Je, kweli ni ngumu kuishi na mwanaume aliyewahi kuoa?

Kwa msaada wa akili mnemba
Miss Aaliyyah
Ni kweli kwamba kuna changamoto ambazo zinaweza kutokea wakati mwanamke anaishi na mwanaume aliyewahi kuoa, hasa ikiwa kuna masuala yasiyokuwa yametatuliwa kutoka ndoa ya awali. Mojawapo ya changamoto hizo ni kama zifuatavyo

1. Masuala ya kihisia: Mwanaume anaweza kuwa bado anashughulikia majeraha ya kihisia kutoka kwa ndoa ya awali, na hii inaweza kuathiri uhusiano wa sasa.

2. Mahusiano na familia ya awali: Ikiwa kuna watoto au mahusiano ya karibu na mke wa zamani, yanaweza kuleta migogoro au changamoto katika uhusiano mpya.

3. Matarajio ya tofauti: Mwanaume aliyewahi kuoa anaweza kuwa na matarajio au mazoea yanayotokana na uhusiano wa awali, ambayo yanaweza kugongana na matarajio ya mwanamke mpya.

4. Kumlinganisha na mke wa zamani: Hili linaweza kuwa tatizo ikiwa mwanaume ana tabia ya kulinganisha mwenza wa sasa na aliyekuwa naye awali.
 
Mimi toka nimechomoka kwa yule nahisi kama nimetoka gereza la ADX Florence la huko colorado , yani mtato wa mtu anikiambia habari za kumuoa ninashtuka sana kwa kwel😂😂
 
Hapo nimekuelewa Sasa
Ikitokea kuwa na mwanaume wa namna hii vipi unaweza kumuweka kwenye mstari maybe mwanamke kama ana weakness au huyu mwanaume analinganisha mwanzo na Sasa hiv
 
Member wengi humu nimewawekea Standard zao kwahiyo acha kujipa Umuhimu wa kunielekeza jinsi ya kumjibu mtu. Ninavyo mjibu Lucas Mwashambwa ni tofauti nitakavyo mjibu Mshana. Au nitakavyomjibu Faiza Foxy ni tofauti nitakavyo mjibu Cute Wife.
 
Mwanamke ndo atakuwa na jukumu la kuamua kupigania ndoa au kushindwa akatembea
Mimi binafsi kwa muda ndio nimekua nikipigania ndoa mpaka sasa nimenyoosha mikono.
Huko nyuma katika moja ya vikao vya usuluhishi nilishawahi tamkiwa na wife mbele ya baba angu mzazi kuwa "aniache aone kama sijapata mtu ndaninya siku mbili tu atakaenipa maisha mazuri zaid ya haya" 😅
Kwasasa nimeamua kunyoosha mikono
 
Uzoefu, unaonesha hili jambo, Kwa kiasi kikubwa linataka kufanana na ishu ya Kuoa Mwanamke aliyewahi kupitia mahusiano mengi kabla hajaolewa nawe.

Kuna ile tendency ya kufanya ulinganisho.

Kwamba alipotoka alikuwa anapewa huduma fulani fulani, ambazo wewe humpatii.

Kuna moment alikuwa anafurahia huko alipokwepo, lakini kwako asipate.

Kwahiyo inapotokea unam-treat tofauti anaweza kuanza kukulalamikia bayana ama kupitia marafiki zako.

Hata hivyo ni rahisi sana kuweza kuishi na kumkamata Mwanaume wa hivi.

Kwanza ishi naye Kwa kumheshimu, jitahidi usimvunjie heshima yake kama Mumeo na Baba wa watoto wako.

Pili mpe mapenzi yatakayomfanya Baba wa watu asione Wala kukumbuka kwingine.

Tatu, kuwa na kauli nzuri Kwa Mumeo, hata kama amekukosea, mueleze taratibu. Kwa kuwa yeye ni mtu mzima, najua ataelewa.

Kila la heri Mjukuu, kumbuka Kadri mvinyo unavyozidi Kulala ndivyo unavyozidi kuwa mtamu
 
Hapo nimekuelewa Sasa
Ikitokea kuwa na mwanaume wa namna hii vipi unaweza kumuweka kwenye mstari maybe mwanamke kama ana weakness au huyu mwanaume analinganisha mwanzo na Sasa hiv
Now sasa ita depend na maturity ya mwanaume. Kama bado ana linganisha means haja move on, and hiko si kitu kizuri.

Mwanaume ambae ametoka huko anatakiwa awe mature enough kujua kila mwanamke ana different behaviour na namna ya kuwaelekeza nayo ni different
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…