Je, kuna mtu yeyote aliyewahi kushuhudia na kuthibitisha uchawi? Njoo tuongee hapa!

Labda nikuitie poti UMUGHAKA tokea pande za Mogabiri kule tunakonunua ndizi sisi majirani, AJE AKUTHIBITISHIE!
Mkuu huyo mleta mada inapaswa aeleze anatafuta uchawi wa namna gani?,Yeye anadhani uchawi unashikika?au anadhani mtu mchawi anajitangaza?

Anaenda kwa waganga matapeli wanamlia hela halafu anasema uchawi haupo?,Ni kama mademu ambao wanatendwa na wanaume vichaa kisa anasema "Wanaume wote ni sawa"

Uchawi ni siri,Mchawi hawezi kukwambia yeye ni mchawi!

Bahati nzuri nimeishi na kuyashuhudia hivyo ninasema UCHAWI UPO
 
Mkuu unaweza kuthibitisha tukio/issue ya uchawi ambayo itatupa majibu mazuri ya research yetu?
 
Kama wewe mwenyewe siye, bhas itakuwa tayari wamesha kuchezesha... Ndio Iko hivyo tu kwa watu wenye mada zenye maudhui ya aina Yako hii.
 
Mimi nilijaribu sana kutafuta ukweli huu na sikufaniliwa.Kuna wakati niliwahi kuishi Namanyere na niliandika uzi mmoja mrefuu wa maisha yangu huko.Kipindi hicho kulivuma habari kwamba Ali Mabodi na Roki Mwanamyoto ambao walikuwa marafiki mno,kwamba ni wachawi wakubwa na walikuwa wanaogopwa mkoa mzima.Huyo Ali Mabodi wengi mnamfahamu kwa jina la Ali Kessy na aliwahi kuwa mbunge wa Nkasi.Hao watu walikuwa wanaogopwa na kuna hadithi nyingi sana juu yao.Watu walikuwa hawashikani nao mkono.Mimi nilishikana na Ali mkono na mji mzima ikawa gumzo lakini sijaona chochote kuthibitisha uchawi wao
 
Uchawi upo na wachawi wapo ila siyo kwa jinsi ambayo wanasimulia watu.kua mchawi anaweza kupita kwenye pembe ya ukuta au mchawi anaweza kuruka na ungo au mchawi anaweza akakuonyesha mbaya wako kwenye kibuyu Kisha akamchoma kisu akafa la hasha uchawi Auko hivyo.Uchawi ni Elimu ya kuogofya watu ndiyo maana ukienda kwa mchawi lazima kwanza akuweke Ktk mazingira ya kumuogopa na ikiwezekana Dawa na mazindiko lazima mkafanye msituni au kwenye mapango makubwa hayo yote nikujenga mazingira ya kukuibia.Ukisikia mtu anaitwa mchawi ujue fika kabisa huyo mtu ni mtu mwenye Roho mbaya ,kukuwekea sumu kwenye chakula kwake ni kazi ndogo sana.Pia wachawi wanashirikiana wanapotaka kumdhuru mtu wanatumia njia zakimafia kumfikia muhusika nakupanga mipango mbali mbali itakayo weza kumuangamiza muhusika.Kuna wachawi ambao wanauwezo wakufuga Simba na fisi nakuwatuma kwenda kufanya uharibufu na madhara kwa walengwa wao, hiyo ni Elimu na science ya Mila natamaduni za Koo Fulani.Nasikia Kuna wataalamu wakutengeneza Radi ila Hilo sikubaliani nalo ila wapo wataalamu wanaweza kukuletea nyuki nyumbani kwako hao wapo,Mchawi anaweza kuwa mtu wa Dini yoyote au hata asiye na dini.ukiambiwa mtu ni mchawi kama naye mbali kwani anaweza kukudhuru bila sababu yoyote Bali tu nikwasababu ya Roho yake mbaya
 
habari hizi umetoa wapi mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…