Je, kweli ni bora kuamini Mungu yupo halafu siku ya mwisho usimkute, kuliko kutoamini halafu ukamkuta?

Je, kweli ni bora kuamini Mungu yupo halafu siku ya mwisho usimkute, kuliko kutoamini halafu ukamkuta?

Duh! We jamaa naona hatuelewani kabisa una tatizo la kushindwa kuelewa unachosoma.

Nachokupinga ni hizo kauliza za kusema sayansi inakubali kukosolewa mara sayansi inasema, unafanya sayansi ni kama mtu hivi kitu ambacho naona unakosea kuelezea hivyo. Mimi sipingi sayansi wala kuidharau sayansi.
Sasa unasema huipingi sayansi, ila at the same time mimi napo nukuu policy za Sayansi kuhusu kukosolewa unazipinga kwa madai ya kuwa naifanya Sayansi kama mtu.

Hivi huoni kama wewe ndio unajichanganya?
 
Kitu ambacho hamkijui ni kuwa, Imani nayo uhakikiwa.

Kwanza lazima tuzohakiki habari hizi zinazowa husu Wamisri na Imani yao hii. Wapi chimbuko la Imani hii ?
Nipe procedures za kuhakiki imani

Halafu niambie final results zinazopatikana baada ya kuhakikiwa zinakuwa katika state gani
 
Tunasema kuhakiki hiki unachokiandika, hizi habari za kuwa Kuna kuzawadiwa mabikra 72, umezipata wapi ? Umezisikia tu pasi na kulifanyia uchunguzi au unazijua kwa kulifatilia na kuzihakiki ?
Zinasimuliwa na waumini wa Kiislamu ikiwemo Masheikh wenye majina makubwa wanao heshimika.

Sasa sijajua pengine ni maswala ya kidhehebu miongoni mwenu hizo stori hamziamini and I don't want to dwell into that kwasababu mimi sio muumini mwenzako.

Lakini kivyovyote vile itavyokuwa haijalishi jinsi gani hizo stori zitavyosimuliwa ila haitabadilisha ukweli kufanya uongo uwe kweli ili ziwe ni stori za uhalisia.
 
Mungu hayupo kila mahali, hii ni Imani potofu.

Mungu ana umbile na Wala Mungu sio Roho, yeye ndio ameumbwa hizi roho.
Twende hatua ya pili

Thibitisha huyo Mungu wa description hiyo yupo.
 
Zinasimuliwa na waumini wa Kiislamu ikiwemo Masheikh wenye majina makubwa wanao heshimika.

Sasa sijajua pengine ni maswala ya kidhehebu miongoni mwenu hizo stori hamziamini and I don't want to dwell into that kwasababu mimi sio muumini mwenzako.

Lakini kivyovyote vile itavyokuwa haijalishi jinsi gani hizo stori zitavyosimuliwa ila haitabadilisha ukweli kufanya uongo uwe kweli ili ziwe ni stori za uhalisia.

Sasa mambo ya kielimu hutakiwi kuchukua chukua tu kisa wamesema masheikh maarufu. Elimu haiko hivyo.

Fatilia hilo kisha ujue unachokiandika.

Sasa ndio maana nikasema fatilia hilo, hitimisho lako linakuwa halina maana kama hujui hakika ya jambo fulani.

Kingine kama unasema kivyovyote vile maana yake unajua unachokijadili. Nakupa kazi chukua unayo ona ni stori uje ukosoe kielimu na kuonyesha uongo wa hizo habari.

Mfano mwepesi ni huu, leta habari yoyote inayosimuliwa kutoka kwenye Qur'an kisha uonyeshe uongo wake uko wapi. Ukiweza kufanya hivyo mimi naacha kuitumia hii ID.
 
Twende hatua ya pili

Thibitisha huyo Mungu wa description hiyo yupo.

Hatua ya pili itafata baada ya wewe kujibu swali hili. Je habari ulizo ziandika hapa uliwahi kuzihakiki ? Kama hujawahi kuzihakiki kwanini unaadika mambo ambayo huna elimu nayo ?

Kisha nitarudi kwenye hatua pili sasa.
 
Kwani tafsiri ya imani ni nini?

Na uweke chanzo ulipoitoa hiyo tafsiri ili tupate rejea.

Tamko Imani linafasiliwa kwa njia mbili, njia ya Kilugha na njia ya Kiistilahi.

Imani kilugha ni KUSADIKI.

Imani Kiistilahi ni kauli kwa ulimi, kusadiki kwa moyo na kutenda juu ya imani hiyo.

Anasema Imam Ahmad (Allah amrehemu), Imani ni kauli na vitendo, inazidi na inapungua.

Na wamewafikiana waja wema ya kuwa Matendo ni katika Imani, kama alivyo nukuliwa Imam Al-Baghawi (Allah amrehemu).
 
Sasa mambo ya kielimu hutakiwi kuchukua chukua tu kisa wamesema masheikh maarufu. Elimu haiko hivyo.

Fatilia hilo kisha ujue unachokiandika.

Sasa ndio maana nikasema fatilia hilo, hitimisho lako linakuwa halina maana kama hujui hakika ya jambo fulani.

Kingine kama unasema kivyovyote vile maana yake unajua unachokijadili. Nakupa kazi chukua unayo ona ni stori uje ukosoe kielimu na kuonyesha uongo wa hizo habari.

Mfano mwepesi ni huu, leta habari yoyote inayosimuliwa kutoka kwenye Qur'an kisha uonyeshe uongo wake uko wapi. Ukiweza kufanya hivyo mimi naacha kuitumia hii ID.
Vipi kama hata haya madai yako pia ni potofu kwa waisilamu wengine na sipaswi kuyachukua chukua as reliable kisa tu wewe umesema?

Halafu kingine hilo mimi sio jukumu langu ni jukumu lako wewe kufuatilia mienendo ya dini yako kuhakikisha unakemea upotoshaji unaosambazwa na waongo.

Kama hizi stori kuhusu ahadi ya bikra 72 peponi ni stori ambayo hujawahi kuisikia kwenye mafundisho ya uislamu basi ni wazi pengine wewe sio muumini mbobevu.

Kama Masheikh wenye big title mliowapa dhamana ya kuhubiri dini wameweza kupotosha stori kuhusu dini yenu basi hamna watu sahihi wa kuihubiri dini yenu.
 
Hatua ya pili itafata baada ya wewe kujibu swali hili. Je habari ulizo ziandika hapa uliwahi kuzihakiki ? Kama hujawahi kuzihakiki kwanini unaadika mambo ambayo huna elimu nayo ?

Kisha nitarudi kwenye hatua pili sasa.
Mungu ni jina moja linalotumika kuwakilisha Miungu yote.

Kila dini ina Mungu wake na namna ambayo imempa sifa za kumuelezea zinazoweza kutofautiana na dini nyingine.

Kwa hiyo wewe kusema Mungu hayupo kila mahali inawezekana upo sahihi kwa muktadha wa dini yako ila usiwe sahihi kwa muktadha wa dini nyingine.

Hivyo basi, kwa maelezo yangu ya kudai kuwa Mungu yupo kila mahali yanaweza yasi match na sifa za Mungu wako lakini haimaanishi kuwa hakuna dini inayoamini Mungu wa sifa hizo.
 
Kwa mujibu wa Kamusi za Kiarabu na Wanazuoni wa Kiislamu.
Kumbe ni tafsiri iliyo base kwenye dini.

Nilitaka utoe tafsiri ambayo ni universal sio religion perception.
 
Tamko Imani linafasiliwa kwa njia mbili, njia ya Kilugha na njia ya Kiistilahi.

Imani kilugha ni KUSADIKI.

Imani Kiistilahi ni kauli kwa ulimi, kusadiki kwa moyo na kutenda juu ya imani hiyo.

Anasema Imam Ahmad (Allah amrehemu), Imani ni kauli na vitendo, inazidi na inapungua.

Na wamewafikiana waja wema ya kuwa Matendo ni katika Imani, kama alivyo nukuliwa Imam Al-Baghawi (Allah amrehemu).
Hii ndio umeitoa kule kwenye kiarabu na wale wanazuoni wako??
 
Hata huko zamani mtu akinywa muarobaini au quinine uthibitisho ulikuwepo na maelezo rudimentary yalikuwepo. dawa za kisasa zilizopo leo zimetokana wanasayansi kujifunza kwa muda mrefu tabia za vidudu na dawa za asili, sio kwamba walilala wakaja tu na dawa mpya. Mti wa muarobaini na quinine upo na unaonekana, hata kama hakukuwa na maelezo ya kutosha ya sayansi kuhusu muarobaini, quinine au majani ya kufukuza mbu(repellants) hao waliokuwa wanatumia walikuwa wanajua content iliyo katika hivyo vitu ndio ilikuwa inafanya kazi, waliendelea mbele zaidi wakawa wanajua watumie vikombe vingapi kwa ukubwa gani wa tatizo. Tatizo litaanza utakopesema mtoto anaumwa tumbo kwa sababu aliangaliwa kwa jicho baya na jirani lakini hata kulielezea hilo jicho baya huwezi. Mtu atakopesema amepewa utajiri na mungu lakini hawezi kusema kwa nini amepewa yeye na sio mwingine n.k
"...hata kama hakukuwa na maelezo ya kutosha ya sayansi kuhusu muarobaini, quinine au majani ya kufukuza mbu" point yangu ipo hapo kwamba hakukuwa na maelezo ya kisayansi, na sio huko zamani tu hata sasa kuna baadhi ya vyakula au mimea ambayo hudaiwa kuwa na faida fulani kiafya ila hakuna maelezo ya kisayansi kusapoti hayo madai.

"walikuwa wanajua content iliyo katika hivyo vitu ndio ilikuwa inafanya kazi" Kwa faida unaweza kuelezea waliweza kujua kwa njia gani kuhusu hizo contents kipindi hicho?
 
Kujua ni bora zaidi kuliko kuamini.

Kwa nini huyo Mungu ajifiche na aachie watu wakisie uwepo wake ilhali angeweza tu kujitokeza na wote tukamjua?
Umewahi kupewa mtihani na majibu yake? Majibu lazima yafichwe ili mwalimu apate kusahihisha mtihani Kuna alie faulu na aliefeli
 
Kwa nini uhitaji kuamini Mungu yupo, Badala ya kujua Mungu yupo kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho?

Huyo Mungu akijulikana yupo kwa uhakika na uthibitisho itampunguzia nini kuwa Mungu?

Huyo Mungu kama yupo kwa nini ajifiche huko alipo, Halafu atake aaminiwe na watu akiwa mafichoni?

Huyo Mungu kama yupo, Anacho ogopa kujulikana hadharani ni nini?
Haya maneno ya kujua na kuamini yanawachanganya sana, kujua hakutenganishi ukweli na uongo.
 
Vipi kama hata haya madai yako pia ni potofu kwa waisilamu wengine na sipaswi kuyachukua chukua as reliable kisa tu wewe umesema?

Swali zuri, sisi Waislamu tuna marejeo yetu na misingi yetu kwayo hurejea kujua lipi sahihi na lipi si sahihi. Kwahiyo najua ninacho kiandika.
Halafu kingine hilo mimi sio jukumu langu ni jukumu lako wewe kufuatilia mienendo ya dini yako kuhakikisha unakemea upotoshaji unaosambazwa na waongo.

Hili tatizo na unapoteza maana ya kuwa na akili na umakini. Unaposikia habari lazima uihakiki kisha uitawanye na kama huna hakika juu ya jambo fulani ni bora kuuliza au kuachana nalo.

Kwahiyo hili ni la lazima endapo ukiamua kuzungumzia habari za watu na si lazima endapo ukikaa kimya ukaachana na yasiyo kuhusu.
Kama hizi stori kuhusu ahadi ya bikra 72 peponi ni stori ambayo hujawahi kuisikia kwenye mafundisho ya uislamu basi ni wazi pengine wewe sio muumini mbobevu.

Kusikia ni jambo moja na kuhakiki habari ni jambo lingine. Kwa upande wangu ninajua hakika ya hizo habari. Swali bado lipo pale pale kwa upande wako mwenye kuchukua kila unachosikia na kukitawanya, hii siyo sifa ya watu wenye akili na watu wa elimu.
Kama Masheikh wenye big title mliowapa dhamana ya kuhubiri dini wameweza kupotosha stori kuhusu dini yenu basi hamna watu sahihi wa kuihubiri dini yenu.

Huu ujinga mwingine, kwa akili hizi ndio maana ni wepesi sana kudai Mungu hayupo, sababu hamna misingi ya elimu na adabu zake. Umashuhuri sio kwamba ndio mtu kuwa na elimu, na kina nani wamewapa dhamana ?

Jitahidi uwe unaandika vitu vya maana vilivyo jengeka katika misingi ya kielimu, walau uwe na tabia kuuliza na kujua ya kuwa wewe hujui.

Hao ambao wewe unawasikia na ni maarufu tukiwapima kwenye mizani hawana sifs hizo bali Uislamu hawajui, shida wanasikilizwa na waislamu ambao hawajishughulishi na kuisoma dini yao.

Labda unitaie hao masheikh Maarufu walau wawili tu. Nijue kwamba je unajua unachokiandika ? Au ni muendelezo wako wa kusikia na kutawanya tu.
 
Kwa nini uishi kwa imani?

Kwa nini usiishi kwa kujua?

Hivi wavumbuzi na wanasayansi wangeishigi kwa imani tu. Bila kudadisi, Bila kutaka kujua, Bila kufanya tafiti za kina.

Je Tungefikia maendeleo tuliyonayo leo hii kwenye nyanja mbalimbali za maisha kwa hiyo imani tu?
Unaelewa kwamba unaweza ukajua hata vitu ambavyo si vya kweli?
 
Hakuna ajuwaye kama Mungu yupo au hayupo. Ila tunachqkataa ni kuaminishwa uongo kuwa Mungu kaandika vitabu vya kutumia kumuabudu. Wakati vitabu hivyo vimeandikwa na watu kama mimi na wewe. Tunakataa kuamini Mungu kama yupo kwa sababu hatujaona kitu chakutuaminisha uwepo wake. Hata kama yupo basi sisi sio viumbe mhim kwake kama vitabu vya dini vinavyo tuaminisha. Au kama yupo basi hana nguvu au uwezo unao elezewa kwenye vitabu vya dini. Kuamini kitu usicho kijuwa ni ujinga. Ukisema unaamini Mungu maana yake huna haja ya kuishi tena, inabidi usibili tu maagiza ya Mungu.
Wewe unasema akuna ajuaye kama Mungu hayupo wakati atheists humu wanasema wazi kuwa hakuna Mungu? Waulize Atheists wamejuaje?
 
Mungu ni jina moja linalotumika kuwakilisha Miungu yote.

Kila dini ina Mungu wake na namna ambayo imempa sifa za kumuelezea zinazoweza kutofautiana na dini nyingine.

Kwa hiyo wewe kusema Mungu hayupo kila mahali inawezekana upo sahihi kwa muktadha wa dini yako ila usiwe sahihi kwa muktadha wa dini nyingine.

Hivyo basi, kwa maelezo yangu ya kudai kuwa Mungu yupo kila mahali yanaweza yasi match na sifa za Mungu wako lakini haimaanishi kuwa hakuna dini inayoamini Mungu wa sifa hizo.

Safi kabisa, ukisoma historia ya Wanafalsafa wakale wa magharibi walau kidogo walikuwa wana maswali sahihi ila walikosa ala za kuwafikisha katika majibu sahihi. Kutofautiana juu ya kitu kimoja kwa majibu mengi na wewe ukaifanya kuwa ni hoja, kunadhihirisha wewe ni mchachefu sana wa elimu juu ya dini hizo, huenda hujazisoma ukajua machimbo yake na kwanini imekuwa hivi.

Ni kweli kuna miungu wengi, ila hata hao wenye kuabudu miungu yao wanajua ya kuwa kuna Mungu Mkuu aliyeumba, rejea historia ya Makafiri wa Makka na wasio kuwa hao.

Jaribuni kusoma vitu ili kidogo muwe mnajenga hoja zenhye maana na zenye nguvu.

Unapo ongelea tamko Mungu. katika Kamusi zote za lugha zinamtambua ya kuwa ni yule Mungu mkuu, muumba wa mbingu na ardhi na apasae kuabudiwa peke yake. Sasa unaposikia kuna dini wanamuabudu Ng'ombe na kumfanya Mungu, kwa akili makini tu inaonyesha wazi Ng'ombe hawzi kuwa mungu zaidi ya ujinga wa watu.

Ndio maana nikasema imani hiyo siyo sahihi, sababu ina chimbuko lake. Kijana kwa kukusaidia tu, unapotaka ujue uhakika wa jambo fulani hasa dini, kwanza tunaangalia historia husika za dini hiyo, kwako wewe na kwa jinsi ulivyo nina uhakika hujawahi kusoma historia za hizo dini na ukajua machimbuko na huu ni udhaifu mkubwa sana katika utafiti.
 
Back
Top Bottom