Je, Magufuli amemfunika Nyerere kwa waombolezaji kwa sababu ya mtandao au ni kweli?

Mimi hata muda huu huu kufa niko poa tu, nitakufa na kafuraha fulani.
Hujui usemalo japo ni haki yako kusema utakacho kwa vile hujui . laiti ungejua ukasema yenye maana badala ya kukosa maanana kusema yaso maana.
 
Aidha, mawasilano yameboreka zaidi kuanzia usafiri kukufikisha mahali; na usambaaji wa habari. Mtu unaona kinachoendelea unaamua nawe ushiriki.
 
Waziri Mkuu alisema alivunja hadi rekodi ya Wacko Jacko 😂😂😂
 
Huyo ni baba wa taifa Julius Nyerere .Mtu kama Huyu akifa unachanganyikiwa ata kutembea huwezi
Kama tukijikita kwenye wingi wa watu ni wazi Magufuli alisindikizwa na watu wengi, huo ndio ukweli sio kwamba tunamvunjia heshima baba wa taifa.
 
Kama tukijikita kwenye wingi wa watu ni wazi Magufuli alisindikizwa na watu wengi, huo ndio ukweli sio kwamba tunamvunjia heshima baba wa taifa.
Unajua kufanya hesabu za "cross multiplication"?

Maana hapa kuna hatari ya watu kusema 4/8 ni kubwa kuliko 1/2 kwa sababu wanaona 4 na 8 ni kubwa kuliko 1 na 2.

Unaweza kufanya hesabu za watu walioshiriki msiba wa Nyerere na wa Magufuli kama ratio ya idadi ya watu wa nchi nzima kwa wakati husika?

Maana unaweza kulinganisha msiba wa Nyerere na Magufuli bila kuangalia ukweli kwamba mwaka 1999 nchi ilikuwa na watu milioni takriban 33 sasa hivi nchi ina watu zaidi ya milioni 61.

When comparing, compare likes.
 
Kwani si tulifundishwa kuwa Nyerere alikuwa hapendwi na Mabeberu lakin alipotaka kupinduliwa na Wanajeshi majeshi ya Mabeberu yakiongozwa na Uingereza yalikuja kusambaratisha lile Jaribio

Unajua kuwa Mabeberu yalimtumia Nyerere kuidhibiti Znz isijiunge na Siasa za kikomunist?
 
Sijasoma maelezo yako yote, but nasikitika kusema sitarajii wingi wa watu waweza kumsaidia marehemu chochote, kama moto wa jehanamu unamuhusu hawezi epuka
 
Ukimuuliza atakuambia amechukua/ siyo kusoma degree ya hesabu???? Na anatafuta kazi hajapata bado....
 
Wengi benders fuata upepo mkuu. Hawajui historia wala hawatafuti marina vitabuni. Hilo nano beberu hata huyo marehemu sina malika kama alikuwa anaelewa mana yake
 
Kabla ya kulinganisha. Zingatia
Msiba wa Rais aliyeko madarakani Vs Msiba wa Rais aliyestaafu tena zaidi ya miaka 14 imepita ni tofauti sana.
Teknolojia,msiba wa mwaka 1999 na msiba wa mwaka 2021 lazima iwe tofauti maana mwaka 1999 picha zenyewe tu mpaka mpiga picha apige goti na anakupiga picha moja 1,mwaka 2021 picha unapiga upendavyo. Teknilojia ya habari imekua sana mwaka 1999 TV,Smart phones,computers ilikuwa shida sio kama leo.
Hivyo ulinganifu huu hauwezi kuwa sawia.
 
Hakuna mtu wa kumfananisha na Nyerere ,msiba wa NYERERE ulikuwa na uzito wake kama angefariki kipindi hiki nathani tungeshuhudia umati mkubwa sana
 
Walikuja kumsaidia January 1964, na yale hayakuwa mapinduzi bali maasi zama za Tanganyika Rifle, Google "Tanganyika Army Mutiny". Na kumbuka wakati ule Nyerere alikuwa bado hajakosona na Mabeberu ndo maana Mkoloni Mwingereza alikuja kuzima maasi yale! Lakini yote kwa yote, hoja ni kwamba "...huyo JPM alichukia vp na mabeberu wakati utawala wake bado ulikuwa unanufaika na mabeberu?" Bila kujali kwamba Nyerere alisaidiwa kuzima maasi (sio mapinduzi) lakini miaka michache baadae akaja kuwa mwiba kwa mabeberu, tena alikuwa mwiba kwa vitendo na sio kwa maneno kama ilivyokuwa kwa JPM!!!
 
Vitendo vip?

Vile vya kuwapeleka Uingereza Kina Kapten Maganga kujifunza Kuendesha na kutumia Vifaru vya kivita kuja kumtoa Iddy Amin Dada 1979?

Uwe Adui wa Mabeberu lakin muda wote Secretary wako binafsi ni Mzungu toka Ubeberuni Uingereza?

Uwe Mwiba wa Mabeberu lakin mfumo wako wote wa Ulinzi unapata mafunzo toka Israel?

Mwiba wa Mabeberu check up zako za Afya miaka yote unafanya Uingereza hata mwisho wako umefika ukiwa St Thomas Uingereza?

Kama Elimu yako ni ya Text books za 'Tanu yajenga Nchi' huwezi kufikiri nje ya wigo uliowekewa
 
Pili msiba wa Nyerere haukufanyiwa siasa. Tofauti na hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…