Kuna kipindi flani zamani kidogo about 18 yrs back,wezi walikuja usiku kwangu wakafanikiwa kufungua mlango wa gari,ikavutwa mpaka karibu na geti wakakomba kila walichoweza,niliposhtuka ndio wanamalizia na wakakimbia.Nilipanic sana nika mjulisha jamaa yangu mmoja hivi akaniambia tuonane jioni,kuna mtaalamu kuna vitu anafanya utawajua walioiba.Tulipokuwa kwa huyo mtaalamu tukiwa kwenye chumba alinipa maji flani nikanywa,akaniambia niangalie kwenye ukuta ambao ni mweupe nisigeuke kulia wala kushoto,ilinichukua kama saa nzima nikaanza kuona kwenye ule ukuta watu jinsi wanavyokuja na gari kutokea mjini mpaka wakafika nyumbani,walikuja na Hiace yao,wakapakia vile walivyoiba na kuondoka,mtu ambaye nilimuona na kumfahamu alikuwa ni rafiki yangu ambaye tulikuwa karibu sana na tunafanya naye ofisi moja,pia mdada mwengine ambaye pia tulikuwa naye ofisi moja.Sikutaka kuamini kabisa kuwa ndio wao waliohusika,kwahiyo nikaondoka pale bila kuamini kuwa nilichokiona ndio kilikuwa uhalisia,Ila baada ya kutoka pale nilisumbuliwa sana na kizunguzungu kilichokaa kwa takribani masaa 6 then nikarudi normal.Nimeandika hii story ninajaribu kuona kuwa inawezekana nilichopewa ikawa ni hiyo Magic mashroom bila ya kujua,kwakua ilikuwa ni kama ninaye angalia movie flani hivi....