Je, kwa mshahara wa Shilingi 310,000 unaweza kuishi Dar es Salaam?

Je, kwa mshahara wa Shilingi 310,000 unaweza kuishi Dar es Salaam?

Kuna siku nilikua naongea na mtu haya mambo ya kipato, akawa ananipigia hesabu kiukweli ni za kufikirika, eti sukari kwa mwezi kilo 1 hivi kilo moja ya sukari inakataje mwezi jamani kwenye familia?

Ndio zile hesabu za shamba unaweka milioni moja unalima unapanda unavuna faida unapata mil 13 ukitoa garama nyingine inabaki mkononi na m12
Inawezekana chai inanywewa wikend tu siku za kawaida haipikwi kwa kuwa watoto wako shule.
 
kwangu natumia kiasi hicho ndo bili ninayolipa ila nimekuwa mpare kidogo
kwanza marufuku kutumia maji kabla hayajakingwa
vyombo havioshi na maji ya moja kwa moja bombani kwa kuwa kawaida yenu glass imetumika kwa kumpa mgeni mara moja lakini inaweza kuoshwa kwa glass tatu utaratibu huu wengi niliowafundisha wamepunguza gharama kwa zaidi ya 50% pia unapofungua maji fungua yatoke taratibu ili usiruhusu upepo uingie katika bill ya maji upo hapo
Aseee[emoji848][emoji849][emoji16]

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
310,000 mbona inatosha japo ni ngumu kufanya saving,kodi ya chumba na sebule medium quality 60000,umeme na maji 10000,chakula unasaga debe 2 za unga kila debe maximum 15000x2 ni 30000,maharage kilo 5x2000 ni 10000,mchele kilo 20x1200 ni 24000,mafuta Lita 5 ni 25000,mkaa nunua gunia moja 50000,gesi 25000 JUMLA NI 234000 hivyo ukiitoa kwenye 310000 itabaki 76000,suala la afya kata bima ya familia 54000 kwa mwaka,itabaki 22000 hii ya kubadilishia mboga kwa mwezi.Nauli kazini itabidi uwe mdau wa tz 11,suala la mavazi ni anasa,chai asubuhi ni anasa,king'amuzi ni anasa,bia ni anasa,kuhonga ni anasa, kutoa sadaka Mungu ndio anajua hali yako atakusamehe,YAANI KIFUPI UTAISHI KAMA SHETANI au nasema uongo ndugu zangu
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Inawezekana chai inanywewa wikend tu siku za kawaida haipikwi kwa kuwa watoto wako shule.
Umenikumbusha zamani tulikuwa tunawadai wazazi hela ya shule tsh 20 ambayo kwa sasa watoto kwenda shule wanapewa buku.Ss usiombe huwe na watoto wengi .Ss hivi nimekua ndio nimeanza kumuonea huruma baba alijinyima sana,kipindi hicho usipopewa hela ya shule unagoma kwenda shule😂😂😂
 
Mshahara wangu ni sh 220,498.16/= Ila Nina mke mmoja na watoto wawili wa kiume na hapa naandika hii comment nimetoka kununua kilo moja ya nyama kwa sh 5000/= ,nimejenga kajumba ka 2 rooms na sebule,sijawahi lala njaa.

Ukubwa wa mshahara sio kipimo Cha maendeleo Bali ni mipango tu mkuu,pambana utatoka
Acha kutufanya sisi watoto wadogo wewe[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
310,000 mbona inatosha japo ni ngumu kufanya saving,kodi ya chumba na sebule medium quality 60000,umeme na maji 10000,chakula unasaga debe 2 za unga kila debe maximum 15000x2 ni 30000,maharage kilo 5x2000 ni 10000,mchele kilo 20x1200 ni 24000,mafuta Lita 5 ni 25000,mkaa nunua gunia moja 50000,gesi 25000 JUMLA NI 234000 hivyo ukiitoa kwenye 310000 itabaki 76000,suala la afya kata bima ya familia 54000 kwa mwaka,itabaki 22000 hii ya kubadilishia mboga kwa mwezi.Nauli kazini itabidi uwe mdau wa tz 11,suala la mavazi ni anasa,chai asubuhi ni anasa,king'amuzi ni anasa,bia ni anasa,kuhonga ni anasa, kutoa sadaka Mungu ndio anajua hali yako atakusamehe,YAANI KIFUPI UTAISHI KAMA SHETANI au nasema uongo ndugu zangu
Unaishi zaidi ya shetani ....

Kuifupi lazima uisome namba kweli kweli
 
Wengi hawazijui, chai mnakunywa saa sita mchana na kiporo Cha Jana Cha ubwabwa na maharage , mkitoka hapo tukutane Tena usiku..
Kama jana mlikula ugali hamna kipolo,Foleni za vibakuli za mihogo zinatusaidia ,yaani unanawa uso unaenda kwenye foleni ya mihogo mpaka foleni yako ikifika saa 6 hapo unakuwa ume double impact milo miwili mchana unapita tu.😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom