Hatupingi uwepo wa uchawi kwa sababu hatujauona kwa macho, tunapinga uwepo wa uchawi kwa sababu ya mkanganyiko (contradictions) na matobo katika story za uchawi.
Kuhusu mfano wako wa maji ya bomba unakosa mashiko kwa sababu maji ni maji tu, kama mtu ameweza kuona mbao au tawi la mpapai likipitisha maji hawezi kushindwa kuelewa chuma au plastic ikipitisha maji.
Zaidi sana Dunia ya Leo Kuna teknolojia ya kunasa picha na sauti.
Pia story za Sayansi za bomba la maji, umeme, gravity, satellite, internet na protozoa ni zile zile, hazibadiliki, ziko constant na replicable miaka yote na sehemu zote duniani sio kama story za uchawi ambazo hata ku define tu uchawi wenye ni tatizo na kila mtu ana experience zake tofauti za uchawi na exceptions kibao.
Hizo story za Satellite, gravity, internet, micro organisms ni vitu vipo widely accepted kwa sababu vimekuwa normalized kwa sasa. Ila kuna kipindi hazokuwepo duniani
Mtu wa karne ya 5 ungemuambia kuhusu umeme, ndege kupaa angani ama satellite, angeona unamuambia vitu vya kufirika kwa sababu havipo katika uwepo wake.
Ndio ilikuwa point yangu hapo. Sio ACCEPTANCE ila EXISTENCE
Wewe umeiweka kwenye ACCEPTANCE and ADAPTION.
Kiufupi, hata katika business kuna innovators, hawa ni watu wanaoichukua na kuitumia bidhaa mwanzoni kabisaa, na kuna laggards, hawa wanatumia bidhaa ikishakuwa imetumika na watu wengi na mara nyingine imeshakuwa sehemu ya culture flani.
Wewe ni innovator kwa upande wa sayansi na unaviona vyote ni rahisi na umevikubali. Lakini kuna mtu madongo kuinama, ukimuambia kuna infrastructure ya umeme ambayo itatokea kwenye satellite. Atakushangaa kwa sababu pengine hata smartphone hajawahi kuitumia
Lakini mtu huyo huyo anaijua mitishamba kukuzidi na pengine, anajua akipata tatizo flani ataenda kwa mganga au kwenye visomo. Atapigwa makombe na atakaa sawa pasipo kutumia dawa za hospitali etc..
Huyu mtu ukimleta kwenye sayansi ataona unazungumza vitu vigumu kwake kwa sababu unatumia lugha ya sayansi kumuelezea lakini pia naye akikuambia yake, ndio hayo utaona pia ya kufirika kwa sababu unataka kutumia njia na maelezo ya kisayansi kuuelezea uchawi ulivyo.
Hawa watu wawili wakikaa sehemu moja si rahisi kukaa sawa..
Na unavyosema vitu kuwa tofauti kutokana na maeneo tofauti.
Je, kwani lazma kuwe na uniformity,
Kwani kuwepo kwa diversity katika kitu flani kilichopo katika sehemu tofauti na kuendeshwa na watu tofauti. Ni conclusion kuwa hiyo inconsistency inaonesha kuwa hicho kitu hakipo...
Kama dunia ilianza na gunpowder huko Asia, je ni sawa na teknolojia iliyotumika kutengeneza silaha za nyuklia
So kama teknolojia inaweza kutofautiana sehemu moja na nyingine. Japo principles na foundation yake inaweza kuwa sawa. Je kwa nini utegemee uchawi wa Wasukuma ufanane na uchawi wa wahausa ijapokuwa nia na msingi wake ni mmoja
Kwa nini unataka explanations za ushirikina ziwe sawa ilhali hata sayansi haipo sawa dunia nzima. Ndio maana kuna mataifa yanavumbua na mengine yanatumua tu