Je, kweli ni bora kuamini Mungu yupo halafu siku ya mwisho usimkute, kuliko kutoamini halafu ukamkuta?

Link haifunguki
 
Nakuelewa jinsi hisia zako zinavyokutuma kuongea hivyo na hii inaweza kutokana na namna ambavyo waislamu wengi mmekuwa hamna muamko kwenye ishu nzima ya Elimu kiujumla hivyo kwenu Sayansi inaweza kuonekana ni kitu kikubwa kisichoeleweka kwa urahisi.

Sayansi ni mchakato wa kujifunza wa jinsi tunaweza kuuelewa ulimwengu unaotuzunguka kwa njia ya testable na kukosoa nadharia ili kupata uelewa ulio bora zaidi.

Sayansi kukubali kuwa haijakamilika ni jambo la busara linalotoa mwanya kwa ukosoaji kwa sababu ni sehemu ya mchakato wa kujifunza pia.

Mfano wanasayansi wanapofanya utafiti huchapisha matokeo yao ili wanasayansi wengine waweze kuyapitia na kuyakosoa. Hii inaweza kusaidia kuwa matokeo ni sahihi na yanaweza kuaminika.

Kwa hiyo, badala ya kuiona sayansi kama dubwasha, ni bora kuiona kama mchakato wa kujifunza unaoendelea ambao unalenga kuboresha uelewa wetu wa ulimwengu. Ni njia ya kutafuta ukweli kwa kutumia ushahidi na mantiki.
 
Tuamini yupo Mungu,Imani ni bayana kwa mambo yasioonekana kwa macho,lakini ni dhahiri kama vile upepo uvumavyo kutoka kusini kwenda kaskazini au magharibi kwenda mashariki .Hatuuoni ila tunahisi!
Sisi hatusemi Mungu hayupo kwasababu haonekani.

Hii ni hygrometer hutumika kupima unyevu (moisture) kwenye hewa


Hii ni thermometer hutumika kupima joto la hewa


Na hii ni Barometer hutumika kupima pressure ya hewa


Na hii ni Digital Anenometer hutumika kupima uelekeo wa upepo


Ni kifaa gani ambacho tunaweza kukitumia kupima uwepo wa Mungu?
 
Imani ya kweli ipo kwa kuamini Mungu yupi kati ya maelfu wanaoabudiwa duniani kote?
 
Elewa kuwa ni wewe ndio unaiona sayansi kama dubwasha sio mimi, maana hapo hata sijui kama unaelewa mie nachokieleza maana naona kama najadiliana na robot.
 
Sio type ya sex ambayo hutokea kufanyika sana kwa sex ya kawaida(sio ya maonyesho) ya faragha.
Kwa hiyo normal sex inayofanywa faraghani isiyo husisha double anal haiwezi kufanywa hadharani?
 
Elewa kuwa ni wewe ndio unaiona sayansi kama dubwasha sio mimi, maana hapo hata sijui kama unaelewa mie nachokieleza maana naona kama najadiliana na robot.
Ni rahisi wewe kuona mimi nai praise sana Sayansi na kuchukulia kitu hicho kama cha kijinga kutokana na msingi wako wa maisha ulilenga kujikita zaidi kwenye madrasa.

Ni kama ambavyo tumezoea kuona jamii nyingi za waislamu wamekuwa wakipuuza elimu dunia halafu ikifika siku ya Iddi wanaanza kuisumbua serikali iwanunulie binocular ya kisayansi kwa ajili ya kutazama mwezi.
 
Kama ambavyo watu wanahukumiwa mahakamani ndio hivyo watavyohukumiwa kwa matendo wanayoyatenda wakiwa hai. Kama matendo ni mazuri utapata unachostahili kutokana na kusudio la Mungu kukuumba
 
Imani ya kweli ipo kwa kuamini Mungu yupi kati ya maelfu wanaoabudiwa duniani kote?
Kuna Mungu mmoja tu wa kweli, sasa mtafute huyo ndio ujenge imani yako juu ya wengine. Ikiwa kuna dawa fake nyingi tu duniani, sio sababu ya wewe kusema hutatumia dawa tena. Utahakikisha unapata dawa isiyo feki ili kuokoa uhai wako!
 
Kuna Mungu mmoja tu wa kweli, sasa mtafute huyo ndio ujenge imani yako juu ya wengine. Ikiwa kuna dawa fake nyingi tu duniani, sio sababu ya wewe kusema hutatumia dawa tena. Utahakikisha unapata dawa isiyo feki ili kuokoa uhai wako!
Kwanini katika maelfu ya miungu kuwe na mmoja tu wa kweli tena yule ambaye wewe una muabudu?

Umejaribu kufikiria hao wanaoamini miungu wengine wao wanaichukuliaje miungu yao?

Je nao hawapati perception kama yako kudhani kwamba Mungu wao pekee ndio wa kweli huku miungu mingine iliyobaki ni ya uongo?

Sasa tunapotaka kufika hitimisho kujua yupi yupo sahihi, tutatumia kigezo gani kupata ukweli??
 
Ulionana naye wapi na una uhakika gani haikuwa hallucinations?
Nilionana nae ni kiwa kazini, sura kabisa huoni ila sauti unaisikia na vitendo vyake mpaka baadae unakuja kujikuta unacheka tuu . Kweli ni mfariji wa moyo.

Mungu yupo nakuambia kubali ukatae yupo
 
Hoja ya kusema ni bora uamini kuwa Mungu yupo kuliko kutoamini halafu ukifa ukakuta yupo. Ni hoja ya kijinga kwasababu inakufanya uendelee kuamini ujinga hata kama umeisha juwa ni ujinga. Ujinga ni kama ugojwa ukiuweka karibu yako lazima utajikuta umekuingia hadi kwenye damu.
 
Nilionana nae ni kiwa kazini, sura kabisa huoni ila sauti unaisikia na vitendo vyake mpaka baadae unakuja kujikuta unacheka tuu . Kweli ni mfariji wa moyo.

Mungu yupo nakuambia kubali ukatae yupo
Ndio nakuuliza unajuaje kama haikuwa hallucinations?

Unajua hallucinations ni nini?
 
Scars
Kiranga
min -me
Infropreneur
Nyani Ngabu

Mmekua mnapinga uwepo wa Mungu kila siku kwa kuuliza maswali yale yale bila kuja na kitu kipya
Sasa naomba niwaulize kama mmeweza kujua kuwa hakuna Mungu, pia kuna uwezekano mmeshajua Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake
Naomba mje kutueleza chanzo cha huu ulimwengu na viumbe vyake ni nini?

Nafkiri sisi wenye imani ya uwepo wa Mungu tuanze kuwa challenge hawa Atheist kwa kuwahoji maswali fikirishi sio kila siku kubishana Mungu yupo au hayupo
 
Labda Mashahidi wa Yehova(JW) walifikiria kama wewe ndio maana hawaamini wenye dhambi watabanikiwa kwenye moto wakifa bali watapotea tu.
 
Sasa kuamua kuabudu miungu feki au ya kweli unabaki uamuzi wako. Ndio maana hata wafanyabiashara wanapokuuzia kitu watakwambia ipo original au feki!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…