Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
unajua hata bodaboda au bajaj huwa wanaingiza pesa kutokana na mahali walipo mkuu.kwa taarifa yako bodaboda wanakipato kikubwa kupita watu wengi na ili waweze kupata kipato kikubwa wanatakiwa wafanye wafuatayo:-
hawa tunaweza kuwatumia kwa mikopo ya dharura kama gas imeisha au unahitaji mboga natoka asubuhi uliondoka mnara hausomi ikifika saa nne unampigia unamwambia samahani mdogo wangu naomba ninunulie nyama kilo moja na nyanya tutaonana jioni wapelekee nyumbani.
- uaminifu kwa wateja
- usafi wao binafsi
- usafi wa bodaboda
- wajue uhitaji wa mteja.
au gas ikiisha unamwagiza na yeye anatoa hela yake wakati wewe unachakarika au chakula chakuku kikiisha unaweza kumkopa achilia mbali kumwambia sementi imeisha site mafundi wamesimama naomba ninunulie mifuko miwili tutaonana! acha kabisa boda boda kwa kweli Mungu awalinde!
Hahahah hesabu za online hizo mambo kwa ground ni mtitiKuna siku nilikua naongea na mtu haya mambo ya kipato, akawa ananipigia hesabu kiukweli ni za kufikirika, eti sukari kwa mwezi kilo 1 hivi kilo moja ya sukari inakataje mwezi jamani kwenye familia?
Ndio zile hesabu za shamba unaweka milioni moja unalima unapanda unavuna faida unapata mil 13 ukitoa garama nyingine inabaki mkononi na m12
Ni kweli japo kwangu mimi watu wenye kipato cha chini ni biashara yangu na boda boda ndio watu wanaojibu maswali mengi ya kwangu kuhusu kipato kwa kuwa natumia usafiri wao kila siku. hivyo ninachokueleza kwa wao kupata hizo fedha inawezekana haijalishi yuko wapi ili mradi azingatie masharti na hasa wenye umri kati ya miaka 20-35unajua hata bodaboda au bajaj huwa wanaingiza pesa kutokana na mahali walipo mkuu.
Bodaboda anaeingia hadi town na anafanya kazi sehemu ambapo watu ni middle income anaingiza pesa nzuri kuliko hawa wanaofanyia kazi sehemu ambazo watu wengi ni kipato cha chini maana kupata route za 5000 - 10000 ni ngumu
kingine mtu mwenye bodaboda yake anaweza akaingiza pesa nzuri tofauti na anaetakiwa kupeleka hesabu kwa boss.. Ndo maana nilisisitiza hapo mkuu
Hahah itakuwa anapikia mitungi ya hospitali ileMmh Hornet feb to june....au unapikia ile mitungi XXXL😁
Mi kila mwezi nanunua gas hiyo ni lazima,
Kila kitu kinategemea location mkuuTatizo msharaha ni fixed ,ukitilea mfano bodaboda ,muuza kandoro unakosea sana.Kuna bodaboda anaishi nyumba ya 150k muuza kandoro anakwambia kwa siku anaondoka na mpk 30k faida sometime inategemea na hali ya hewa (jua).
sawa mkuu naheshimu mawazo yakoNi kweli japo kwangu mimi watu wenye kipato cha chini ni biashara yangu na boda boda ndio watu wanaojibu maswali mengi ya kwangu kuhusu kipato kwa kuwa natumia usafiri wao kila siku. hivyo ninachokueleza kwa wao kupata hizo fedha inawezekana haijalishi yuko wapi ili mradi azingatie masharti na hasa wenye umri kati ya miaka 20-35
Multicooker nyingi ni watts 600-800Labda nami nijaribu kuswitch kwenye multcooker nimejaribu kupikia maharage dk 45 umeme hata unit 1 haikuisha
310,000 mbona inatosha japo ni ngumu kufanya saving,kodi ya chumba na sebule medium quality 60000,umeme na maji 10000,chakula unasaga debe 2 za unga kila debe maximum 15000x2 ni 30000,maharage kilo 5x2000 ni 10000,mchele kilo 20x1200 ni 24000,mafuta Lita 5 ni 25000,mkaa nunua gunia moja 50000,gesi 25000 JUMLA NI 234000 hivyo ukiitoa kwenye 310000 itabaki 76000,suala la afya kata bima ya familia 54000 kwa mwaka,itabaki 22000 hii ya kubadilishia mboga kwa mwezi.Nauli kazini itabidi uwe mdau wa tz 11,suala la mavazi ni anasa,chai asubuhi ni anasa,king'amuzi ni anasa,bia ni anasa,kuhonga ni anasa, kutoa sadaka Mungu ndio anajua hali yako atakusamehe,YAANI KIFUPI UTAISHI KAMA SHETANI au nasema uongo ndugu zangu
hahaaaa hapo hujapita ukasikia harufu ya nyama chomautakuwa msabato wewe hata soda hunywi
mjinga unapenda sana wali maharage weee,mbona haujaandika dagaa au vichwa vya kuku na utumbo wa mama kibona au mayai zege la nyanya😂😂😂😂Imebidi nicheke tu
Weekend kitimoto rosti na ka bia kamoja 😂😂😂hahaaaa hapo hujapita ukasikia harufu ya nyama choma
Kila mwezi utakuwa unatumia kale kamtungi kamasela 6Kg gas😂😂😂😂😂Hahah itakuwa anapikia mitungi ya hospitali ile
Unaishije???Mimi kwa 310K naishi Dar bila zengwe.
70K Chakula Cha Mwezi Mzima.Unaishije???
Kuonga unaonga kiasi gani kwa mwezi?70K Chakula Cha Mwezi Mzima.
20K Vocha.
40K kwa wazee.
50K nauli ya mizunguko ya mwezi.
Inayobaki ni ya kusave na pocket money.
Ooh hapo kweli.Kuonga unaonga kiasi gani?
Bia ngapi kwa wiki unakunywa au wewe msabato??
Mbona umesahau kuweka kwenye bajeti hayo
Huwa najiuliza wale mama lishe huwa wanapata Tsh ngapi kwa mwezi.Habari wadau!
Ebu nisaidieni hivi kweli 310,000/= inatosha mtu kufanya kazi na kuishi DAR au unatakiwa kuwa na miundombinu mingine?