Je, mahakama kukataa kuwa summon Rais Samia, VP Mstaafu Philip Mpango na PM Mstaafu Kassimu Majaliwa inaathiri "Fair trial" ya kesi ya Lissu?

The Palm Beach

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
4,249
Reaction score
11,592
By Advocate Paul Boniventure;

Jibu la moja kwa moja ni NDIYO inaweza, lakini kwa upande mmoja pia ni HAPANA kwa sbb ni discretion ya kawaida ya kisheria ya mahakama kuchukua uamuzi huo kwa kuzingatia relevance ya shahidi na ushahidi. Nitaeleza...

Yes, uamuzi huu ni mgumu na mzito sana kwa sababu Mahakama imeweka wazi mipaka ya defence katika hatua hii, lakini pia haijafunga kabisa mlango wa mashahidi wa defence

Kwenye hoja ya mashahidi 11, Mahakama imekubaliana na prosecution kwamba kutowataja wakati wa committal proceedings hakuwezi kurekebishwa kwa kuwataja baadaye wakati wa PH.

Hapa Mahakama inaweka mkazo kwenye procedural compliance, yaani haki ya defence ipo, lakini inatumika ndani ya utaratibu uliowekwa na CPA.

Lakini sehemu ya muhimu zaidi ni kwamba Mahakama haikatai summons zote.

Imetumia discretion yake chini ya kifungu cha 314 na imeona IGP, CDF na DCI wana relevance ya kutosha kuja kutoa ushahidi.

Hii ni muhimu sana kwa sababu inaonyesha Mahakama haikatai ushahidi wa viongozi wa vyombo vya dola kwa sababu ni upande wa Serikali, lakini inapima relevance ya kila shahidi mmoja mmoja.

Kuna pia clarification muhimu sana kuhusu burden of proof.

Mahakama inasisitiza kwamba katika kesi ya jinai, Jamhuri ndio yenye burden ya kuthibitisha guilt, na sio defence kuthibitisha innocence.

Lakini kutowaita Rais au viongozi wengine hakupunguzi wajibu wa prosecution kuthibitisha ingredients za kosa linalomkabili Lissu.

Kwa upande wa defence, ruling hii inaweza kuonekana kama setback kwenye mashahidi fulani, lakini sio mwisho wa safari.

IGP, CDF na DCI bado wanaweza kuleta ushahidi wa moja kwa moja unaogusa masuala ya usalama, operation ya Serikali au allegations ambazo prosecution inazihusisha na kosa.

Na hapa tukumbuke uzito wao utategemea watakachothibitisha, na sio vyeo vyao.

Na jambo la mwisho na muhimu la kuondoka nalo leo ni kwamba, Mahakama imeonyesha kwamba relevance ndio gatekeeper.

Hivyo defence sasa inaendelea na mashahidi ambao Mahakama yenyewe imeona wanaweza kuwa na evidentiary value.

Kesho itakuwa muhimu kuona ushahidi wa Heche unaendelea kuelekea wapi, hasa baada ya ruling hii kubadilisha mazingira ya ushahidi wa defence.

Naweza kusema mahakama imepunguza idadi ya mashahidi, lakini haijapunguza burden ya Jamhuri. Na imeacha dirisha la ushahidi wa vyombo vya dola likiwa wazi.

===========​
Baada ya maelezo haya, wadau wengi wameuliza maswali kadhaa. Baadhi ya maswali hayo na majibu yake

Q. Nimekufatilia kwenye analysis zako kwa sikuzote. Kwanza niseme ahsante kwa kazi Yako nzuri ya ufafanuzi. Nina swali la Msingi hapa; Hakimu wa Mahakama ya Kisutu alikataa kuwaandika wale Watu ambao mshitakiwa aliwataja kama mashahidi wake. Hapa Haki ya mshitakiwa iko wapi?

================​
JIBU LA WAKILI:
Swali lako linaingia moja kwa moja kwenye kiini cha fair trial.

Naweza kukujibu kwamba sio kwamba haki ya mshtakiwa imeondoka kwa sababu Hakimu hakuwataja mashahidi,

Bali ni kwamba kuna tofauti kati ya haki ya kuwa na defence na utaratibu wa kuitumia haki hiyo.

Kwa mujibu wa uamuzi uliosomwa, Mahakama Kuu imeona kwamba tatizo lilikuwa la procedural.

Yaani mashahidi hao hawakuonekana kwenye orodha ya committal proceedings, na Mahakama ikaona kutajwa kwao baadaye wakati wa PH hakukurekebisha dosari hiyo.

Lakini muhimu sana, Mahakama haijasema Lissu hana haki ya kuleta ushahidi wa defence.

Ndio maana imetumia discretion yake na kuruhusu IGP, CDF na DCI kuitwa kwa sababu imeona ushahidi wao una relevance.

Na unapo uliza haki ya mshtakiwa iko wapi.

Naweza kukujibu iko kwenye kuhakikisha kwamba ana nafasi ya kuwasilisha defence yake kwa haki na kwa usawa, lakini hiyo haki inatekelezwa ndani ya procedural rules..

Katiba yenyewe inalinda fair hearing, na kanuni hiyo inahusisha pia uwezo wa mshtakiwa kuandaa na kuwasilisha defence yake.

==============​

Q2. Sasa hapa nani mwenye kosa kati ya TAL na hakimu wa kule commital? Maana TAL aliwataja na hakimu Kiswaga akakataa kuwaandika

MAJIBU YA WAKILI:

Hapa kisheria kuna jambo muhimu sana. Tukichukua kama fact kwamba TAL aliwataja mashahidi wakati wa committal proceedings.

Lakini Hakimu akakataa kuwaingiza kwenye record, basi suala haliishii kwenye kusema majina hayapo kwenye record.

Kifungu 281 cha Criminal Procedure Act kinatambua haki ya summons kwa mashahidi ambao majina na anuani zao zimetolewa na accused kwa committing magistrate.

Pia kifungu 295 kinaweka wazi kwamba accused anaweza kupewa summons kwa shahidi ambaye ushahidi wake ni material to the case.

Kwa hiyo hapa kama TAL alitimiza wajibu wake wa kuwataja, lakini omission ikafanywa na Mahakama ya committal,

Kuna tofauti kubwa kati ya failure by the accused to name a witness na failure by the court to record a witness who was named. Haya ni makosa mawili tofauti kabisa kisheria.

Na hapa ndipo fairness inapoingia, yaani haiwezi kuwa mantiki kwamba mshtakiwa anasema, nilimtaja shahidi, Mahakama ya chini inasema, sitamuandika,

Halafu kwenye hatua inayofuata mshtakiwa anaambiwa, huwezi kumuita kwa sababu hakukuwa kwenye record.

Hapo procedural rule inaweza kugeuka kutoka kuwa chombo cha kusimamia utaratibu na kuwa chanzo cha prejudice dhidi ya defence.

Lakini pia fahamu kuna nuance, kwamba kutajwa kwa shahidi hakumaanishi Mahakama inalazimika kumuita bila kuangalia relevance.

Kifungu 295 kinaipa Mahakama mamlaka ya kutoa summons pale inapojiridhisha kwamba ushahidi wa huyo shahidi ni material to the case.

Kwa hiyo Mahakama inaweza kuchuja ushahidi usio na relevance, ila haiwezi. kwa mtazamo wangu, kutumia omission ambayo haikusababishwa na accused kama sababu pekee ya kumfunga mikono.

Na hapa ndipo tofauti ya IGP, CDF na DCI kuwa wameruhusiwa inakuwa muhimu.

Inaonyesha kwamba Mahakama haioni sheria kama mlango uliofungwa kabisa, lakini bado inatumia discretion yake.

Kwa kifupi naweza kusema, kama ushahidi wa committal proceedings unaonyesha TAL aliwataja na Hakimu akakataa kuwaandika, basi mzigo wa dosari hiyo haupaswi moja kwa moja kubebwa na TAL.

Hapo ndipo appellate court inaweza kujiuliza kama procedural compliance imepewa uzito mkubwa kuliko substantive right to a fair opportunity to present the defence.

Hiyo ndio hoja nzito ya kisheria naweza kusema hapa.
 
Ni ujinga kutaka raisi makamu na waziri mkuu kwenye kesi ya kiongozi wa chama cha siasa kati vyama zaidi ya 10 apewe huo umuhimu usio hata kuwa na uhalali wa kisheria kuwaita mahakamani ni zaidi ya ndoto za alinacha

Ni mfano kama Trump aitwe kwenye kesi ya uhaini ya Edward Snowdon alietuhumiwa kwa uhaini
hawa wote walikutwa na uhaini US na wengine kunyongwa, na hakuna Eaisi wa US alieitwa mahakamani#
Acheni upumbavu na utoto

 
Ungeweka kifungu cha sheria kinachokataza Raisi kuitwa mahakamani kama shahidi ungetusaidia sana sisi maamuma.
 
Ila Tz bado tunaishi kwenye lindi la giza sana. Imagine ingekuwa Kenya. Sisi tunawachukulia viongozi kama mamungu fulani hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…