Mkuu kuamini tu sio ishu, mtu unaweza kuamini chochote, jambo la msingi je ni "fact".
Hitler na Nazi walikuwa wanaamini Aryan au Wajerumani ni master race, Wayahudi na Wakristo wengi wanaamini Wayahudi ni taifa teule(chosen people), Kuna wakati Wazungu na Waarabu walikuwa wanaamini sisi Waafrika sio binadamu kamili, Kuna kipindi watu walikuwa wanaamini jua linazunguka dunia hadi wakamuua Galileo aliposema Dunia ndio inazunguka jua, watu walikuwa wanaamini hewa chafu ya mvuke(miasma theory) ndio ilikuwa inasababisha magonjwa mbalimbali kama Malaria, homa, ukoma, kipindupindu n.k