Je, leo inaweza kuwa ndio ile siku? Ukweli halisi ni upi? Nini hasa kilitokea na kwanini tulijulishwa baada ya siku 5?

Kuna wimbo wa Lucky Dube siukumbuki jina ila kuna verse wanaimba Thank you father for making politician lie to us.

Nikambuka kuna mmoja akiwa sehemu takatifu macho makavu kuwa jamaa yuko fit ofisini anachapa kazi,

Wanasiasa hamuendi mbinguni
Atakuwa kadanganywa na yeye akadanganya hivyo sio kosa lake ni amekoseshwa ila baada ya kujua alikoseshwa, na baada ya kuujua ukweli halisi wa kilichotokea tarehe 12 Machi, alipaswa kuomba radhi kwa ku apologise or just say sorry.

Kitendo cha kusema uongo mchana kweupe tena kwenye kadamnasi ya watu na ukajua ulisema uongo mkubwa vile, nchi za wenzetu ni unawajibika!.

Kitendo cha kutoomba radhi ni dharau kubwa kuwa wote wale aliowadanganya anawaona ni majuha hawastahili kuombwa radhi.
P
 
Bro pascal viongozi wetu wameshatugeuza misukule wanajua hatuwezi kuwafanya kitu
 
Alikufa kwa complications za COVID zilizosababisha tatizo la moyo kuwa kubwa zaidi. Ikumbukwe tatizo la moyo alikuwa nalo tangu akiwa mwanafunzi UDSM. Ilichukua muda kutangaza kwani kulikuwa na mambo mengi ya kuweka sawa kati ya viongozi wa serikali na hasa wale wa mtandao wake uliokuwa mkubwa. Muda wa siku 5 ulitumika kufanya uharibifu na uhalifu mkubwa hasa wa kifedha na hili mama analijua ila yupo chini ya “kiapo” flani na itamwia vigumu kuwawajibisha waliohusika na yote. Yote haya yalifanywa kwa kisingizio cha usalama wa Taifa. Mengi yatafichuka taratibu.
 
Tarehe umeiweka kiufundi sana. Ijapokuwa sidhani kama kulikuwa na ulazima wa kuandika hapa.

Heshima yako mkuu!

Tangu ulipoamua kuachana na siasa za Tanzania umekuwa unaonekana jamvini kwa machale.
 

Tofautisha hoja tofauti na hisia Zako za kijinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…