Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Ngoja nijaribu tenaLink haifunguki
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ngoja nijaribu tenaLink haifunguki
Link haifunguki
Neno BIBLIA lina maana ya mkusanyiko wa vitabu na ndani ya mkusanyiko huo kuna maandiko ya AGANO LA KALE na maandiko ya AGANO JIPYA.... Maandiko ya AGANO LA KALE ni mengi sana yamepangiliwa vyema na ni rahisi sana kueleweka kuliko maandiko machache ya AGANO JIPYA... Ndio maana Wasabato na Waislamu wengi wanayakubali sana maandiko ya AGANO LA KALE kuliko maandiko ya AGANO JIPYA.🙏
Ukisoma kitabu cha AGANO LA KALE kuanzia MWANZO hadi MALAKI unaweza kuwafahamu vyema wahusika wote na hata koo zao.👉 Lakini ukisoma kitabu cha AGANO JIPYA utaona waandishi wamelipua au wameunga unga vipande vya maandishi wala huwezi kukuta kurasa walau 4 zinaelezea kitu kimoja. Stori hazijitoshelezi.
Kuanzia MATHAYO mpaka UFUNUO... Utakutana na stori au hadithi zilezile chache zinazofanana harafu utakuta mwandishi ktk AGANO JiPYA, anasema eti "Kuna mambo mengi aliyofanya Yesu, ambayo yakiandikwa mojamoja nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa" YOHANA 21:25.
Je, hii ilikuwa ni kweli? Waandishi walijisahau au waandishi waliamua tu kufanya makusudi Kwa lengo Yesu asiweze kusomeka kwa mambo mengi ambayo mengineyo (huenda) yangedhoofisha 'Utakatifu' 'Unabii' 'Uana wa Mungu' au 'Uungu wake?' Maana haiwezekani waandishi kama MATHAYO, MARKO, LUKA na YOHANA... Wakajikuta wote kwa pamoja wanaandika jambo lilelile kumhusu Yesu, bila ya kusimulia story tofauti wakati kila mmoja aliandika INJILI kwa wakati wake.
Kwamfano... MATHAYO angeandika INJILI yake kwa ufasaha kabisa kuhusu uzao wote wa Yesu uzao wa wazazi wake pamoja na ndugu zake wote. Kisha MARKO naye angeandika INJILI yake historia ya maisha ya Yesu kuanzia alipofikisha umri wa miaka 12 mpaka 29 kwamba (Yesu) alikuwa anaishi wapi, alikuwa anapendelea kufanya nini na nini na alipofikisha umri wa kufanya kazi alifanya kazi gani?
LUKA na YOHANA pamoja nyaraka kadhaa za akina Mtume PAULO... Wenyewe wangeandika kama hivi walivyoandika kazi za Yesu alipoanza kuhubiri INJILI akiwa na umri wa miaka 30... Naamini vitabu vingetosha kabisa na sisi wasomaji tusingechoka kuvisoma na wala tusingefikia hatua ya kutofautiana hata kuzalisha madhehebu mbalimbali ya kidini.
Angalia jinsi waandishi wote wa AGANO JiPYA walivyoacha kuandika Siku, Tarehe, Mwezi na hata Mwaka aliozaliwa Yesu... Watu wengine baadae walipokuja kusema kuwa "Yesu amezaliwa Desemba 25" Ndipo Wasabato na Waislamu walipoamua kupingana ktk hilo... Na sio ktk hilo tu...Hata kwenye masuala ya ulaji wa nyama ya Nguruwe, siku maalum ya kuabudu Mungu, Kufunga mwezi mtukufu, Sikukuu ya Pasaka na hata kuoa, kuolewa na Talaka... AGANO JIPYA halifafanui kwa uwazi kama ilivyo AGANO LA KALE.
Mitume na Manabii wote walioandikwa ktk kitabu cha AGANO LA KALE wametajwa kwa uwazi majina ya wazazi wao wote mpaka ndugu zao... Lakini ukisoma kitabu cha AGANO JIPYA ni vigumu sana kukuta majina ya wazazi wa mama yake Yesu na vigumu sana kukuta majina halisi ya ndugu zake Yesu. Ingawa inasemekana Yesu alikuwa na mama zake wadogo, Shangazj zake, Wajomba zake, Kaka na Dada zake...
Pia alikuwa na Babu pamoja na Bibi zake ambao wanatajwa kuwa ni (Anna na Yoakimu), lakini ndani ya AGANO JiPYA hawakuwekwa wazi.
Vilevile si rahisi kukuta ktk AGANO JIPYA imeandikwa kazi alizofanya Yesu (kabla hajaanza kuhubiri), si rahisi kukuta imeandikwa kama Yesu alikuwa na mke au mpenzi au alikuwa hana kabisa AGANO JIPYA limekwepa kabisa kuandika yote hayo, ingawa inatambua wazi Yesu alikuwa ni mwanadamu mkamilifu kama walivyo wanadamu wengine... Alikuwa Analala, Anakula na Kunywa, Alikuwa anavaa Nguo. Alikuwa anajisaidia haja ndogo na kubwa... Alikuwa anachukia na kufurahi... Alikuwa anachoka, Alibatizwa, Alitahiriwa, Alikuwa anasali na kuomba Dua na pia alikuwa na matamanio kama walivyo wanadamu wengine (maana alitamani hata kula matunda ktk mti fulani) na alipokuta matunda hakuna Yesu alichukia.
Kama ukisoma kwa kuunga unga maandiko ndani ya AGANO JIPYA, utagundua kuwa akina YUDA walikuwa wawili na mmoja ni ndugu yake Yesu. Akina Mariamu walikuwa watatu ambapo mmoja ni mama yake mzazi, wa pili mama yake mdogo na wa tatu ni Mariamu Magdalena (ambaye amezua gumzo sana ulimwenguni). Pia utagundua Simeoni Petro, Andrea, Yakobo, Yohana, Yuda, Yosefu au Yusufu, Salome na Yohana walikuwa ni ndugu wa mama mmoja (Mariamu mama yake mdogo Yesu) lakini baba tofauti. Lakini Yohana Zakaria alikuwa ni kaka wa Yesu (mtoto wa mama yake mkubwa Elizabeth).
Unga unga maandiko haya ili kuwajua ndugu wa Yesu: MATAYO 13:55 👉 MARKO 6:3 👉 LUKA 6:13:16 👉 MARKO 15:40 👉 LUKA 24:10 👉 MARKO 1:29 👉 YOHANA 19:25 👉 MATENDO 12:12:17 👉 MATENDO 12:2 na YUDA 1:1. Petro na Andrea baba yao ni Yohana. Yakobo na Yohana baba yao ni Zebedayo.
Bado kuna hili la mafumbo! Katika AGANO JIPYA kuna maandiko mengi yenye muundo wa Mifano, Methali na Mafumbo... Ambayo ni vigumu kwa watu wengi kuelewa wakati kitabu chenyewe kimatafsiriwa katika llugha zote za ulimwengu... Mfano ni INJILI ya YOHANA INJILI hii ndio imehusika zaidi kumficha mwanafunzi aliyependwa na Yesu bila ya kumtaja jina mpaka mwisho. Je, lengo hapa lilikuwa nini?
AGANO JIPYA haikuandika wazi kusema kama Yusufu na Mariamu (baada ya posa) walioana? Waliendelea kuishi pamoja hadi kifo kilipowatengenisha? Walizaa watoto wengine tofauti na Yesu? Je, walikufa wakiwa na umri wa miaka mingapi? Walizikwa wapi?
AGANO LA KALE wamezingatia kuandika yote haya... Lakini AGANO JIPYA limepuuzia Ndio maana watu wengi wanajikuta wakisema: "INJILI ni ngumu sana kuielewa mpaka uvuviwe na Roho Mtakatifu" MATENDO 19:13: 20 na MATENDO 8:9:25 🙏
Je, waandishi wa AGANO JiPYA walijisahau au waliamua tu kufanya makusudi kutoandika kweli yote?
Nakuelewa jinsi hisia zako zinavyokutuma kuongea hivyo na hii inaweza kutokana na namna ambavyo waislamu wengi mmekuwa hamna muamko kwenye ishu nzima ya Elimu kiujumla hivyo kwenu Sayansi inaweza kuonekana ni kitu kikubwa kisichoeleweka kwa urahisi.Yani hayo maelezo yako ndio yanathibitisha nilichokisema jinsi unavyoichukulia sayansi, hebu soma hayo maelezo yako vizuri.
Unaposema sayansi inakubali haipo perfect, mara sayansi inatoa mwanya kuruhusu ukosoaji. Huoni tu unakuwa unaifanya sayansi kama dubwasha fulani hivi?
Sayansi haisemi wala kukosolewa, tafiti za kisayansi zinazofanywa na watu ndio husema hivi au vile na ndio maana unaweza kuzikosoa.
Sisi hatusemi Mungu hayupo kwasababu haonekani.Tuamini yupo Mungu,Imani ni bayana kwa mambo yasioonekana kwa macho,lakini ni dhahiri kama vile upepo uvumavyo kutoka kusini kwenda kaskazini au magharibi kwenda mashariki .Hatuuoni ila tunahisi!
Imani ya kweli ipo kwa kuamini Mungu yupi kati ya maelfu wanaoabudiwa duniani kote?Ukiamini Mungu yupo ili tu ikitokea kweli yupo u-save, hiyo si imani ya kweli, utakuwa unapoteza muda wako.
Ili kumpendeza Mungu lazima uwe na imani ya kweli kwamba yupo, siokuamini kwa namna ya kujikatia insurance ili kama yupo utoboe siku ya mwisho!
Elewa kuwa ni wewe ndio unaiona sayansi kama dubwasha sio mimi, maana hapo hata sijui kama unaelewa mie nachokieleza maana naona kama najadiliana na robot.Nakuelewa jinsi hisia zako zinavyokutuma kuongea hivyo na hii inaweza kutokana na namna ambavyo waislamu wengi mmekuwa hamna muamko kwenye ishu nzima ya Elimu kiujumla hivyo kwenu Sayansi inaweza kuonekana ni kitu kikubwa kisichoeleweka kwa urahisi.
Sayansi ni mchakato wa kujifunza wa jinsi tunaweza kuuelewa ulimwengu unaotuzunguka kwa njia ya testable na kukosoa nadharia ili kupata uelewa ulio bora zaidi.
Sayansi kukubali kuwa haijakamilika ni jambo la busara linalotoa mwanya kwa ukosoaji kwa sababu ni sehemu ya mchakato wa kujifunza pia.
Mfano wanasayansi wanapofanya utafiti huchapisha matokeo yao ili wanasayansi wengine waweze kuyapitia na kuyakosoa. Hii inaweza kusaidia kuwa matokeo ni sahihi na yanaweza kuaminika.
Kwa hiyo, badala ya kuiona sayansi kama dubwasha, ni bora kuiona kama mchakato wa kujifunza unaoendelea ambao unalenga kuboresha uelewa wetu wa ulimwengu. Ni njia ya kutafuta ukweli kwa kutumia ushahidi na mantiki.
Ni rahisi wewe kuona mimi nai praise sana Sayansi na kuchukulia kitu hicho kama cha kijinga kutokana na msingi wako wa maisha ulilenga kujikita zaidi kwenye madrasa.Elewa kuwa ni wewe ndio unaiona sayansi kama dubwasha sio mimi, maana hapo hata sijui kama unaelewa mie nachokieleza maana naona kama najadiliana na robot.
Kama ambavyo watu wanahukumiwa mahakamani ndio hivyo watavyohukumiwa kwa matendo wanayoyatenda wakiwa hai. Kama matendo ni mazuri utapata unachostahili kutokana na kusudio la Mungu kukuumba🤔
Wakati mwingine huwa najiuliza na kukosa majibu. Kwa mfano ukiwa na mwanao akawa na tabia za ajabu na kukera mfano Wizi, Umalaya, Ujinga ujinga nk.
Je utamchoma moto kwa sababu ya hizo tabia na matendo yake ?
Na maandiko matakatifu yanasema Mungu ni pendo yaani ana upendo na huruma sasa kwanini siku ya mwisho aje akubanike kwenye moto ?
Kuna nadharia nyingi sana ambazo huwa zinafikirisha na ukijifikirisha sana unakosa hata majibu.
Kuna Mungu mmoja tu wa kweli, sasa mtafute huyo ndio ujenge imani yako juu ya wengine. Ikiwa kuna dawa fake nyingi tu duniani, sio sababu ya wewe kusema hutatumia dawa tena. Utahakikisha unapata dawa isiyo feki ili kuokoa uhai wako!Imani ya kweli ipo kwa kuamini Mungu yupi kati ya maelfu wanaoabudiwa duniani kote?
Kwanini katika maelfu ya miungu kuwe na mmoja tu wa kweli tena yule ambaye wewe una muabudu?Kuna Mungu mmoja tu wa kweli, sasa mtafute huyo ndio ujenge imani yako juu ya wengine. Ikiwa kuna dawa fake nyingi tu duniani, sio sababu ya wewe kusema hutatumia dawa tena. Utahakikisha unapata dawa isiyo feki ili kuokoa uhai wako!
Nilionana nae ni kiwa kazini, sura kabisa huoni ila sauti unaisikia na vitendo vyake mpaka baadae unakuja kujikuta unacheka tuu . Kweli ni mfariji wa moyo.Ulionana naye wapi na una uhakika gani haikuwa hallucinations?
Hoja ya kusema ni bora uamini kuwa Mungu yupo kuliko kutoamini halafu ukifa ukakuta yupo. Ni hoja ya kijinga kwasababu inakufanya uendelee kuamini ujinga hata kama umeisha juwa ni ujinga. Ujinga ni kama ugojwa ukiuweka karibu yako lazima utajikuta umekuingia hadi kwenye damu.Makala hii nitaiweka kwa vipande kuepusha kero ya usomaji.
Moja ya hoja maarufu kutoka kwa watu wanaoamini Mungu (Theists).
Ni hoja ambayo imelenga kuweka matumaini ya mwelekeo katika maisha ili kuwafanya watu waone kuamini Mungu yupo ndio uchaguzi bora zaidi (rational) kwasababu haitakupa matokeo mabaya mwishoni.
Hii ni Analogy iliyopata sana umaarufu miaka ya 1640s na muazilishi aitwaye Pascal Wager.
Huyu jamaa alihoji kuwa ni vyema ukaamini kuwa Mungu yupo ukafa na usimkute kuliko kutokuamini halafu ukafa ukamkuta.
Pascal analaani kuwa kuamini kuwepo kwa Mungu ni tendo la busara zaidi kuliko kutokuamini kuwepo kwake, hata kama hatuna uhakika kuhusu kuwepo kwake. Hii ni kwasababu zifuatazo.
- Kama Mungu yupo na tutamwabudu, tutapata thawabu ya milele (kama ushindi mkubwa).
- Lakini kama Mungu hayupo na hatumwamini, hatutapata chochote (kama hasara ndogo).
- Kwa upande mwingine, kama Mungu yupo na hatumwamini, tutapata adhabu ya milele (hasara kubwa).
- Lakini kama Mungu hayupo na hatumwamini, hatutapata chochote (ushindi mdogo).
Hivyo, Pascal anasema kwamba kuamini kuwepo kwa Mungu ni tendo la busara zaidi, kwasababu unaweza kupata thawabu ya milele na kuepuka adhabu ya milele, hata kama hatuna uhakika kuhusu kuwepo kwake.
Swali: Je Atheists hawatuogopi siku ya mwisho kukutana na hukumu ya Mungu na kutupwa kwenye moto wa milele?
Hatuogopi kubaini kuwa hadithi za mitume zinazosimuliwa kuhusu Yesu na Muhammad kuwa ni za kweli na kwamba tumepoteza nafasi ya kuishi maisha ya milele peponi kwa kutoamini?
Je isingekuwa vyema Atheists kuwa upande salama wa kumuamini Yesu, Muhammad na Mungu kama backup just in case?
Ndio nakuuliza unajuaje kama haikuwa hallucinations?Nilionana nae ni kiwa kazini, sura kabisa huoni ila sauti unaisikia na vitendo vyake mpaka baadae unakuja kujikuta unacheka tuu . Kweli ni mfariji wa moyo.
Mungu yupo nakuambia kubali ukatae yupo
Labda Mashahidi wa Yehova(JW) walifikiria kama wewe ndio maana hawaamini wenye dhambi watabanikiwa kwenye moto wakifa bali watapotea tu.🤔
Wakati mwingine huwa najiuliza na kukosa majibu. Kwa mfano ukiwa na mwanao akawa na tabia za ajabu na kukera mfano Wizi, Umalaya, Ujinga ujinga nk.
Je utamchoma moto kwa sababu ya hizo tabia na matendo yake ?
Na maandiko matakatifu yanasema Mungu ni pendo yaani ana upendo na huruma sasa kwanini siku ya mwisho aje akubanike kwenye moto ?
Kuna nadharia nyingi sana ambazo huwa zinafikirisha na ukijifikirisha sana unakosa hata majibu.
Sasa kuamua kuabudu miungu feki au ya kweli unabaki uamuzi wako. Ndio maana hata wafanyabiashara wanapokuuzia kitu watakwambia ipo original au feki!Kwanini katika maelfu ya miungu kuwe na mmoja tu wa kweli tena yule ambaye wewe una muabudu?
Umejaribu kufikiria hao wanaoamini miungu wengine wao wanaichukuliaje miungu yao?
Je nao hawapati perception kama yako kudhani kwamba Mungu wao pekee ndio wa kweli huku miungu mingine iliyobaki ni ya uongo?
Sasa tunapotaka kufika hitimisho kujua yupi yupo sahihi, tutatumia kigezo gani kupata ukweli??