Pesa inahitaji discipline tu,ukishafanikiwa ktk hili pesa lazima ikutoshe . Wengi tunapenda kuishi maisha ambayo yasiyoendana na vipato vyetu.Tunaiga iga tu,unakuta jirani ana kipato cha milion moja na kila siku anabadil mboga bas na wewe mwenye laki tatu unataka ushindane nae , hapa lazma maisha yakushinde tu,laiti tungekua tunajikubali kuishi na kuandaa budget zetu kulingana na kipato tulicho nacho basi wengi tungefika mbali.Unakuta mtoto wa jirani anafanyiwa birthday kila mwaka na wewe unataka uige ili tu usipitwe,lakin wakat huo huo tunasahau kua binadam tunatofautiana vipato.
Kingine ni vipaumbele,yupo mmoja namfaham ye na mkewe kwa mwez wana 2m lakin pia hawalipi kodi wanaisha kwenye nyumba ya kampuni.Hawa vipaumbele vyao ni kula vizuri kuvaa vizuri na gari mda wote iwe full tank,na kuna wakati wanaishiwa ad ada za watoto na wanaishia kwenda kukopa.Wana watoto watatu.Nikisema kula vzr yan mboga zao kwa siku ni lazima nyama samaki maharage na mboga za majan ziwepo.bila kusahau matunda.HIVYO BASI KIPATO CHOCHOTE KIKITUMIKA KWA NIDHAMU MTU UNAPIGA HATUA.KIKUBWA NI KUJIKUBALI NA HALI ULIYO NAYO HUKU UKIMWOMBA MUNGU AZIDI KUKUPA UFAHAMU WA NJIA ZINGINE ZA KUJIONGEZEA KIPATO