoo tuongee hapa!

Vyengine ni issue za viumbe wasioonekana pia sio kila kitu ni uchawi tu.
 
Hizi porojo zako za kijinga , sina mda wa kurudia kuzijibu , thibitisha uchawi upo, hauwezi sijakulazimisha
 
Reactions: Lax
Upo fasta sana kukimbilia hilo neno thibitisha, sema mtafiti unatakiwa uwe unamalizia kusema kuwa anatakiwa kuthibitisha kisayansi nje na hapo ni mambo tu tusiyoyaelewa.
Uthibitisho sio lazima uwe kisayansi, hata kwa philosophy unaweza thibitisha.
 
Reactions: Lax
mkuu kuna zile documentary ambazo wanaonyesha wnaenda kutafuta mchawi ndani ya nyumba wanaongea nae kutumia vifaa vya frequency, au ni content tu
Sasa mkuu hata tofauti ya mchawi na ghost haujui ila upo hapa kupinga haya mambo, unadhani sisi tunapata ugumu kiasi gani kujadiliana nanyi? Halafu hamtaki tutoe maelezo mnataka tuthibitishe moja kwa moja hayo msiyoyaelewa ila mnayapinga.
 
Reactions: Lax
Upo fasta sana kukimbilia hilo neno thibitisha, sema mtafiti unatakiwa uwe unamalizia kusema kuwa anatakiwa kuthibitisha kisayansi nje na hapo ni mambo tu tusiyoyaelewa.
Wewe unayajua unashindwa vipi kufanya hivyo?
 
Reactions: Lax
Binafsi nimemuona kwa macho ndani ya chumba Cha kulala pia nimewahi shika kiganja Cha mkono wake tatu nimewahi kuonana macho kwa macho na macho gizani chumbani.
 
Reactions: Lax
Wewe mbona hujathibitisha ya kuwa Uchawi haupo kweli zaidi ya kuleta stori tu ?

Kwako wewe uthibitisho ili uwe uthibitisho inabidi uweje ?
Yeye kaishia kafanya uchunguzi sijui kazunguka kote ila hajaeleza chochote cha maana kwenye huko kuzunguka kwake kote.
 
Reactions: Lax
Uthibitisho sio kisayansi tu, hata kwa philosophy unaweza thibitisha kama huo uchawi upo kweli.
 
anawabebesha watu udongo kwenda kawe na baadae wanaurudisha shamba,

kuna mkutano alisema watu waende na passport zikaombewe ili waweze enda nje ya nchi
 
Usipende kuongea kwa hisia mkuu fuatilia, hizo imani za ghost zipo hadi sasa huko kwa wazungu na wapo watu ndio kazi zao.z
 
Reactions: Lax
Hizi porojo zako za kijinga , sina mda wa kurudia kuzijibu , thibitisha uchawi upo, hauwezi sijakulazimisha
Ingekuwa porojo hapo sawa. Lazima uwe na adabu na ushike adabu.

Umekosa sifa za kujadili huu mjadala, sababu hujui unachokipinga.

Kazi yangu nimemaliza.
 
Wanapingana wanasayansi kuhusu ukimwi.
 
Reactions: Lax
Hiv jf yote hii hakuna mchawi ajitokeze afanye demo moja ubishi uishe?
Ubishi hauwezi kuisha kwa sababu ya kuhitajika ushahidi wa kisayansi na kinyume na hivyo ni tricks tu au mambo tusiyoyajua tu ila sio uchawi, kwahiyo mnaopinga uchawi mtabaki kuwa washindi milele.
 
Ingekuwa porojo hapo sawa. Lazima uwe na adabu na ushike adabu.

Umekosa sifa za kujadili huu mjadala, sababu hujui unachokipinga.

Kazi yangu nimemaliza.
Thibitisha uchawi hauwezi tulia , mambo ya kukubaliana na wewe tafuta watoto wa chekechezea ukawaeleze
 
Reactions: Lax
nachokukubaliana na wewe mkuu ni matumizi mazuri ya neno "imani" na "kuamini"
kimsingi ukishaamini nguvu za mwanga, kuamini nguvu za giza ni direct proportional hata kama bado hujaziona hizo za giza

kupima si sayansi peke yake mfano chuma ulete mimi nikae dukani peke yangu tu siku nzima, hata kopo la kukojolea nikae nalo humo ndani tuhesabu stock iliyopo, cash at hand na kila kinachouzwa kinarekodiwa na pesa kuhakikiwa --- alafu wewe njoo na timu ya chuma elete jioni/usiku tutapata majibu chuma ulete ni kweli au story tu.
 
Ubishi hauwezi kuisha kwa sababu ya kuhitajika ushahidi wa kisayansi na kinyume na hivyo ni tricks tu au mambo tusiyoyajua tu ila sio uchawi, kwahiyo mnaopinga uchawi mtabaki kuwa washindi milele.
Ili isiwe, ajitokeze mchawi afanye demo moja , uchawi kama upo sifikiri atakosekana humu , na kama upo wanaoufanya wanashindwa vipi kuthibitisha hapa
 
Reactions: Lax
bwenini huko huko kuna wadau walikua wanawanyoa wenzao alafu watu wakiwa wanawacheka asubuhi walionyolewa kwamba wachawi ndo wamefanya hivyo hadi wanyoaji nao wanaunga kwenye tela la kucheka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…