Ushirikina hauna formula wala principles zake, coz vitu vyenye formula na principles vinathibitishika beyond reasonable doubt.
Kama ungekuwa na formula, wala tusingekuwa na hii conversation muda huu.
So, unatuaminisha wewe ulitumia ufahamu wako? Wakati kwenye post hapo chini umekiri kwamba ndo ulikuzwa hivyo kwenye kuamini uchawi na ushirikina.
Kwa kifupi, ukitulia utaona kwamba wanaokataa uchawi ndo haswa wanaotumia ufaham wao coz wamekataa kuaminishwa vitu potoshi vinavyochonganisha watu bila ushahidi zaidi ya stori za hearsay tu.
Ulichoki-type hapo umejileta mwenyewe kwenye point yangu.. Sabb umekiri hapo kwamba vitu ambavyo watu wakishindwa ku reason ndo wanadai ni uchawi, just finding an excuse.
As you said, "kwa makuzi yako, utaendelea kuamini uchawi na ushirikina"
so unakubaliana nami kwamba na wewe umekaririshwa kuamini, kama ambavyo umesema mimi nimekaririshwa sayansi.
Tatizo wote mnaopinga huwa mnatafuta nyufa za kutengeneza attacks.
Mnajaribu kuhalalisha kuwa "sijui ninachokiongelea"
Nimekaririshwa, nimeaminishwa na mimi nikaamini.
Ukiweza soma post zangu za nyuma
Actually nipo open minded. Naweza kuwa mkristu ila hainifanyi nisijue nguvu ya visomo na hata baadhi ya principles za uislamu. Na hata sababu ya kujiunga jf , ni kwa sababu nilivutiwa na ideas za atheist Kiranga
Pia naweza kuwa ni graduate lakini haimaanishi sijui vitu ambavyo kwa graduates ama wasomi wengi wanaviona kama vya kipuuzi kwenye jamii zao
Again, sijakuzwa sehemu moja,
Nimekuzwa kwa kuishi maeneo tifauti hii nchi kwa hiyo sikuwa programmed kufikiri navyofikiri. Kwa hiyo Nilichoamua kuamini ni kutokana na mambo nilioyaona na niliyoyathibitisha. Aidha kwa experience yangu binafsi ama ya watu wangu wa karibu.
Huwa nipo curious, na napotaka kujifunza, simfanyi mtu anaeniambia kitu ajihisi kuwa yeye ni mpumbavu. No
Nakaa chini na nijikuza au kujishusha kwa level itakayomfanya yeye kuwa comfortable..
Nikikuambia nishafuatilia hadi mizimu japo kwa sasa watu hawajali. Je, wewe umeshawahi fikiria hilo
Mimi nipo curious by nature, sio kwamba na_fake ili nionekane intelligent ama msomi. Na zamani nilikuwa Narendr kufuatilia history na nilikaa na wazee. Wanakusimulia vitu ambavyo hata havipo documented.
Na tabia ya kujifunza ni kuwa open kupokea unayoambiwa na kuyachuja ili uone ukweli na uongo ni upi .
Naamini katika spiritual world, naamini ipo, nimeshakutana nayo and unless uzame kwenye spiritual world kwa kufuata system na principles zake ambazo wewe huamini kama zipo. Huwezi kujua