Vipi kama hata haya madai yako pia ni potofu kwa waisilamu wengine na sipaswi kuyachukua chukua as reliable kisa tu wewe umesema?
Swali zuri, sisi Waislamu tuna marejeo yetu na misingi yetu kwayo hurejea kujua lipi sahihi na lipi si sahihi. Kwahiyo najua ninacho kiandika.
Halafu kingine hilo mimi sio jukumu langu ni jukumu lako wewe kufuatilia mienendo ya dini yako kuhakikisha unakemea upotoshaji unaosambazwa na waongo.
Hili tatizo na unapoteza maana ya kuwa na akili na umakini. Unaposikia habari lazima uihakiki kisha uitawanye na kama huna hakika juu ya jambo fulani ni bora kuuliza au kuachana nalo.
Kwahiyo hili ni la lazima endapo ukiamua kuzungumzia habari za watu na si lazima endapo ukikaa kimya ukaachana na yasiyo kuhusu.
Kama hizi stori kuhusu ahadi ya bikra 72 peponi ni stori ambayo hujawahi kuisikia kwenye mafundisho ya uislamu basi ni wazi pengine wewe sio muumini mbobevu.
Kusikia ni jambo moja na kuhakiki habari ni jambo lingine. Kwa upande wangu ninajua hakika ya hizo habari. Swali bado lipo pale pale kwa upande wako mwenye kuchukua kila unachosikia na kukitawanya, hii siyo sifa ya watu wenye akili na watu wa elimu.
Kama Masheikh wenye big title mliowapa dhamana ya kuhubiri dini wameweza kupotosha stori kuhusu dini yenu basi hamna watu sahihi wa kuihubiri dini yenu.
Huu ujinga mwingine, kwa akili hizi ndio maana ni wepesi sana kudai Mungu hayupo, sababu hamna misingi ya elimu na adabu zake. Umashuhuri sio kwamba ndio mtu kuwa na elimu, na kina nani wamewapa dhamana ?
Jitahidi uwe unaandika vitu vya maana vilivyo jengeka katika misingi ya kielimu, walau uwe na tabia kuuliza na kujua ya kuwa wewe hujui.
Hao ambao wewe unawasikia na ni maarufu tukiwapima kwenye mizani hawana sifs hizo bali Uislamu hawajui, shida wanasikilizwa na waislamu ambao hawajishughulishi na kuisoma dini yao.
Labda unitaie hao masheikh Maarufu walau wawili tu. Nijue kwamba je unajua unachokiandika ? Au ni muendelezo wako wa kusikia na kutawanya tu.