Status
Not open for further replies.
Wajinga ndio waliwao,hao hawanatofauti na wanao bet.
 
Hii haina tofauti na ile waliyokua wanasema ukiunganisha watu unalipwa ila sasa wewe ukijiunga wanakuambia weka laki 5 au zaidi, alafu ukiweka wanakupa vipodozi uteseke kuviuza huku wanakuambia tafuta mtu mwingine umuunganishe upate kamishen na ofa ya safari za kupanda pipa na marupurupu ya hapa na pale.


Ila sasa ukiwachunguza utagundua hata wanaokuambia hivyo wanaonufaika kupiga mamilioni wana maisha magumu sana na semina ikiisha mnaenda kugombania mihogo
 
Maelezo yao:

I
LEWE LBL

πŸ’ πŸ’ TANZANIA ADVERTISING MEDIA LIMITED
πŸ’ πŸ’ 

βœ…LBL Imeanza tangu mwaka 1967

βœ…LBL
kirefu chake ni Leo burnett London

♻️Hapa Tanzania imeingia mwaka huu mwezi wa pili baada ya kualikwa na serikali yetu ya jamuhuri ya Muunguano wa Tanzania. Baada ya usajili na kukamilisha taratibu zote ikaanza kufanya kazi rasmi mwezi wa saba mwaka huu.

♻️Hapa manispaa ya Morogoro mtu wa kwanza/muasisi wetu ni Dr David Lugomela ambaye ndiye kiongozi wetu mkuu na kutushirikisha fursa hii.

♻️ LBL inafanyaje kazi.
Kumbuka ni kampuni inayohusiana na utangazaji. Ni kampuni iliyobobevu duniani.
1. Makampuni mengi makubwa ya filamu dunia. Wale wapenzi wa movie mtaelewa hili. Mfano.
πŸŒ€ *Paramount,
πŸŒ€20th century Fox,
πŸŒ€ destiny* ,
πŸŒ€Warner Brothers,
πŸŒ€DreamWorks picture,
πŸŒ€Universal Picture
πŸŒ€MGM Picture na mengine mengi
Yameweka ubia na kampuni ya LBL isaidie kutangaza matangazo yao ya movie na filamu ili yawafikie watu wengi duniani.
Hivyo basi ili kampuni ya LBL ifanye jukumu hilo vyema wakaona iajiri watu wengi ambao watatazama matangazo ya movie na hapo idadi ya watu wengi itafikiwa. Ndo mana inasisitiza kualika watu zaidi

πŸ”° _Baada ya muda wanapeleka kwa makampuni na kuwaonesha mfano:...........
_
πŸŒ€*PARAMOUNT * movie yako hii imetazamwa na watu milioni 10.5 mwezi huu.( Utakuta walikubaliana hivi kwamba Kila viewers mmoja( mtu mmoja aliyetazama) Lbl watalipwa Dola 1. Hebu jaribu kuchukua Dola 1 Γ— mil 10.5 LBL wanaingiza. Kwanini wasirudishe fadhira. Hivyo ndivy LBL Inavyofanya kazi.

βœ…UZOEFU
_Wengi wetu twajua nyakati hizi wengi hupata pesa Kwa mitandao.

_Diamond huingiza fedha YouTube kwa kuwa tu na viewers wengi.

_MiladAyo anaingiza fedha Kwa kuwa tu na viewers wengi

πŸ–ŠοΈNote vipi wewe unayetazama kazi zao unalipwa ? Au unagharamika bando lako?

♻️LBL UNAPOVIEW video hawakuachi hivihivi. Kwasababu wanajali ikiwa tunawaingizia fedha nyingi sana basi wakaona nasi tupate kifuta jasho. Ambacho kwetu kinathamani Kubwa, kwa level tofauti kama ifuatavyo........... πŸ‘‡

1️⃣ P1 LEVEL

_πŸ’ Ukiweka 50,000
πŸ’ Unapewa picha 5 za kuangalia
πŸ’ Kila picha unalipwa 335
πŸ’ Kwa siku unalipwa 1675
πŸ’ Kwa mwezi unalipwa 50250
πŸ’ Kwa mwaka 611,375 /=_

2️⃣ P2 LEVEL

πŸ’ Ukiweka 150,000
πŸ’ Unapewa Picha 10 za kuangalia
πŸ’ Kila picha unalipwa 500
πŸ’ Kwa siku unalipwa 5000
πŸ’ Kwa mwezi 150,000
πŸ’ Kwa mwaka 1,825,000
πŸ’ Hivyo 150,000 itakuwa imezaa sh 1,675,000

πŸ’ Ukiweka 540,000
πŸ’ Unapewa picha 15 za kuangalia
πŸ’ Kila picha unalipwa 1200
πŸ’ Kwa siku unalipwa 18000
πŸ’ Kwa mwezi 540,000
πŸ’ Kwa mwaka 6,570,000
πŸ’ Hivyo 540,000 itakuwa imezaa 6,030,000 /

✳️ILI kujiunga nijulishe nikutumie Link.

✳️Kujiunga na LBL * ni bure kabisaa ila ili uwe mwajiriwa au mfanyakazi rasmi wa LBL unatakiwa kuwa na mtaji wa *50000/= kwa ngazi ya P1 , 150000/= kwa ngazi ya P2, na 540000/= kwa ngazi ya P3 Kumbuka hakuna biashara unayoweza ifanya kama hauna mtaji ni lazima uwe na mtaji. ukikamilisha account yako nitakuadd kwa group la WhatsApp
UTAKUWA TAYARI UANZE KAZIπŸ’ πŸ’ 

πŸ”°MWISHO
.
✳️ LBL MAFANIKIO ni hakika
✳️LBL sio matapeli. Tuwe makini na matapeli watakao jitokeza na kuharibu sifa ya kampuni.

✳️Hii ni kazi sio kamali au bahati nasibu .
✳️Usipoview huwezi pata pesa Kwa sababu nao hawajapata pesa kupitia wewe."
Mwisho wa kunukuu.
_____________________________


Baada ya kupitia maelezo haya nikaanza kuchimba kuhusiana na kampuni ya LBL:

Leo Burnett London (LBL
) ni tawi la Leo Burnett, ambayo ni mojawapo ya makampuni makubwa ya matangazo duniani, iliyoanzishwa na Leo Burnett mwaka 1935 huko Chicago, Marekani. Leo Burnett London ni sehemu ya McDonald's, Procter & Gamble, Coca-Cola, na wateja wengine wakubwa.

Historia ya LBL: Leo Burnett London imejizolea umaarufu kwa kutoa ubunifu wa matangazo na mikakati ya uuzaji kwa wateja wake. Kampuni imejulikana kwa kuunda kampeni maarufu na za ufanisi. Kwa mfano, wameunda matangazo maarufu kama ya "Proud to be a Coke" kwa Coca-Cola na "Because You're Worth It" kwa L'OrΓ©al.

Kazi ya Leo Burnett London: Leo Burnett London inajivunia kuwa na timu ya wabunifu na wataalamu wa mikakati ambao huunda matangazo ya kuvutia na yenye athari kubwa. Kampuni ina mchanganyiko wa ubunifu na utafiti wa soko ambao husaidia wateja kufikia malengo yao ya biashara.

Pesa Wanazopata: Leo Burnett London inapata pesa kupitia huduma za utangazaji, mikakati ya uuzaji, ubunifu wa matangazo, na huduma nyingine za ushauri wa biashara kwa wateja wao. Hii inajumuisha:

1. Malipo ya Kampeni za Matangazo: Wanapofanya kampeni kwa wateja, kampuni hulipwa kulingana na ukubwa na aina ya kampeni.

2. Konsati na Ushauri: Wanatoa ushauri wa kimkakati na huduma za ubunifu kwa wateja kwa malipo ya huduma hizi.

3. Kuuza Huduma za Utafiti: Wateja wanalipa kwa tafiti za soko na uchambuzi wa maoni ya walaji.

Kwa hiyo, mapato yao yanatokana na huduma zao za utangazaji na mikakati, siyo kutoka kwa malipo ya views au kitu kingine cha moja kwa moja kutoka kwa watumiaji wa media.

Hivyo: Leo barnet london wao ndiyo hulipwa na kampuni tofauti kwa kufanya ubunifu wa matangazo tofauti tofauti kwenye Radio, channel za Tv, mitandaoni n.k ikiwemo movie Trailors.

Zingatia kitu kimoja hapo wao ndiyo wanalipwa hawalipi.

Nikaona niulizie zaidi kupata uhakika, wote tunajua chatGPT inakusanya taharifa kila sehemu ya mtandao, majibu yakawa hivi;

Ieleweke LBL sio matapeli wala hawahusiki na kulipa kwa namna yeyote ile.

Ila hao jamaa wanaotoa matangazo haya nfiyo matapeli, wanachafua jina la kampuni hiyo.

Cc: NoncChalant
 
Unataka kiingilio Tena..msenge kweli we,fanya kazi hakuna pesa Bure,utapelekewa moto mkubwa
 
Bado mnaiba na kuibiwa kijinga namna hii!?
 
Binafsi nimekuelewa ila sijakuamini!
 
Wazee wa Qnet hao πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ ...Zipo kwa ajili ya upigaji ,
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…