GE2025 Je, Maandamano yamefeli mpaka sasa? Barabara nyeupe, mikwara yote kwisha

GE2025 Je, Maandamano yamefeli mpaka sasa? Barabara nyeupe, mikwara yote kwisha

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Nilitengeneza ka bango kangu ,asubuhi saa moja nimechungulia getini niwaone wenzangu tuzame kitaa wapi .
Nawapigia simu wanangu tuliokuwa tunakubaliana lazima liwalo na liwe Kama ajira tuwaachie wao ,kichekesho mmoja ameanza kunisimulia mama yake alivyomsomesha kwa tabu .

Aise kiukweli nimeishiwa pawa ,nitoe wito Tena na Tena kwa serikali tafadhali muachieni Hamphrey polepole wengine maisha yetu hayaendi bila yeye .

Free polepole
 
IMG_0243.jpeg
 
Kila siku ilikuwa mikwara kibao tarehe 29 tarehe 29 leo hamna hata sisisimizi barabarani nyumbu zote zimekaa zinafuatilia kinachoendelea kwenye simu hii ni Kali ' hahahaha mtanzania ni mnafiki sana acha wakina Abduli wale mabilioni yao kwa raha bhana hii inaitwa Raha jipe mwenyewe 🤣🤣🤣🤣🤣
Hahahaha akina Retired Lord Denning Salary Slip
qKila siku ilikuwa mikwara kibao tarehe 29 tarehe 29 leo hamna hata sisisimizi barabarani nyumbu zote zimekaa zinafuatilia kinachoendelea kwenye simu hii ni Kali ' hahahaha mtanzania ni mnafiki sana acha wakina Abduli wale mabilioni yao kwa raha bhana hii inaitwa Raha jipe mwenyewe 🤣🤣🤣🤣🤣
technically Braza j JokaKuu
 
Nyumbu ni hatari sana wakiwa mtandaoni wanaweza kukupiga mikwara hadi ukafa wa maneno tu ila mwambie Nyumbu aje kwa ground atekeleze anachoandika mtandaoni atakuachia vumbi tu hutamuona.

Mangekimambi analia huko nyumbu zimemuachia vumbi tu
Na vile alivyoacha udaku iliyokuwa inamuingizia pesa sijui atakuwa kwenye Hali gani hawa ndio keyboard warrior
 
Mpo salama!

Kwa waliopo Dar hii haijawahi kutokea. Hata siku ya jumapili haiwagi hivi. Barabara ni nyeupe sana sijapata kuona. Fikiria Morogoro road unaweza ukavuka barabara ukiwa umefumba macho. Barabara ambayo kwa hapa Tanzania ndio iko busy 24/7 kwa siku zingine kwani ndio barabara lango la mji wa Darisalama.

Daladala zipo moja moja yaani kila baada ya dakika kumi hivi wakati siku nyingine hapakaliki.

Siku ya leo kama Lisu akichukuliwa akawekwa ndani ya gari siri ya nyuma. Ili aonyeshwe hali ilivyo hakika ataumia kuliko alivyopigwa risasi au kuliko alivyowahi kupata maumivu wakati wowote katika maisha yake.

Hata Polisi, Askari na serikali hawajategemea mambo yawe rahisi kiasi hiki. Wenyewe hawaamini kama Watu wangeweza kuwasaliti wengine kwa kiwango hiki. Hii ndio tafsiri ya Usaliti.

Kwenye maisha yako. Hakuna jambo baya kama kutetea watu wajinga na maskini wasiokuwa tayari kutetewa.

Kwa hizi barabara zilivyo unaanzia wapi kuandamana. Ni nyeupe ajabu. Nilitokea Kimara mpaka ubungo kweupe kuna doria za hapa na pale za askari.
Nimeenda njia ya Mwenge, kisha makumbusho, nimerudi Magomeni mpaka mjini, posta kumepoa. Aiseeh!

Yaani hapa ukibeba bango lako hata askari wenyewe watakucheka sana. Barabara zimekumeza. Unakuwa kioja na kituko.

Nimehoji baadhi ya askari huku kwenye doria kutaka maoni yao kuhusu hali ilivyo wenyewe wanashangaa sana. Wanasema hata kama ni uoga sio wa kiwango hiki. Ni uoga uliopitiliza sana.

Zaidi wanasema wanajisikia uchungu kwa taifa kupata aibu kwa wananchi wake kushindwa hata kujitokeza walau pawe busy na vyombo vya kimataifa vipate kazi ya kufanya.

Upande wa wapiga kura hali yao bado ni mapema kueleza situation ilivyo. Ila baadhi ya watu niliokutana nao asubuhi hii ni kama wanategeana.
Hawaelewi kama watapiga kura au hawatapiga.

Kwa ujumla siku ya leo;

1. Serikali imeshinda, vyombo vya usalama, Dola vimeshinda kwenye hii vita.
Inaweza kuonekana ni jambo rahisi lakini wamejitahidi pakubwa.
Ubao unasoma 2-0 dakika bado ni zamapema.

2. Waandamanaji sio tuu wapo nyuma kwa bao moja lakini pia kimchezo wamezidiwa. Uwanja umeinama.
Hawachezi kama timu. Timu yao imevurugwa na kuvunjwa vunjwa.

3. Kuna uwezekano leo asipigwe hata mtu mmoja. Yaani kusiwe na fujo ya aina yoyotem yaani hata rungu moja hutosikia.

4. Wapiga kura watakuwa wachache sana. Kwa hali Ilivyo.
Ingawaje hii haiwathiri upande wa serikali. Wao lengo lao siku ya leo ipite salama. Pili watakaojitokeza hata kama ni elfu moja haohao watatumika kueleza kwa kulikuwa na uchaguzi.

5. Baada ya siku ya leo nini kitatokea?
a) Waandamanaji watakuwa wamekatishwa tamaa na watakuwa wamepata aibu kubwa ambayo sijui kama itaisha hivi karibuni.

b) Waliokuwa vinara mtandaoni watakasakwa wiki za mwanzoni za mwezi November kisha serikali itaachana na mambo ya uchaguzi kwani hang over na tension ya uchaguzi itakuwa imeisha.
So ni vizuri kama ulikuwa mstari wa mbele kuhamasisha maandamano wiki hizi mbili ujitahidi sana kujificha. Ukifanikiwa basi utakuwa umeokoka.

c) Matusi mitandaoni yatarudi tena kutukana sasa waandamanaji kwa kuwa waoga na kunguru. Kenya watatukana Sana watanzania.

d) Maridhiano ya kitaifa kufanyika na wale waliokamatwa kwa sababu za kisiasa na kiuchaguzi kuachiliwa.

e) Kusafisha baadhi ya taasisi za dini na kuunda sheria mpya zitakazobana taasisi za dini kujihusisha na siasa.

f) Influencers wa mitandaoni kubanwa zaidi na kuwekewa sheria za kitaaluma, na kimaudhui na kikodi.
Kwamba bila kiwango fulani cha taaluma kuna mambo haupaswi kuyajadili mitandaoni kama muanzisha maudhui na influencer.
Ila ku-post mambo personal kama picha zako utapewa uhuru.

g) Bado vuguvugu la waliotekwa, kuuawa na kupotezwa litaendelea kusakama huku kelele za wanaharakati mmojammoja wakiwa wanajitahidi kukumbushia.

h) serikali muda huo itafanya jitihada kuwasahaulisha watu habari hizo na mambo ya kukamatana kamatana baada ya mwezi mmoja kuelekea 2026 yatapotea. Jambo ambalo litafanya wale wanaharakati wanaokumbushia utekaji n mauaji kuchokwa na watu kama sio kupuuzwa.

I) mwaka 2026 utakuwa mwaka wa kitofauti sana.

J) Lisu atakuwa ameachiwa lakini atakuwa amekata tamaa. Sio kwa sababu ya kunyoroshwa na Serikali bali kutokana na Wale anaowapigania kumnyorosha, kumsaliti na kumtelekeza.

Poleni wote. Hayo ndio maisha.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Uwezo wako wa kupambanua mambo ni mdogo sana ungeniuliza mimi nikuonyeshe nini ni nini ...uliyo andika ni kinyume chake uwezi kushinda vita bila ya kumuua adui au adui kujisalimisha ...kete za kumdondosha samia zipo sawa sawa kabisa zinavyo kwenda ...ulicho andika umekikosea kwa asilimia 99% huu uchaguzi unakwenda kumbatilisha samia na ccm ...niliwaambia kuwa 2025 hakuna uchaguzi hata ccm na upinzani wangetaka ndivyo ilivyo na ndivyo itakavyo kuwa kuhusu maandamano hiyo alina shaka yatakuja tu tena ya jinsi yake ...
 
Hellow, Tanzania mpaka sasa tunaweza kusema tumefeli katika issue ya maandamno ee mungu tupe mwanga na matumaini ili tuweze kuishi katika mateso, karaha na kutekwa na serikali CCM hii imeisha tumeanzisha vita ambayo ilikuwa bado kwa Tanzania, bado watanzania tuna maisha ya raha sana mpaka tutekwe wote, ndipo tutatoka.
 
Na vile alivyoacha udaku iliyokuwa inamuingizia pesa sijui atakuwa kwenye Hali gani hawa ndio keyboard warrior
Kwa jana tu alikua na wasiwasi kuwa hizi nyumbu hazitatoka akawa anaongea huku anataka kulia sasa leo kashuhudia kweli Nyumbu hazijatoka nafikiri sahivi kaangusha bonge la kilio huko alipo
 
Nyie ndio mnateseka.

Kipindi hiki wanaoteseka ni wale waliokamatwa.
Sio serikali.
Sio wewe uliyejificha nyumbani kwako,
Sio wachambuzi
Sio waandishi wa habari
Sio yeyote

Waliokamatwa leo ndio wanapata maumivu makali kwa kuonyeshwa wale waliokuwa wanawapigania. Maumivu ya kutekelezwa na kusalitiwa unayajua?
 
Tanzania ni moja ya nchi zenye mifumo imara sana msifananishe na state/Nchi ambazo zilishaanguka kama za west hata Kenya uonevu wanaoupata kutoka kwa Al shabab ni wazi wana Jeshi legelege sana. Tanzania siyo ya kuchezea hali ni shwari sana nimetoka kwangu naelekea magomeni gari naendesha kama dereva wa Formula one (max verstapen au Lando Noris kibati speed 200km/h oya tufanyeni kazi tutafute pesa tuache fikra za kijinga I thought before you’re coward dogs barking on the keyboards of cellphones.

MIMI NAJITOA CHADEMA


HAKUNA NYWI NYWI WALA NYWI NYWIIII
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom