Tz mbongo
JF-Expert Member
- Mar 12, 2015
- 13,332
- 7,351
Sijui kama umeelewa ulichoandika mwenyewe.Kwanza watu wa kale kutibu maradhi kwa mitishamba kulitokana na wao kuyafahamu vyema mazingira yaliyowazunguka.
Kwa hiyo watu ambao waliweza kutofautisha dawa hii ni ya kichwa na hivyo tusiitumie kutibu tumbo, sio kweli kwamba wangeshindwa kuelezea kwanini hizo dawa zinafanya kazi.
Lakini yote kwa yote kwa yote hizo dawa bado unabaki kuwa ni mjadala wa vitu ambavyo tayari vipo na vinathibitishika kuwa vipo ila wewe umehoji tu kujua maelezo yake katika ufanisi wa hizo dawa.
Ni tofauti na swala la Mungu, Mungu hathibitishiki na hakuna namna ya kuthibitisha ili kufananisha na mazingira ya zile dawa za watu wa kale.
Kwa hiyo mfano wako upo irrelevant kabisa.
Halafu kitu kingine ni kuwa fact ya kwamba sayansi imeshindwa kuthibitisha vitu fulani haitoi guarantee ya kukubali vitu vingine ambavyo havijathibitishwa kuwa ni kweli eti kwakuwa tu kuna baadhi ya vitu sayansi haijathibitisha.
Mkuu hadi leo zipo dawa za asili ambazo tunajua faida zake na watu hutumia ila hakuna uthibitisho wa kisayansi na ndio hoja yangu hapa, na ndio maana nikatoa mfano hadi wa Dowsing ambayo imekuwa ikitumika sana na ina visa vikubwa tu ila inapingwa kwa sababu bado haijathibitika kisayansi hivyo si kwamba nataka ukubali vitu tu kuwa ni kweli ila suala la kupinga kitu kisa hakijathibitika kisayansi.