Je, Magufuli amemfunika Nyerere kwa waombolezaji kwa sababu ya mtandao au ni kweli?

Huwezi kufanya comparison ya viongozi ambao wamefariki katika vipindi tofauti na mzazingira tofauti! Tofauti ya miongo miwili siyo ndogo.

Nyerere alifariki akiwa ameshatoka madarakani kwa muda mrefu. Zaidi ya miaka 15.. kwa hiyo kuna watu wengi tu walikuwa wamezaliwa hata hawajui kama nyerere alikuwa raisi,walikuwa wanasikia tu.Lakini Magufuli amefariki akiwa madarakani. Tofautisha mazishi ya raisi na mustafu. Huwezi kufanya mlinganisho wa namna hiyo.

Halikadhalika,population ya wakati huo ilikuwa ndogo ukilinganisha na sasa.

Miundombinu ya mawasiliano ilikuwa duni. Hakuna barabara za lami na magari ya kutosha. Hakuna tv. Ilikuwepo ITV peke yake. Hakuna mitandao ya simu. Hakuna internet. Kwa hiyo upashanaji habari ulikuwa mgumu.

Kwa sababu hizo na nyingine nyingi, huwezi kufanya ulinganisho wa vitu ambavyo premise hazifanani! Hivyo Magufuli kupata waombolezaji wengi siyo kielelezo cha kwamba alipendwa kuliko Nyerere. Kumbuka hata Ruge na Mengi walipata waombolezaji wengi kuliko Nyerere. Je walipendwa kumzidi Nyerere! Hapana.
 
Kumbukumbu zako ni nzuri kabisa. Nyerere alipendwa acha kabisa. Hata waliomchukia hawakufikia kiwango cha kufanya sherehe.
 
Uko sahihi kabisa!
 
Kwa hiyo amefufuka?
 
Nyerere hakuzungushwa mikoa kadhaa.Watu walilia machozi hayakuonwa na Instagram et al.
 
Nyerere akasome babaa, Magu ni kipenzi cha watu.
Acha mizaha yako.

Naamini Nyerere ameongoza wewe hujazaliwa,hivyo hakuna unachojua!

Nyerere was a great leader. Siyo Tanzania tu,bali Afrika na Dunia kwa ujumla.Legacy ya Nyerere ni ya kipekee. Kuna maeneo sehemu mbalimbali duniani yamepewa jina lake mpaka Uingereza kwa mama Elizabeth.
 
Mitandao,

Ongezeko la watu,

Kutembezwa vituo vingi

Mwisho Nyerere alikufa baada ya miaka 15 hivyo alishaanza kusahaulika.
 
[emoji106][emoji106][emoji106][emoji106]
 
Halafu vingine vinavyoonyeshwa amejenga ni vile vilivyojengwa awamu ya mtangulizi wake yeye akaenda kuzindua mf. Daraja la Kigamboni,JNIA TERMINAL III, Hospital ya Mloganzila,nk
 
watangazaji wa TBC waligoma kiaina mara nauguliwa mara niko safari nk

Jk nyerere weee thubutu mpaka leo wastani wa watu 100 kila siku wanaenda mwitongo kuhiji.
 

Hayo ni maono yako wala sikupingi


Magufuli βœ”
Babu ❌
 
Na kuongezea nyama, mwili wa Nyerere uliagwa Dsm pekee, haukuzungushwa mikoani kama mbio za Mwenge. ..
 
Wangempelekea na mikoa kama singida, mbeya, arusha, songwe afu mngeleta hizo siasa zenu

Katika mikoa ambayo haikutegemewa kwa Marehemu kujizolea kura nyingi moja wapo kanda ya ZIWA/MWANZA. Nani alitegemea hayo??? Huko Arusha hatuhitaji kura zao, tunawajua kitambo tu, wengi wao wabinafsi na lichama lao.
 
Na kuongezea nyama, mwili wa Nyerere uliagwa Dsm pekee, haukuzungushwa mikoani kama mbio za Mwenge. ..
Ile habari ya kuizungusha maiti mikoani kama a circus show ni jambo la aibu sana.
 
Mkuu punguza ukali wa maneno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…