Je, Mama yake Gigy Money ndio chanzo cha tabia alizonazo mtoto wake?

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Msanii Gigy money ameendelea kumtupia lawama mama yake huku akisema inawezekana maisha magumu anayo yapitia sasa ni kutokana na malezi mabovu aliyo lelewa na mama yake.

Pia Gigy amesema, mama yake alimzaa Kwa bahati mbaya Kwa sababu mimba yake aliitoa na kwenda kumtupa chooni ila Kwa bahati nzuri watu walipata habari wakaenda kumtoa chooni akiwa bado ana pumua.

Gigy ameendelea kusema kuwa, hizo habari zote alipewa na bibi yake na akaongeza Kwa kusema, mama yake na Gigy alipalalaiz baada ya kutoa mimba hiyo.

Mbali na hivyo pia, Gigy amesema ameanza kufukuzwa nyumbani akiwa na miaka 12 tu huku mama yake akimsingizia kuwa anatoka na bwana wake (baba wa kambo).
 
Kama kweli bibi yake Gigy ndiye alimsimulia mjukuu wake hivyo,basi ni mchonganishi sana au uzee ulimsahaulisha kumezea mambo.
Bibi amesema mimba ilitolewa, hvy hapa ishu sio kujifungua bali n kutoa mimba.

Yn mm nachoshangaa n mimba kutolewa then mtoto awe Hai afu ndo huyu gigy, maana ake mtoto alikuwa hai kabisa hvy mimba ilikuwa na miezi 8 au 9🙌

Kvp mtu aweze kutoa mimba ikiwa na umri huo?

Huyo bibi kama vile ametupiga
 
Sawa vingine anavyofanya huyu bint ni vya common sense tuu, Kuna lugha anaongea za hovyo zisizo na mantiki kabisa
Ni matokeo ya malezi,makuzi,mazingira,aliemlea,alivyomlea.
Mengine anafanya Kwa utimamau wake ila mengine ni out of her control.yuko traumatized na makuzi aliyopitia.
Mtu unapitia magumu kiasi kwamba una uwezo wa kufanya lolote ukiwa na attitude ya "Sina Cha kupoteza"
Huna baba tangu uzaliwe mambo ya aibu kuyafanya umuonee nani aibu?
Mamako mcharuko kwanini nawe usiwe mcharuko?
Huna Cha kupoteza
 
Bibi amesema mimba ilitolewa, hvy hapa ishu sio kujifungua bali n kutoa mimba.

Yn mm nachoshangaa n mimba kutolewa then mtoto awe Hai afu ndo huyu gigy, maana ake mtoto alikuwa hai kabisa hvy mimba ilikuwa na miezi 8 au 9🙌

Kvp mtu aweze kutoa mimba ikiwa na umri huo?

Huyo bibi kama vile ametupiga
Msimuliaji hakuwa anamalizia na kukamilisha sentensi zake sababu ya uvutaji wa goso.Yawezekana alitaka kueleza kwamba,bibi yake alimwambia mama yake alijaribu kuitoa mimba na kushindwa.Na,alipomzaa alimtupa chooni kumpoteza.Bahati yake wasamaria wema walimuokoa kama siyo kumuopoa.
 
Msanii Gigy money ameendelea kumtupia lawama mama yake huku akisema inawezekana maisha magumu anayo yapitia sasa ni kutokana na malezi mabovu aliyo lelewa na mama yake.

Pia Gigy amesema, mama yake alimzaa Kwa bahati mbaya Kwa sababu mimba yake aliitoa na kwenda kumtupa chooni ila Kwa bahati nzuri watu walipata habari wakaenda kumtoa chooni akiwa bado ana pumua.

Gigy ameendelea kusema kuwa, hizo habari zote alipewa na bibi yake na akaongeza Kwa kusema, mama yake na Gigy alipalalaiz baada ya kutoa mimba hiyo.

Mbali na hivyo pia, Gigy amesema ameanza kufukuzwa nyumbani akiwa na miaka 12 tu huku mama yake akimsingizia kuwa anatoka na bwana wake (baba wa kambo).
Gigy money sio kichaa ana deep layers za trauma ambazo hata namna ya kuzijua inakuwa ngumu sana

Mtu ana miaka mingi mno, kuanza ku unwound trauma inakuwa changamoto nyingine plus tayari anamajukumu ya kulea pia.

Ndo maana unakuta kila mda kadata, kwa sababu hawezi tena ku address pain
 
N kweli ila mtoto anaweza kurekebisha palipokosewa kwa 100%

Tuachane na mama, gigy nae n mwehu tuu
Anaweza.ndio kama hivyo kaamua kuolewa atulie.kaamua kuzaa

Maisha na misukosuko pia mahangaiko ndio yanachangia kutushape ukubwani.Lakini tukituliza akili na kujua hapa nakosea sio sahihi,ukiamua kubadilisha binafsi inawezekana.Lakini sio rahisi Kwa Kila mtu.
 
Msimuliaji hakuwa anamalizia na kukamilisha sentensi zake sababu ya uvutaji wa goso.Yawezekana alitaka kueleza kwamba,bibi yake alimwambia mama yake alijaribu kuitoa mimba na kushindwa.Na,alipomzaa alimtupa chooni kumpoteza.Bahati yake wasamaria wema walimuokoa kama siyo kumuopoa.
Gigy yeye amesema nn kutoka mdomoni mwake.?

Kwamba bibi alimwambia mama alitoa mimba au mama alijifungua then akatupa mtoto?
 
Back
Top Bottom