Je, kweli ni bora kuamini Mungu yupo halafu siku ya mwisho usimkute, kuliko kutoamini halafu ukamkuta?

Yaani kama Biblia imewapanga sana watu aiseee, kuna uzi niliuanzisha humu ngoja niutafute nikutag
 
Yani hayo maelezo yako ndio yanathibitisha nilichokisema jinsi unavyoichukulia sayansi, hebu soma hayo maelezo yako vizuri.

Unaposema sayansi inakubali haipo perfect, mara sayansi inatoa mwanya kuruhusu ukosoaji. Huoni tu unakuwa unaifanya sayansi kama dubwasha fulani hivi?

Sayansi haisemi wala kukosolewa, tafiti za kisayansi zinazofanywa na watu ndio husema hivi au vile na ndio maana unaweza kuzikosoa.
 
Labda uweke Double chance ( X1, X2 au 12)
 
Tuamini yupo Mungu,Imani ni bayana kwa mambo yasioonekana kwa macho,lakini ni dhahiri kama vile upepo uvumavyo kutoka kusini kwenda kaskazini au magharibi kwenda mashariki .Hatuuoni ila tunahisi!
 
Kujua ni bora zaidi kuliko kuamini.

Kwa nini huyo Mungu ajifiche na aachie watu wakisie uwepo wake ilhali angeweza tu kujitokeza na wote tukamjua?
Kinachotangulia ni elimu inayohusu Mungu uisikie akili ielewe, baada ya kujua imani inazaliwa moyoni,
"Chanzo cha imani ni kusikia neno la Kristo" Rum 10:17.
 
Maswali umeyacomplicate sababu unamweka Mungu kama mtu mwenye mwili.Lakini sio hivyo, Mungu ni Roho hawezi kuonekana kwa macho anaonekana kwa imani kwa wale waloamua kuongozwa na neno lake.Hivyo hakuna sababu ya kubet kama yupo au hayupo kwani imani yako itadhirisha kuwa Mungu ni Bwana,
 
Ukiamini Mungu yupo ili tu ikitokea kweli yupo u-save, hiyo si imani ya kweli, utakuwa unapoteza muda wako.

Ili kumpendeza Mungu lazima uwe na imani ya kweli kwamba yupo, siokuamini kwa namna ya kujikatia insurance ili kama yupo utoboe siku ya mwisho!
 
Yani wewe hubadilikagi ni mzito kuelewa.

Hivi wewe unaweza kufananisha ngono inayofanywa na wacheza filamu za ngono na ngono inayofanywa na watu wa kawaida katika faragha? Lengo la ngono ni kufanya kama maonesho hadharani?
Kwani ngono ya wacheza filamu huwa haihusishi penetration of sex organ?
 
Kwanza unatakiwa kujua kuwa Sayansi haisemi kuwa inajua kila kitu.

Pili Sayansi ilisha set standard zake za namna inavyo operate kwa hiyo huwezi kuona inatoka kwenye njia kwa ajili ya ku feed ego za watu. Na ndio maana utaona wapo wanasayansi wana amini Mungu yupo lakini sio Sayansi.

Kitu cha tatu ambacho naweza kukuongezea kama ziada kuhusu dawa za asili nyingi zinatoka katika mazingira ya kitamaduni sehemu ambayo Sayansi haija take over na hutumika kwa asilimia kubwa katika mazingira hayo hayo. Ulitegemea kuiona wanasayansi wanazunguka kila kona kufanya utafiti wa hizo dawa?

Kusema kwamba kuna dawa zinatibu na watu wanapona ila hakuna maelezo ya kisayansi, its like kusema mauaji ya albino kama kafara ya kujitajirisha yamekosa uthibitisho wa kisayansi ila kuna watu wanaua Allbino na wanapata hela.
 
Unaweza kuthibitisha huyo Mungu yupo?
 
Duh! Mkuu ni hoja ipi hapa ambayo unanipinga kwenye hili suala la sayansi? Labda hapo ndio nitajua nikueleweshe vp maana naona naeleza kitu ambacho umeshindwa kabisa kielewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…