Wanabodi,
Jee Kuna Uhusiano Kati ya IQ, Dini ya Mtu na Longevity?. Naomba Kuwatumia Marais wa Tanzania as Sampling factors.
Haya ni maswali valid yanayo hitaji majibu ya utafiti wa kina.
Tanzania tumebahatika kuwa na marais 6.
- Julius Kambarage Nyerere
- Ali Hassan Mwinyi
- Benjamin William Mkapa
- Jakaya Mrisho Kikwete
- John Pombe Magufuli
- Samia Suluhu Hassan
Dini Zao
- Mkiristu
- Kiislamu
- Mkiristu
- Muislamu
- Mkiristu
- Muislamu
Hapa kwenye Dini zao, naona kama kuna kupokezana kati ya Mkiristu na Muislamu, jee is it planned au imetokea tuu?. Kama ni planned, then anayefuata ni lazima atoke upande wa pili. If it just happened, then anaweza kufuatiwa na wa kutoka upande wowote.
Denominations zao
- Mkiristu RC
- Muislamu
- Mkiristu RC
- Muislamu
- Mkiristu RC
- Muislamu
Kwa Wakristu, rais akiwa Mkiristu je ni lazima awe RC?. Kwanini wote walioshika urais ni RC only?. Is this planned or it just happened?.
If it's planned ni nani anayepanga?. Hivi Wakristu wa dominions nyingine kama Lutherans, Anglicans, Wasabato, Walokole etc hawawezi?.
Kwa Waislamu, Tanzania tuna Sunni, Issmailia Ahamadia, wale Mabohora, jee nao kuna siku watapata zamu?.
Uhai wao
- Amekufa
- Yuko Hai
- Amekufa
- Yuko Hai
- Amekufa
- Yuko Hai
Jee kuna uhusiano wa dini fulani na longevity?. Kwanini ni marais wa dini moja tuu ndio wametangulia, lakini wa dini nyingine wote wapo?.
Elimu Zao
- Straight to University Masters Level
- Aliunga Unga ila alipata Masters
- Straight to University Masters Level
- Aliunga Unga Ila alipata Bachelor ya GPA flani
- Straight to University Ph.D iliotiliwa shaka humu JF, (mtia shaka just vanished into thin air)
- Aliunga Unga to Masters
Jee kuna uhusiano wa IQ na dini ya mtu?.
Kwa nini watu wa dini fulani shule imesimama, halafu wa dini nyingine ni shule za kuunga Unga?.
Matumizi ya Busara
- Busara Sana
- Busara Sana na ustaatarabu
- Hakuna Busara Ila Ustaatabu
- Muungawana, Busara, Ustaarabu
- Hakuna Busara, Uungwana wala Ustaarabu
- Busara, Uungwana, Ustaarabu Ila na Mipasho!.
Kwanini watu wa dini fulani ndio wanaonekana na busara zaidi kuliko wa dini nyingine?. Jee kuna uhusiano wa dini ya mtu na busara?
Dhana ya Udikiteta
- Dikiteta
- Hakuwa Dikiteta
- Dikiteta
- Hakuwa Dikiteta
- Dikiteta
- Sio Dikiteta
Viongozi wetu madikiteta au wenye udikiteta ni wa dini fulani tuu!. Jee kuna uhusiano wa dini na udikiteta?.
NB. Ni wakati naliandika bandiko hili ndio nikaisikia hii sauti
Wanabodi Haya mambo ya mtu kusikia sauti, sio mambo ya ulimwengu huu wa mwili, haya ni mambo ya ulimwengu wa Roho. Hii ni thread ya maono tuu ya unabii, sio utabiri, sio trends readings, ni unaisikia tuu sauti inakuambia jambo fulani bila kukuambia sababu za jambo hilo, na huwezi kuuliza, hivyo...
Paskali