Germany, Na nchi nyingi bara la ulaya wanautambua uchawi, Na kipo chuo cha uchawi ( Humo wanafundishana rituals na mambo mengi )
Kwahiyo tengua kauli kuwa ni Africa na Asia
tulia kijana.
sitengui kauli, kwanza elewa maana ya "wengi (majority)"
soma tena mara tatu tatu bila kukurupuka.
Kuhusu hiyo ya Europe, kuna mwenzio alikuja na hoja kama hiyo na nilishamjibu na hajarudi tena.
Rejea replies zilizopita utapata jibu lako.
ipo hivi, Europe miaka ya 1400-1700 nao walikuwa na imani hizi potofu, na watu walipoteza maisha kisa tu watu kusema flani ni mchawi (imagine mtu ulikuwa ukipata shida tu basi unasema flani kaniroga na huyo flani anaadhibiwa na nchi),.. ila baadae reasoning, logical sense na science iliwasanua watu.
So, kinachofundishwa kwenye hizo kozi ni "Historia na athari za imani hizo potofu zilikuwaje Europe kipindi kile na impact zake" na wanashangaa sana kwamba kw nn Africa still mpk sasa watu wengi bado wanaamini ktk huu upuuzi.
Hence, hayo masomo unaweza kuyafananisha kama tu kwetu tunavyofundisha "Historia ya Ukoloni faida na athari zake negative, ili watu wajue wapi tulitoka ili tupange yajayo"
Binafsi, ningependa hizi Elimu/kozi zianzishwe kwenye shule za TZ just kama walivyofanya baadhi ya nchi Europe kuwa na hizo kozi ili watu wengi waelimike, waache kuamini upuuzi.
Hebu, ona sasa mtu anaamini eti "ukiguswa bega tu nyeti zinapotea" . Aisee!
Kuna kipindi watu wameua ma-albino kisa imani hizi hizi, aisee so sad!
Yaani uchawi uwepo afu USA, Israel, Iran, Russia,
Ukraine wapoteze matrilioni kwenye ballistic missiles na Air defense systems? 🤔
Si wangetumia tu huo uchawi kurogana.
Coz sio siri wao ndo wangekuwa mamaster kuliko sisi.
TZ hapa kama uchawi ungekuwepo, ungemtumia sana kwenye vurugu za uchaguzi Octoba 2025 ila nilichoona ni vitu vya kisayansi tu (bunduki, n.k) ..
Mkuu, Acha kuwa primitive
mzee usiturudshe enzi za vita ya maji maji.