Je, kwa mshahara wa Shilingi 310,000 unaweza kuishi Dar es Salaam?

Je, kwa mshahara wa Shilingi 310,000 unaweza kuishi Dar es Salaam?

Nadhani unaweza anza nao mkuu, huku ukipambana kupata zaidi, wanasema bora kitu kuliko kukosa kabisa. Na inabidi usikae mbali sana na sehemu ya kazi maana hiyo pesa inaweza ishia kwenye usafiri tu. Maisha haya unalamba laki 3 na kuna wengine wana hadi 10M na kuendelea 😪 ila yote maisha
 
Mungu ni mwema sana, hiyo kazi imenipa kumbukumbu muhimu sana katika maisha yangu, niliweza kusafiri hadi bara jengine, nimepanda usafiri wa aina tofauti kama Dreamliner, SGR, treni za underground, mabasi ya mwendokasi yanayotumia umeme. Kikubwa ni kumuomba Mungu, pia uvumilivu wakati mwengine huleta mafanikio
 
210k, una familia, hivi unaishije serious....japo nami naishi ila sijui naishije [emoji23][emoji23][emoji23] nadhani huu ni muujiza tosha, sihitaji miujiza tena kwenye maisha yangu

210K buguruni unapata double room kwa 70K inayobaki maji na umeme plus chakula maisha yanasogea
 
Watanzania wanamatizo Sana , ndio maana magabachori hawaishi kuwatumikisga kama slaves Kwa ujira WA ovyo kuliko maelezo na manyanyaso juu ,makondoo ni wengi .
We mtu unakubali vipi kulipwa mshahara chini ya laki SITA Kwa Maisha haya ya sikuhizi kila kitu ghali like how ? Tena huo mshahara WA laki SITA ni unlivable wage , hakika Tanzania ni taifa la Manamba
Mkuu sidhani kama kuna mtu anapenda mshahara mdogo ila kuna mda inafika unakosa options zingine kabisa, imagine ajira zilivo ngumu ukapata offer ya chini ya 600k unadhani utaiacha kweli? Kujiajiri bila pesa pia changamoto. Nikikumbuka msoto wa kutafuta ajira aah nilikua Tayari hata kulipwa 200,000/=
 
Ndio maana dsm watu muda wote wako na hasira ,...

Sasa 200k kwa mwezi mtu unaishi vipi na unafamilia [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
😀 umenikumbusha kwenye daladala leo nimemgusa mbaba huyo bahati mbaya dah kanikata jicho la hasira hilo 🙌
 
Back
Top Bottom