Je, kwa mshahara wa Shilingi 310,000 unaweza kuishi Dar es Salaam?

Je, kwa mshahara wa Shilingi 310,000 unaweza kuishi Dar es Salaam?

Ishu kubwa hapo ni matumizi, inaweza ikawa inatosha au isitoshe kulingana na matumizi and lifestyle
Mzee kwa town chakula cha chini lunch ni 3500 times 21 working days = 73,500
Nauli kwenda na kurudi job ni 800 times 21 = 16,800

Kwa hiyo tumefuta hivi viwili kumfanya aweze kuishi town kwa mshahara huo - wewe umeviita lifestyle.
 
kwa taarifa yako bodaboda wanakipato kikubwa kupita watu wengi na ili waweze kupata kipato kikubwa wanatakiwa wafanye wafuatayo:-
  1. uaminifu kwa wateja
  2. usafi wao binafsi
  3. usafi wa bodaboda
  4. wajue uhitaji wa mteja.
hawa tunaweza kuwatumia kwa mikopo ya dharura kama gas imeisha au unahitaji mboga natoka asubuhi uliondoka mnara hausomi ikifika saa nne unampigia unamwambia samahani mdogo wangu naomba ninunulie nyama kilo moja na nyanya tutaonana jioni wapelekee nyumbani.
au gas ikiisha unamwagiza na yeye anatoa hela yake wakati wewe unachakarika au chakula chakuku kikiisha unaweza kumkopa achilia mbali kumwambia sementi imeisha site mafundi wamesimama naomba ninunulie mifuko miwili tutaonana! acha kabisa boda boda kwa kweli Mungu awalinde!
Boda boda sio poa anaweza kumzima boss hesabu ya wiki nzima akamdanganya pikipiki ilikuwa gereji hapo ana bei gani.
 
Mzee kwa town chakula cha chini lunch ni 3500 times 21 working days = 73,500
Nauli kwenda na kurudi job ni 800 times 21 = 16,800

Kwa hiyo tumefuta hivi viwili kumfanya aweze kuishi town kwa mshahara huo - wewe umeviita lifestyle.
Kama unaishi gogo la mboto au mbagala jioni nauli 1000/= tambua hilo.
 
usiwaambie kama umepata kazi
wakikuuliza vipi unawatangazia njaa
ikiwezekana piga simu kwa ndugu ukope 10,000 wataacha kukusumbua
Hizo ni "MBWINU" za kijasusi marufuku kuweka hadharani.
 
Hujasema kama una familia? ukiishi maisha ya kawaida inatosha kabisa 2007 nilikuwa nafanya kazi maeneo ya Quality plazer halafu naishi kijiwe samli uswahilini, jioni natembea mdogo mdogo mpaka tazara napanda daladala. Mshahara ulikuwa 100K kwa mwezi. Uzuri wa Dar kuna michongo kibao ya hela ukipambana.
 
Ishu kubwa hapo ni matumizi, inaweza ikawa inatosha au isitoshe kulingana na matumizi and lifestyle
kabisa mkuu tatizo wengi wanafikiria kwa kutumia lifestyle wakati kiuhalisia kuna watu wanaishi maisha ambayo hawawezi kuishi.
Kingine kila level ya maisha ina anasa zake tofauti na watu wanavyofikiria kuwa lazma mtu aende lounge, Pub au club
 
Back
Top Bottom