Je, kweli ni bora kuamini Mungu yupo halafu siku ya mwisho usimkute, kuliko kutoamini halafu ukamkuta?

Je, kweli ni bora kuamini Mungu yupo halafu siku ya mwisho usimkute, kuliko kutoamini halafu ukamkuta?

Chukua mfano mdogo tu kwamba huko zamani kabisa watu walitumia tiba zao za asili kutibu maradhi yao ila kama ungewauliza wakati huo waeleze na kuthibitisha jinsi hizo dawa zinavyoweza kutibu wasingeweza ila zilikuwa zikitibu, kukosa uthibitisho wa kisayansi kuelezea hizo tiba haikufanya kuwa hizo tiba hazikuwa za kweli.
Hata huko zamani mtu akinywa muarobaini au quinine uthibitisho ulikuwepo na maelezo rudimentary yalikuwepo. dawa za kisasa zilizopo leo zimetokana wanasayansi kujifunza kwa muda mrefu tabia za vidudu na dawa za asili, sio kwamba walilala wakaja tu na dawa mpya. Mti wa muarobaini na quinine upo na unaonekana, hata kama hakukuwa na maelezo ya kutosha ya sayansi kuhusu muarobaini, quinine au majani ya kufukuza mbu(repellants) hao waliokuwa wanatumia walikuwa wanajua content iliyo katika hivyo vitu ndio ilikuwa inafanya kazi, waliendelea mbele zaidi wakawa wanajua watumie vikombe vingapi kwa ukubwa gani wa tatizo. Tatizo litaanza utakopesema mtoto anaumwa tumbo kwa sababu aliangaliwa kwa jicho baya na jirani lakini hata kulielezea hilo jicho baya huwezi. Mtu atakopesema amepewa utajiri na mungu lakini hawezi kusema kwa nini amepewa yeye na sio mwingine n.k
 
Wewe unahubiri tu kila siku wala haujawahi thibitisha uwepo wa Mungu , unachokifanya unataka niamini mahubiri yako ,wakati mimi sitaki kuamini nataka nijue sijui kama unaelewa🤔

Hapa ndipo huwa nawaona hamko makini na hii mijadala, kwa ufupi hamna mnachokijua.

Kusema kwako bahubiri hakubadilisho maana ya kuwa wewe huna uwezo wa kukosoa ninacho kiandika.

Unapo ongelea kujua hata sisi kwenye kuamini tunajua hicho tunachokiamini. Shida yenu hamsoni na hamjui maana ya haya maneno.

Uwepo wa Mungu uko wazi kwa mtu mwenye akili na kutumia akili, hili tumeshalifanya sana humu ndani.
 
Scars
Kiranga
min -me
Infropreneur

Mmekua mnapinga uwepo wa Mungu kila siku kwa kuuliza maswali yale yale bila kuja na kitu kipya
Sasa naomba niwaulize kama mmeweza kujua kuwa hakuna Mungu,
Madai ya uwepo wa Mungu yametoka kwenu nyie waamini Mungu.

Ninyi Theists ndio mnadai kuna Mungu.

Hivyo ninyi waamini Mungu ndio mna jukumu la kuthibitisha madai yenu ya uwepo wa huyo Mungu mnayedai yupo.

Sisi Atheists tunapinga madai yenu ya kusema kuna Mungu.

Hivyo ninyi Theists ndio mnapaswa kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu mnayedai yupo.

Mkishindwa kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu mnayedai yupo, Ni kwamba madai yenu ya kusema kwamba kuna Mungu ni madai ya UONGO.

Na huyo Mungu mnayedai yupo, HAYUPO.
pia kuna uwezekano mmeshajua Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake
Naomba mje kutueleza chanzo cha huu ulimwengu na viumbe vyake ni nini?
Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe na chanzo, Hata chanzo cha kila kitu lazima kiwe na chanzo chake kingine.

Pasiwepo kitu chochote kile kilicho jitokeza chenyewe tu pasipo chanzo, Maana kitazua maswali ya kiliwezaje ku exist chenyewe tu pasipo chanzo.

Hivyo kutakuwa na vyanzo vingi visivyokuwa na mwisho Endless to infinity...

Ili ulazima huu, U apply kwa kila kitu kilichopo kiwe na chanzo.

Na kama si lazima kwamba kila kitu kilichopo kina chanzo, Hata Ulimwengu, Viumbe na vitu vyote vilivyomo except man-made things Havina na havihitaji kuwa na chanzo.

Do you get the point?

Huwezi kumu exclude huyo Mungu kwenye logic ya kuwa na chanzo, Halafu uanze kufosi kwamba ulimwengu una chanzo.

Ukifanya hivyo utakuwa unafanya Special pleading fallacy.
Screenshot_20241218-151311_1.jpg

Nafkiri sisi wenye imani ya uwepo wa Mungu tuanze kuwa challenge hawa Atheist kwa kuwahoji maswali fikirishi sio kila siku kubishana Mungu yupo au hayupo
Hukatazwi kuwa na imani juu ya uwepo wa Mungu.

Hukatazwi kuamini, kuamini ni haki yako ya kikatiba. Hata ukiamua kuamini mawe, milima, mapango, majabali makubwa kama Mungu wako, huo ni uhuru wako kabisa kufanya hivyo.

Kuamini unaweza kuamini hata uongo Lakini ukianza kudai kwamba hicho unacho kiamini ni ukweli lazima utoe uthibitisho ili tufanye uhakiki.

Ukianza kudai kwamba imani yako ina ukweli lazima uthibitishe na utoe uthibitisho wenye uhakika. Ili tupime ukweli wa hiyo imani yako.

Usipofanya hivyo, imani yako inabaki ya kufikirika na kusadikika tu. Isiyo na ukweli wowote ule.
 
Kutoamini na umkute ni poa zaidi. Mungu ni mwemye huruma kwa watoto wake, atakusamehe. Utakuwa umeshaponda raha zote za dunia, utakuwa sawa tu na yule aliyekuwa anapasua sala mara kwa mara.
Nimecheka kwa nguvu aisee, na hio ndio pointi ya muhimu
 
Bora kuamini kuliko kuto amini.
Kwa nini uhitaji kuamini Mungu yupo, Badala ya kujua Mungu yupo kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho?

Huyo Mungu akijulikana yupo kwa uhakika na uthibitisho itampunguzia nini kuwa Mungu?

Huyo Mungu kama yupo kwa nini ajifiche huko alipo, Halafu atake aaminiwe na watu akiwa mafichoni?

Huyo Mungu kama yupo, Anacho ogopa kujulikana hadharani ni nini?
 
Hivi umesoma vizuri nilichokiandika ? Kwanini kwanza unahisi lazima kuwe na chanzo?

Unapo niuliza kwanini nahisi, hili ni kosa. Bali Mimi nina uhakika ya kuwa lazima chanzo kiwepo sababu hakuna kinyume chake.

Labda kama hutumii akili, naomba unipe sababu tatu ambazo zinalazimika au chanzo kisiwe cha lazima kuwepo.
 
Hili swali nafikiri sio la kwako , na sita kuwa na muda wa kurudia kujibu kitu nilichokijibu huko juu.
 
Kwa nini uhitaji kuamini Mungu yupo, Badala ya kujua Mungu yupo kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho?

Huyo Mungu akijulikana yupo kwa uhakika na uthibitisho itampunguzia nini kuwa Mungu?

Huyo Mungu kama yupo kwa nini ajifiche huko alipo, Halafu atake aaminiwe na watu akiwa mafichoni?

Huyo Mungu kama yupo, Anacho ogopa kujulikana hadharani ni nini?
Ishi kutokana na imani yako.
 
Ishi kutokana na imani yako.
Kwa nini uishi kwa imani?

Kwa nini usiishi kwa kujua?

Hivi wavumbuzi na wanasayansi wangeishigi kwa imani tu. Bila kudadisi, Bila kutaka kujua, Bila kufanya tafiti za kina.

Je Tungefikia maendeleo tuliyonayo leo hii kwenye nyanja mbalimbali za maisha kwa hiyo imani tu?
 
Scars
Kiranga
min -me
Infropreneur
Nyani Ngabu

Mmekua mnapinga uwepo wa Mungu kila siku kwa kuuliza maswali yale yale bila kuja na kitu kipya
Sasa naomba niwaulize kama mmeweza kujua kuwa hakuna Mungu, pia kuna uwezekano mmeshajua Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake
Naomba mje kutueleza chanzo cha huu ulimwengu na viumbe vyake ni nini?

Nafkiri sisi wenye imani ya uwepo wa Mungu tuanze kuwa challenge hawa Atheist kwa kuwahoji maswali fikirishi sio kila siku kubishana Mungu yupo au hayupo
Hakuna ajuwaye kama Mungu yupo au hayupo. Ila tunachqkataa ni kuaminishwa uongo kuwa Mungu kaandika vitabu vya kutumia kumuabudu. Wakati vitabu hivyo vimeandikwa na watu kama mimi na wewe. Tunakataa kuamini Mungu kama yupo kwa sababu hatujaona kitu chakutuaminisha uwepo wake. Hata kama yupo basi sisi sio viumbe mhim kwake kama vitabu vya dini vinavyo tuaminisha. Au kama yupo basi hana nguvu au uwezo unao elezewa kwenye vitabu vya dini. Kuamini kitu usicho kijuwa ni ujinga. Ukisema unaamini Mungu maana yake huna haja ya kuishi tena, inabidi usibili tu maagiza ya Mungu.
 
Scars
Kiranga
min -me
Infropreneur
Nyani Ngabu

Mmekua mnapinga uwepo wa Mungu kila siku kwa kuuliza maswali yale yale bila kuja na kitu kipya
Sasa naomba niwaulize kama mmeweza kujua kuwa hakuna Mungu, pia kuna uwezekano mmeshajua Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake
Naomba mje kutueleza chanzo cha huu ulimwengu na viumbe vyake ni nini?

Nafkiri sisi wenye imani ya uwepo wa Mungu tuanze kuwa challenge hawa Atheist kwa kuwahoji maswali fikirishi sio kila siku kubishana Mungu yupo au hayupo

Swali lako ni logical non sequitur fallacy.

Nakuuliza swali.

Unaweza kujua jibu fulani si sahihi kabla ya kujua jibu sahihi?

Mfano, ikiwa Juma ana miaka 30 leo, unaambiwa umtafute mama mzazi wa Juma. Unaambiwa kuna binti mchanga anaitwa Amina, ana miezi 6 leo, unaambiwa huyo binti Amina ndiye mama mzazi aliyemzaa Juma, mwanamme mwenye miaka 30 leo.

Hapo unaweza kujua kuwa huyo Amina hawezi kuwa mama yake Juma bila ya kumjua mama yake Juma ni nani?
 
Ndio naweza, Hoja hapo ni nini?
 
Ndio naweza, Hoja hapo ni nini?
Hoja ni kwamba, habari ya kujua ulimwengu ulianzaje haina uhusiano wowote na habari ya kujua Mungu yupo.

Nikijua mambo fulani ya msingi, naweza kujua Mungu hayupo, na si chanzo cha ulimwengu, bila ya kujua chanzo cha ulimwengu ni nini.

Kama vile ninavyoweza kujua Amina si mama yake Juma bila kujua mama yake Juma ni nani.

Naweza kujua jibu fulani si sahihi, bila ya kujua jibu sahihi ni lipi.

Katika mantiki ukitumia elimination method kutafuta jibu unaanza kuyaondoa majibu yasiyo sahihi mpaka unalifikia jibu sahihi.

Sasa, katika kutafuta chanzo cha ulimwengu, tumefanya elimination method, tunatafuta jibu sahihi, hatujalipata bado, lakini jibu la Mungu tumeshaliona si sahihi, na tumeliondoa.

Atheism ni kusema Mungu hayupo. Atheism si kusema najua chanzo cha ulimwengu ni nini.

Swali linalomhusu atheist si swali la chanzo cha ulimwengu ni nini, maana hajasema anajua chanzo cha ulimwengu ni nini.

Swali linalomhusu atheist ni, unajuaje Mungu si chanzo cha ulimwengu? Hilo ndilo swali fair kwa atheists, kwa sababu atheism ni kusema Mungu hayupo, na ukisema Mungu hayupo, unatakiwa uwe na uwezo wa kuonesha Mungu hajaumba ulimwengu (kwa sababu hayupo) hutakiwi kusema ulimwengu umeanzaje (kwa sababu hujawahi kusema unajua ulimwengu umeanzaje).

Ukiuki,a atheists chanzo cha ulimwengu ni nini unawapa swali lisilo lao.

Hilo ni swali la cosmogonists.

Ushawahi kusikia neno hili cosmogony ?
 
Scars
Kiranga
min -me
Infropreneur
Nyani Ngabu

Mmekua mnapinga uwepo wa Mungu kila siku kwa kuuliza maswali yale yale bila kuja na kitu kipya
Sasa naomba niwaulize kama mmeweza kujua kuwa hakuna Mungu, pia kuna uwezekano mmeshajua Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake
Naomba mje kutueleza chanzo cha huu ulimwengu na viumbe vyake ni nini?

Nafkiri sisi wenye imani ya uwepo wa Mungu tuanze kuwa challenge hawa Atheist kwa kuwahoji maswali fikirishi sio kila siku kubishana Mungu yupo au hayupo

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikiwa kama Abzu hakuuumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikiwa kama Ahura Mazda hakuuumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikama Akongo hakuuumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikiwa kama Anansi hakuuumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikiwa kama Alatangana hakuuumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikiwa kama Aiomun-Kondi hakuuumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikiwa kama Anulap hakuuumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikiwa Aramazd hakuuumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikiwa kama Atua Fafine hakuiumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikiwa kama Atum hakuuumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikiwa kama Brahma hakuuumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikiwa kama Enki hakuuumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikiwa kama Damballa hakuuumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikiwa kama Odin hakuuumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikiwa kama Ukunlunkulu hakuumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikiwa kama Makemake hakuuumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikiwa kama Uranus hakuuumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikiwa kama Flying Spaghetti Monster hakuumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikiwa kama Tupã hakuumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikiwa kama Tonacatecuhtli hakuumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikiwa kama Prajapati hakuumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake kama Mbombo hakuuumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikiwa kama Viracocha haikuumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikiwa kama Q'uq'umatz hakuuumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikiwa kama Wisakedjak hakuuumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikiwa kama Pacha Kamaq hakuuumba?

Nini Chanzo cha huu uliwengu na viumbe vyake ikiwa kama maelfu ya miungu wengine ambao kwenye list hapo hawapo kuwa hawakuumba?

"Naomba mje kutueleza chanzo cha huu ulimwengu na viumbe vyake ni nini?"

Hatujui nini chanzo cha huu ulimwengu lakini tuna hakika haujaumbwa na Mungu yeyote, na wako akiwemo.
 
Sasa kuamua kuabudu miungu feki au ya kweli unabaki uamuzi wako. Ndio maana hata wafanyabiashara wanapokuuzia kitu watakwambia ipo original au feki!
Ndio maana nikakuuliza nijue ni kipi ulichotumia kujua Miungu feki ambacho waumini wa hiyo Miungu wameshindwa kukitumia kukijua u fake wa Mungu wao ili nao waachane na Mungu wao feki waungane kuabudu Mungu wako ambaye ni original?
 
Imani ya Mola haitaki kubahatisha, hata ukiamini kwa lengo la kwamba ukimkuta iwe kheri kwako, hapa Imani yako sio sahihi na utaenda motoni tu. Bali Imani ya Mola inataka elimu, mazingatio na uhakika usilo kuwa na shaka kabisa, kwa ufupi ni mchakato wa muda mrefu wenye kuambatana na utiifu na kumpwekesha yeye katika ibada.

Ndio maana Allah anataka watu wenye kutafakari kwa kina na wenye mazingatio.
Kwani tafsiri ya imani ni nini?

Na uweke chanzo ulipoitoa hiyo tafsiri ili tupate rejea.
 
Ni kusadiki kwa moyo na kutamka kwa ulimi juu ya kauli au matendo fulani yenyewe kufungamana na elimu yaani ujuzi.
Hii ni kwa mujibu wa kamusi gani? Au ni perspective yako?
 
Back
Top Bottom