Sasa unasema huipingi sayansi, ila at the same time mimi napo nukuu policy za Sayansi kuhusu kukosolewa unazipinga kwa madai ya kuwa naifanya Sayansi kama mtu.Duh! We jamaa naona hatuelewani kabisa una tatizo la kushindwa kuelewa unachosoma.
Nachokupinga ni hizo kauliza za kusema sayansi inakubali kukosolewa mara sayansi inasema, unafanya sayansi ni kama mtu hivi kitu ambacho naona unakosea kuelezea hivyo. Mimi sipingi sayansi wala kuidharau sayansi.
Nipe procedures za kuhakiki imaniKitu ambacho hamkijui ni kuwa, Imani nayo uhakikiwa.
Kwanza lazima tuzohakiki habari hizi zinazowa husu Wamisri na Imani yao hii. Wapi chimbuko la Imani hii ?
Zinasimuliwa na waumini wa Kiislamu ikiwemo Masheikh wenye majina makubwa wanao heshimika.Tunasema kuhakiki hiki unachokiandika, hizi habari za kuwa Kuna kuzawadiwa mabikra 72, umezipata wapi ? Umezisikia tu pasi na kulifanyia uchunguzi au unazijua kwa kulifatilia na kuzihakiki ?
Zinasimuliwa na waumini wa Kiislamu ikiwemo Masheikh wenye majina makubwa wanao heshimika.
Sasa sijajua pengine ni maswala ya kidhehebu miongoni mwenu hizo stori hamziamini and I don't want to dwell into that kwasababu mimi sio muumini mwenzako.
Lakini kivyovyote vile itavyokuwa haijalishi jinsi gani hizo stori zitavyosimuliwa ila haitabadilisha ukweli kufanya uongo uwe kweli ili ziwe ni stori za uhalisia.
Twende hatua ya pili
Thibitisha huyo Mungu wa description hiyo yupo.
Hii ni kwa mujibu wa kamusi gani? Au ni perspective yako?
Kwani tafsiri ya imani ni nini?
Na uweke chanzo ulipoitoa hiyo tafsiri ili tupate rejea.
Vipi kama hata haya madai yako pia ni potofu kwa waisilamu wengine na sipaswi kuyachukua chukua as reliable kisa tu wewe umesema?Sasa mambo ya kielimu hutakiwi kuchukua chukua tu kisa wamesema masheikh maarufu. Elimu haiko hivyo.
Fatilia hilo kisha ujue unachokiandika.
Sasa ndio maana nikasema fatilia hilo, hitimisho lako linakuwa halina maana kama hujui hakika ya jambo fulani.
Kingine kama unasema kivyovyote vile maana yake unajua unachokijadili. Nakupa kazi chukua unayo ona ni stori uje ukosoe kielimu na kuonyesha uongo wa hizo habari.
Mfano mwepesi ni huu, leta habari yoyote inayosimuliwa kutoka kwenye Qur'an kisha uonyeshe uongo wake uko wapi. Ukiweza kufanya hivyo mimi naacha kuitumia hii ID.
Mungu ni jina moja linalotumika kuwakilisha Miungu yote.Hatua ya pili itafata baada ya wewe kujibu swali hili. Je habari ulizo ziandika hapa uliwahi kuzihakiki ? Kama hujawahi kuzihakiki kwanini unaadika mambo ambayo huna elimu nayo ?
Kisha nitarudi kwenye hatua pili sasa.
Hii ndio umeitoa kule kwenye kiarabu na wale wanazuoni wako??Tamko Imani linafasiliwa kwa njia mbili, njia ya Kilugha na njia ya Kiistilahi.
Imani kilugha ni KUSADIKI.
Imani Kiistilahi ni kauli kwa ulimi, kusadiki kwa moyo na kutenda juu ya imani hiyo.
Anasema Imam Ahmad (Allah amrehemu), Imani ni kauli na vitendo, inazidi na inapungua.
Na wamewafikiana waja wema ya kuwa Matendo ni katika Imani, kama alivyo nukuliwa Imam Al-Baghawi (Allah amrehemu).
"...hata kama hakukuwa na maelezo ya kutosha ya sayansi kuhusu muarobaini, quinine au majani ya kufukuza mbu" point yangu ipo hapo kwamba hakukuwa na maelezo ya kisayansi, na sio huko zamani tu hata sasa kuna baadhi ya vyakula au mimea ambayo hudaiwa kuwa na faida fulani kiafya ila hakuna maelezo ya kisayansi kusapoti hayo madai.Hata huko zamani mtu akinywa muarobaini au quinine uthibitisho ulikuwepo na maelezo rudimentary yalikuwepo. dawa za kisasa zilizopo leo zimetokana wanasayansi kujifunza kwa muda mrefu tabia za vidudu na dawa za asili, sio kwamba walilala wakaja tu na dawa mpya. Mti wa muarobaini na quinine upo na unaonekana, hata kama hakukuwa na maelezo ya kutosha ya sayansi kuhusu muarobaini, quinine au majani ya kufukuza mbu(repellants) hao waliokuwa wanatumia walikuwa wanajua content iliyo katika hivyo vitu ndio ilikuwa inafanya kazi, waliendelea mbele zaidi wakawa wanajua watumie vikombe vingapi kwa ukubwa gani wa tatizo. Tatizo litaanza utakopesema mtoto anaumwa tumbo kwa sababu aliangaliwa kwa jicho baya na jirani lakini hata kulielezea hilo jicho baya huwezi. Mtu atakopesema amepewa utajiri na mungu lakini hawezi kusema kwa nini amepewa yeye na sio mwingine n.k
Umewahi kupewa mtihani na majibu yake? Majibu lazima yafichwe ili mwalimu apate kusahihisha mtihani Kuna alie faulu na aliefeliKujua ni bora zaidi kuliko kuamini.
Kwa nini huyo Mungu ajifiche na aachie watu wakisie uwepo wake ilhali angeweza tu kujitokeza na wote tukamjua?
Haya maneno ya kujua na kuamini yanawachanganya sana, kujua hakutenganishi ukweli na uongo.Kwa nini uhitaji kuamini Mungu yupo, Badala ya kujua Mungu yupo kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho?
Huyo Mungu akijulikana yupo kwa uhakika na uthibitisho itampunguzia nini kuwa Mungu?
Huyo Mungu kama yupo kwa nini ajifiche huko alipo, Halafu atake aaminiwe na watu akiwa mafichoni?
Huyo Mungu kama yupo, Anacho ogopa kujulikana hadharani ni nini?
Vipi kama hata haya madai yako pia ni potofu kwa waisilamu wengine na sipaswi kuyachukua chukua as reliable kisa tu wewe umesema?
Halafu kingine hilo mimi sio jukumu langu ni jukumu lako wewe kufuatilia mienendo ya dini yako kuhakikisha unakemea upotoshaji unaosambazwa na waongo.
Kama hizi stori kuhusu ahadi ya bikra 72 peponi ni stori ambayo hujawahi kuisikia kwenye mafundisho ya uislamu basi ni wazi pengine wewe sio muumini mbobevu.
Kama Masheikh wenye big title mliowapa dhamana ya kuhubiri dini wameweza kupotosha stori kuhusu dini yenu basi hamna watu sahihi wa kuihubiri dini yenu.
Unaelewa kwamba unaweza ukajua hata vitu ambavyo si vya kweli?Kwa nini uishi kwa imani?
Kwa nini usiishi kwa kujua?
Hivi wavumbuzi na wanasayansi wangeishigi kwa imani tu. Bila kudadisi, Bila kutaka kujua, Bila kufanya tafiti za kina.
Je Tungefikia maendeleo tuliyonayo leo hii kwenye nyanja mbalimbali za maisha kwa hiyo imani tu?
Wewe unasema akuna ajuaye kama Mungu hayupo wakati atheists humu wanasema wazi kuwa hakuna Mungu? Waulize Atheists wamejuaje?Hakuna ajuwaye kama Mungu yupo au hayupo. Ila tunachqkataa ni kuaminishwa uongo kuwa Mungu kaandika vitabu vya kutumia kumuabudu. Wakati vitabu hivyo vimeandikwa na watu kama mimi na wewe. Tunakataa kuamini Mungu kama yupo kwa sababu hatujaona kitu chakutuaminisha uwepo wake. Hata kama yupo basi sisi sio viumbe mhim kwake kama vitabu vya dini vinavyo tuaminisha. Au kama yupo basi hana nguvu au uwezo unao elezewa kwenye vitabu vya dini. Kuamini kitu usicho kijuwa ni ujinga. Ukisema unaamini Mungu maana yake huna haja ya kuishi tena, inabidi usibili tu maagiza ya Mungu.
Mungu ni jina moja linalotumika kuwakilisha Miungu yote.
Kila dini ina Mungu wake na namna ambayo imempa sifa za kumuelezea zinazoweza kutofautiana na dini nyingine.
Kwa hiyo wewe kusema Mungu hayupo kila mahali inawezekana upo sahihi kwa muktadha wa dini yako ila usiwe sahihi kwa muktadha wa dini nyingine.
Hivyo basi, kwa maelezo yangu ya kudai kuwa Mungu yupo kila mahali yanaweza yasi match na sifa za Mungu wako lakini haimaanishi kuwa hakuna dini inayoamini Mungu wa sifa hizo.