Je, kuna uhusiano kati ya IQ ya mtu na kabila lake, umasikini wake au kimo chake?

Je, kuna uhusiano kati ya IQ ya mtu na kabila lake, umasikini wake au kimo chake?

Pascal Mayalla Ni wazi Juma Nkamia ana IQ ndogo sana, kwa kuanzisha issue ambayo haina mashiko wala msukumo, isipokuwawa kwake mwenyewe.

Na naona Pasko umejitahidi kuleta ulinganishi wa makuzi na matunzo kiafya yanavyoweza kuathiri afya ya akii.

Juma Nkamia kama ulivyo elezea , sidhani kama ana afya njema sana kiakili kutokana na makuzi yake au kule alikotoka.
Ingawaje ukiligeuza geuza waweza kusema argument imekaa kibaguzi.

Hata hivyo wataalam wa afya wamesha sema usipopata mlo wenye kuleta afya, hata akili yako inadumaa.
Juma Nkamia n mfano hai!
 
Hoja ya umasikini kuwa tatizo la IQ ndogo sikubaliani nayo. Nimesomaga shule ya msingi kata, wanafunzi waliokuwa wanafanya vizuri darasani, walitoka ktk familia duni sana, shule yenyewe walikuwa wanakuja peku.

Kuna familia mbili jirani zetu maisha yao ni duni ila watoto wote wa familia hizo walifaulu vizuri mitihani yao ya darasa la saba, familia moja kwa msaada mkubwa wa ndugu jamaa na marafiki ilifanikiwa kusomesha watoto wote 5 ila hii famikia nyingine ilisomesha 1 tu kati ya 4.
 
Factor za ufaulu Tanzania sio swala la IQ. Kuna vitu vingi sana ikiwemo social influence na mazingira na kuwepo kwa option. Mfano maeneo ya pembezoni mwa bahari wengi wanakula samaki ambapo biologically lazima wawe na akili nyingi, tatizo pesa za mazao ya bahari hasa kipindi cha utoto inawapumbaza.

Lakini angalia mifumo na mazingira ya elimu na usomeshaji pia. Kuna maeneo kupitia wakoloni walikuwa moved on mapema kama wachaga na wala sio issue ya IQ. Hakuna standard sawa katika elimu kwahiyo ondoa kigezo cha matokeo ya mitihani.
 
Sidhani kama issue ya Low income inakuwa determined na Kabila au UKANDA atokao mtu.Ila kujiamini kunaweza kukawa au kukaletwa na familia husika.

Mfano Mzazi Mchagga anaweza kumwambia mwanae na kusomesha mpaka kidato cha nne ukifeli nenda katafute maisha usitegemee pesa yangu,na kijana akifeli kweli asitegemee Mzee atarudi kumsaidia,ndiyo imetoka hapo unakuta kijana anajiingiza kwenye biashara mpaka anatoboa na kikubwa ni kujiamini.

Wengi wanaotoka huko kwa akina Juma Nkamia wameshindwa kujiamini,na anachokosa Nkamia ni kujiamini.Kwa maeneo ya Pwani,Tanga na Zanzibar nadhani tatizo lililowakumba ni kukosa opportunities,wahindi na waarabu walibase kwenye biashara zaidi na kufundisha dini kuliko ELIMU dunia lakini wakipata nafasi wako vizuri.

Hivyo Shemeji yangu PAscal IQ ya mtu inategemea vitu vingi sana hasa kwenye familia na eneo husika.Kuna maeneo waliwalea mabinti zao kwa kuwaaminisha wao ni viumbe vya kuolewa tu na si kwenda shule,lakini waliotoka kwenye familia zilizopata uelewa mapema familia hizo zimetoboa kiuchumi.

Mila na desturi pia zimechangia kufanya maeneo mengine masikini hasa imani za kishirikina.Hope mtanielewa,nimetaja baadhi ya maeneo sababu nimekaa maeneo hayo kwa kipindi kirefu kama miezi sita hadi miaka 10.
 
Wewe ndo unazidi kuonyesha hata usivyoelewa Historia yetu, hakuna kitu kama Kabila la Wanyamwezi Dunia hii kama vile ilivyo kuwa hakuna kabila la Wachaga, Wahaya au hat Wagogo!

Hao wanaojiita Wanyamwezi siyo Kabila, kwanza unajua ni kwa nini wanaitwa Wanyamwezi? Hilo jina walipewa na watu wa Pwani wakati wa Biashara ya utumwa na Pembe za Ndovu, enzi za makaravani ktk Kongo mpaka Pwani, hivyo kabla ya kuanza kwa Biashara ya makaravani watu waliokuwa wanaishi hilo eneo hawakujiita Wanyamwezi kwa maana nyingine hilo unaloliita Kabila la Wanyamwezi halikuwepo kama vile Wagogo inatokana na magogo yaliyokuwa kwenye njia ya karavani sasa watu eneo hilo wakaitwa Wagogo lkn siyo Kabila ni kwamba imezoeleka hivyo tu, hata Wachaga ni hivyo hivyo siyo Kabila bali ni makundi ya watu mbali mbali yanaoyoongea lugha mbali mbali yaliounganishwa na Muzungu (Mjerumani) na kuitwa Wachaga!!
Wewe unamatatizo kwahiyo zile jamii za kiafrika zilizo zungumza lugha moja na kuwa mila moja unaziitaje?
 
Lishe bora kuanzia utotoni na maisha yote ya shule na ukuaji.
Malezi bora toka utotoni, makazi bora, mazingira mazuri ya nyumbani.

Hivyo ni vitu muhimu sana kutengeneza na kukuza IQ.
Tofauti na hapo ni MUNGU mwenyezi na rehma zake..
 
Pasckali usiseme 2020 upinzani utakufa shauri ya magu kuipeleka nchi ktk uchumi wa kati sema kwa sababu ccm inasaidiwa na police na tume ya uchaguzi na wasimamizi ni makada wa ccm.na kama magu anajiamini aachie democrasia na mikutano ya vyma kama katiba ilivoruhusu.mbona ccm wanafanya .achie bunge live .aweke tume huru ya uchaguzi uone .yéyé anapigna na kmafunga miguu namikono anashinda anaashangilia .ccm ni wepesi kam tissue wafanye hhvo uone wanaondoka asubui .wanajidanganya wanapendwa waachie demokrasia uon
 
Uzi wako mwanzoni unafurahisha na kuvutia lakini ukifikia mahali unapoanza kutaja makabila kwa kuainisha yale yenye high IQ Didi ya yale yenye low IQ, mbaya zaidi ukigeneralise eti wagogo, wataturu nk, umeniudhi na kunifanya nijisikie kichefuchefu kabisa!!!
 
Wewe ndo unazidi kuonyesha hata usivyoelewa Historia yetu, hakuna kitu kama Kabila la Wanyamwezi Dunia hii kama vile ilivyo kuwa hakuna kabila la Wachaga, Wahaya au hat Wagogo!

Hao wanaojiita Wanyamwezi siyo Kabila, kwanza unajua ni kwa nini wanaitwa Wanyamwezi? Hilo jina walipewa na watu wa Pwani wakati wa Biashara ya utumwa na Pembe za Ndovu, enzi za makaravani ktk Kongo mpaka Pwani, hivyo kabla ya kuanza kwa Biashara ya makaravani watu waliokuwa wanaishi hilo eneo hawakujiita Wanyamwezi kwa maana nyingine hilo unaloliita Kabila la Wanyamwezi halikuwepo kama vile Wagogo inatokana na magogo yaliyokuwa kwenye njia ya karavani sasa watu eneo hilo wakaitwa Wagogo lkn siyo Kabila ni kwamba imezoeleka hivyo tu, hata Wachaga ni hivyo hivyo siyo Kabila bali ni makundi ya watu mbali mbali yanaoyoongea lugha mbali mbali yaliounganishwa na Muzungu (Mjerumani) na kuitwa Wachaga!!
Wacha kuchanganya madesa wewe, wanyamwezi siyo kabila? Ni nani sasa hao?
 
Hivi kwa mfano Mikoa kama ya Mara, Kagera, Mwanza na Shinyanga utawapataje kweli Watu Wajinga / Mangumbaru? Hivi unawezaje kwa mfano ukawa unakula Samaki aina za Sato na Sangara pamoja na Ugali wa Mtama, Muhogo na Ulezi halafu ukawa goigoi Kichwani? Watu wa Kanda ya Ziwa ' wamebarikiwa ' sana na Mwenyezi Mungu.
 
Ndg Mayalla. kwa Ujuzi wangu katika maisha nimegundua Hakuna mwanadamu Maskini, ila umaskini uanzia kichwani na matokeo udhiirika mwilini, ukitaka kuwa Bilionea Badili fikra zako jinsi unavyowaza, na ukitaka kuwa maskini endelea kuwaza kushindwa na kulalamika utakuwa maskini wa kutupwa.

Siku zote fursa za kufanikiwa uwa zimesitirika sana uonekanatu kwa wale wanao waza kinyume na mazingira.huwezi kuwa tajiri kama fikra zako hazikubaliani wewe ni tajiri,unapoanza kuwaza tofauti na kujitamkia maneno ya ushindi na kufanikiwa kamwe mwili wako hautoweza kutoa ushirikiano wa kutekeleza yale unatoyakiri maana maneno ni Nguvu na Mwongozo wa mwili.

computer kama chombo uendeshwa na program zilizoingizwa ndani yake! vivyo mwili utegemea mawazo kujiendesha, hivyo ukitaka kuwa tajiri utajiri uanzia kichwani na mwili ni mtekelezaji. watanzania wanalalamika Vyuma vimekeza!!!!! uo ni uvivu wa kufikiri unaopelekea kuzubaa kwa mwili katika kuona fursa na kutengeneza fedha. Mimi Binafsi Nampongeza sana Mh Magufuli. kwa kuwafanya watu wafikiri zaidi na kufanya kazi. Taifa hili lillikua Watu hawafanyi kazi na kupelekea kuwa Taifa la watu Tegemezi.

Mimi Tangu Rais Magufuli Aingie Madarakani nilibadilika Kufikiri kwangu Kulikopelekea Kunifanya Nifokasi zaidi kwenye Biashara zangu kulikopelekea Kuwa Bize Muda Wote na Kutengeneza Pesa Nyingi sana kwa Muda Mchache kabisa, hivyo kama unataka kuendelea kuwa maskini wewe ilaumu Serikali Mwanzo wa Asubui mpaka jioni na kumtukana Mh Rais na kuhakikishia utakuwa mtumwa na homba hoba katika nchi yenye utajiri mkubwa ila watu wake ni maskini wa fikra.

Nakutakia Siku Njema Ndg Paskali.
 
Hata kuchagua hawa wabunge hebu tufuatilie akili za waliowachagua, huenda huko ndio kuna tatizo kubwa zaidi ya tunavyofikiri.
 
Pascal unakoendea lazima utaanza kupiga ramli, hata waganga nguli wa kienyeji walianza hivi hivi kuhoji hoji mambo hasa yasiyoonekana.
 
Paskali kuna uhusiano mkubwa wa IQ na kabila au taifa la mtu, mazingira ya maisha ya binadamu huyo kwa wakati fulani.

Mfano ulio hai ni kabila la wayahudi mchango wao ni mkubwa sana kwenye nyanja ya sayansi,tekinologia na sanaa japo ni watu wachache sana duniani ukilinganisha na wahindi,wachina,waindonesia,wazungu na waafrika.

Kwetu Tanzania kuna watu wana vipaji vya ushawishi wa jambo fulani kwa njia au lugha rahisi na sahihi likaeleweka na kukubalika kwa jamii japo huyo mtu hana elimu ya shuleni au vyuoni.

Kwa mfano mwandishi nguli wa vitabu vya Kiswahili marehemu Shaaban Roberts alikuwa chosa ni wazi alikuwa na IQ kubwa japo hakuwa na elimu ya chuo lakini vitabu vyake vinatumika kufundishia kiswahili katika vyuo vikuu mbali mbali duniani.
 
Back
Top Bottom