Je, Mapambano ya Wanaharakati na Diamond yana faida kwa nchi?

Je, Mapambano ya Wanaharakati na Diamond yana faida kwa nchi?

Ukiwasikiliza wanaharakati unaweza kudhani kuwa muda wowote ule huko mtaani watu wataanza kuchinjana.

Diamond ni mtafutaji wa riziki kupitia muziki, anayo haki ya kuipamba CCM kama wanamlipa pesa nzuri.

Sasa kama kuna unyama umefanyika wenye kuihusu CCM Diamond kama mwanamuziki hata asingeimba nyimbo za siasa bado angekuwa hana ubavu wa kuufanya unyama huo usifanywe popote ulipofanyika.

Hao watu 15,000 ni wachache sana kulinganisha na mamilioni ya watu waliosimama barabarani kumuaga JPM na wengine wakatandika kanga zao ili matairi yazikanyage.

Diamond anaweza kushinda hiyo tuzo na akaendelea kuimba nyimbo za CCM na bado hizi harakati za wanaharakati zisiathiri muziki wake.

Nongwa za kipuuzi kama hizi za activists ni sawa sawa na zile za miaka ya 1980 mwanzoni wakati Nico Njohole alipotakiwa kufanya majaribio Arsenal halafu viongozi wa FAT wakamuwekea mizengwe.

Nongwa kama hizi zilimnyima Mwameja nafasi ya kucheza timu ya ligi daraja la kwanza Uingereza.
Uaikumbuka ile kura kura ya kumtafuta kiongozi bora wa afrika na wabongo wakaungaana kumpigia rais wa Ghana ili mwendazake asishinde,kuanzia hapo tafuta kwa nini inakuwa hivyo,kuna chuki dhidi ya raia na kama ndio kwa nini?
 
Hoja ya hao wanaharakati ni kwamba Diamond hakusimama upande wa haki pindi uongozi wa awamu ya tano ukitekeleza uovu kwa watanzania na badala yake diamond alitumia title/platform alonayo kuwasafisha na kuwapigia debe hao wanaoitwa madhalimu wa utawala wa awamu ya tano

Sasa kabla ya kuja heading yako ilikua kwanz uhoji ni faida zipi walizopata watanzania wakati diamond amesimama upande dhalimu
Hao wadhalimu ndio walitumia nguvu na akili zao katika kuijenga Tanzania. Haiwezekani asilimia pana ya walichokifanya kikawa ni udhalimu tu.

Mwanamuziki ni mtu mdogo sana kuweza kuuweka hadharani huo udhalimu halafu akaendelea kuwa na urafiki na uongozi wa juu wa watuhumiwa wa udhalimu.
 
Katika hili nimefurahi kuwaona mashabiki wenzangu wa Diamond wa tangu enzi na enzi, nimemuona data Evelyn Salt Phoenix

Hili jambo si personal, labda kama kuna watu wanalitumia pesonally, Mtu ambaye ni celebrity siku zote hatakiwi kuside na oppressors akawaacha wananchi, hii iwe funzo kwao wote wasanii wetu, wautumie umaarufu wao vizuri kwa ajili ya jamii pia maana na wao ni wana jamii.

Movements kama hizi zisiishie kwa Diamond tu, ziende kwa wasanii wote wanaoside na oppressors na wana habari pia.

nakukumbuka vyema shabiki nguli.
 
Uaikumbuka ile kura kura ya kumtafuta kiongozi bora wa afrika na wabongo wakaungaana kumpigia rais wa Ghana ili mwendazake asishinde,kuanzia hapo tafuta kwa nini inakuwa hivyo,kuna chuki dhidi ya raia na kama ndio kwa nini?
Hao waliompigia kura rais wa Ghana ni wachache walio sehemu ya kundi la wanafiki, hao siku zote wapo.

Tunazo roho mbaya siku zote.
 
Yule ni mfanyabiashara kaenda pale kufanya burudani baada ya kulipwa sio kufanya siasa ungeelewa Hili lisingekusumbua na kuna wengine wameenda pale kufuata burudani sio hotuba za wanasiasa ndio maana baada ya diamond kutumbuiza wanasepa shida ni nyinyi mnaoteseka
Kama ni mfanya biashara kwa nini aliona na aliunga mkono maandano na harakati za wanaigeria kupinga uonevu wa polisi #End SARS,lakini binaadamu huyuhuyu anawaambia raia wa nchi yake wakae kimya kwa yanayoendelea nchini mwake hilo ndio swali watu wanajiuliza na kumuona kuwa ulikuwa na ufahamu wa kutosha bali alijitia upofu,hakuona hata wasanii wenzake yaliyo wapata kwa nini hakupaza sauti pamoja nao ila akashauri tukae kimya?


 
Kwa mliokuwa hamjui, ogopa sana mtu/watu wenye uwezo wa kuandika. Ukiandikwa majambo yako yote kwa namna inavyostahili, utapata au kukosa ukitakacho chote. Mwambie Diamond Platnumz apoe, akae, aombe radhi kwa umma na ajirekebishe. Akitunisha mabega anaweza kuishia hapa kwa sababu biashara yake inategemea sana public relations.
Hajui hili..

Fedha imeshamlevya. Ufahamu umeshatekwa na fedha. Macho yake yanaangalia fedha tu. Kila akipata fursa anabwabwaja kwa dharau dhidi ya hao hao wanaomfanya apate hizo fedha...

Kosa analofanya Diamond Platimuz ni kukifungamanisha kipaji cha sanaa yake ya muziki na siasa hususani siasa za CCM moja kwa moja....

This is a grave mistake...

Hii maana yake ni moja tu, kuwa, ufikapo mwisho wa CCM ndiyo utakuwa mwisho Wa sanaa yake pia na ndiyo utakuwa mwisho wa kila alichonacho...!!

Diamond Platinumz ajifunze kwa akina Ole Sabaya, Paul Makonda na wengine wa aina hiyo ambao starehe zao, jeuri yao, kula yao, akili na ufahamu wao umliomtegemea mtu. Sasa mtu kafa nao wanakufa taratibu na ndiyo mwisho Wa mambo yao yote...!!

Kama ambavyo wengi walikuwa hawaamini kuwa John P. Magufuli atafikia mwisho wake haraka sana, ndivyo ambavyo watu hawaamini kuwa CCM inasambaratika sana and it's very soon hilo litakuwa wazi kwa kila mtu...

Sanaa ya muziki haipaswi kufungamanishwa na siasa. Kina Diamond Platimuz na wanamuziki wengine kama wanataka kuishi ktk nyakati zote, waanze kuacha taratibu kuifungamanisha sanaa na vipaji vyao vya muziki kwenye siasa za moja kwa moja...
 
Umeandika upuuzi mwingi kwa faida ya aliekutuma. Kukosa kwako elimu isiwe sababu ya ww kuja kuanika ujinga wako hapa jukwaani, ukiendelea kuendekeza njaa kuna siku hao waliokutuma watakuomba to.bo la taka.. Shauri yako
Bado unaishi dunia ya masaria? tayari upepo ulishabadirika kama hujui muulize sabaya atakupa ubuyu.
 
Diamond si wizkid na wizkid si diamond system ya mziki wa nigeria huwezi kufananisha na bongo na siasa ya nigeria huwezi kufananisha na hapa bongo pesa nyingi za wanamuziki wa bongo wanapata kwenye hii mikutano ya kisiasa mfano mzuri diamond kalipwa show moja tu ya CCM million 100 fanya calculation kama alifanya mikoa 10 alipata shilling ngapi? Wewe lini umewahi kununua kazi za wasanii zaidi ya kuburn kazi zao.Ukiacha na hivyo Diamond amewekeza hapa bongo hiv akiamua kuiponda serikali hali yake ya biashara itakuaje?utamsaidia kulisha familia yake? Wizkid anaweza kufanya harakati za kisiasa dhidi ya serikali lakini nchi yao hawana mambo kama bongo ya kuharibiana au kurudishwa nyuma ndio maana huyo wizkid anajeuri hiyo.
the kind
The Palm Tree
unadhani chanzo kikubwa cha fedha za Diamond ni show? hujui hiyo ni mara moja tu kila baada ya miaka mitano,kwa hiyo tuelewe kuwa yeye anathamini pesa hata kama sote tutaisha! kama jibu ni ndio basi hafai hata kwa kulumangia.
 
Acheni uchawi wenu wa msata nyie watu..Vuta picha wewe ndio Diamond na nature ya utawala uliopita ulivyokuwa ungediliki kukataa kuwa upande wao? Hali ya nchi yetu inajulikana unataka apewe makesi ya kuhujumu uchumi? Kampeni yenu hii ni rubbish
Mbona wa kina Ney bado wapo?
 
Kufatilia siasa za Tanzania ni ujinga, full stop.
Huu ni wito kwa Tuzo za BET zinazoendeshwa na kutayarishwa na Black Entertainment Television (BET) kumzuia Diamond Platnumz kushiriki tuzo.

View attachment 1810525


Movement #ChangeTanzania started this petition to bet awards and 3 others

Hadi jana 6/6/2021 saa 11;45 jioni watu 11,938 kati ya kura 15,000 zinazohitajika


11,938 have signed.
Let’s get to 15,000!
bofya link hii chini maandishi mekundu kuona uungaji mkono wa hili pingamizi unavyo endelea

Sign the Petition

Diamond Platnumz ni msanii mashuhuri duniani wa muziki wa Tanzania ambaye alitumia umaarufu wake na kipaji chake kufunika uchafu na harufu ya ukandamizaji wa kinyama wa dikteta wa mwisho John Magufuli na utawala wake. Diamond pia ni rafiki wa karibu na mshirika wa kibiashara wa Paul Makonda mkuu wa mkoa wa zamani wa Dar -es-Salaam, ambaye ametesa waziwazi na kuwadhulumu watu wa LGBTI. Mnamo mwaka 2020 Makonda alitajwa na Idara ya Mambo ya Nje ya Marekani kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kukandamiza uhuru wa kujieleza na kushirikiana.

Muktadha:

Tanzania ilikumbwa na ukandamizaji wa kikatili na kurudisha nyuma demokrasia tangu 2016 wakati (marehemu) Rais Magufuli alipoingia madarakani. Utawala wake ulipunguza uhuru wa kidemokrasia, haki za kimsingi za kibinadamu na watanzania walishuhudia ukatili ambao hawakuwahi kuushuhudia huko nyuma kama kutoweka kwa kutekwa, miili iliyofungwa na kutupwa ufukoni mwa bahari ya Hindi, kuwekwa kizuizini kinyume cha sheria kwa wanasiasa wa upinzani, wakosoaji na wafanyabiashara, kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari , vitisho kwa wabunifu na wasanii wakiwemo wanamuziki, waigizaji na wachekeshaji. Tukio la kushangaza sana ni kumshambulia kinyama kwa mbunge wa upinzani Tundu Lissu mchana kweupe. Lissu alinusurika na risasi 16 mwilini mwake kusimulia hadithi yake. Hivi sasa anaishi uhamishoni Brussels, Ubelgiji.

Mwaka 2020, Magufuli aligombea tena uchaguzi chini ya chama chake Chama cha Mapinduzi (CCM). Bwana Lissu alihatarisha maisha yake na akarudi kushindana na Magufuli chini ya tiketi ya chama chake - CHADEMA. Uchaguzi huo uligubikwa na kasoro, vurugu ikiwa ni pamoja na mauaji ya raia wasio na hatia na vikosi vinavyofanya kazi kwa niaba ya serikali. Baada ya uchaguzi huo, Magufuli na wapambe wake waliwakamata viongozi wa chama cha upinzani na kuwatishia mashtaka ya uhaini. Baadhi ya viongozi wa upinzani walishuhudia wanafamilia wakiuawa. Leo viongozi kadhaa wa upinzani wanaishi uhamishoni, wakati mamia bado wanateseka gerezani kwa mashtaka ya uwongo.

Magufuli pia alikuwa mkanushaji mkali wa COVID19 ambaye kukataa kwake kurudia kufuata miongozo inayokubalika kimataifa juu ya kinga na matibabu ya COVID19 ilisababisha vifo vingi ambavyo bado havina hati hadi sasa kwa sababu ya kukataa kwa serikali kuchapisha takwimu zozote zinazohusiana na COVID19 tangu Mei 2020.

Uhusika wa Diamond Platnumz:
Mnamo 2016, Diamond alimfanya Paul Makonda kuwa Mlezi wa lebo yake ya muziki na kampuni ya media inayoitwa Wasafi. Makonda alitumia Tamasha la Wasafi kutangaza na kusafisha picha yake. Pia katika kipindi chote cha ongezeko la ukandamizaji wakati wasanii wenzake walipofungwa na kutekwa nyara Diamond alikaa kimya. Mnamo 2017, kwa makusudi alitoa wimbo moja aliouita "Acha Nikae Kimya"
kama jibu kwa umma uliokuwa una paza sauti na kulaani ukandamizaji. Diamond hadi leo hajalaani au kusema juu ya unyama wowote uliofanywa.

Diamond Platnumz ni mwanachama wa chama cha CCM anayejiamini na alikuwa mwanamuziki anayeongoza katika kampeni ya CCM mnamo 2015 na 2020. Mnamo mwaka wa 2020 licha ya kilio kikubwa ndani na kimataifa dhidi ya Magufuli na utawala wake, Diamond alimpitisha dikteta huyu katili, akamtolea wimbo ("Magufuli Baba Lao") na mara kadhaa alishiriki naye kwenye jukwaa wakati wa kampeni. Mnamo Oktoba 2020 wakati wa maandamano ya #EndSARS huko Nigeria, Diamond alituma ujumbe wa mshikamano na Nigeria lakini kwa makusudi alichagua kukaa kimya juu ya ukatili unaotokea Tanzania wakati wa uchaguzi.

Baada ya uteuzi wa Tuzo za BET 2021 , Diamond alienda mbele ya vyombo vya habari na kuzungumza kwa dharau juu ya wanaharakati, kisha akatembelea makao makuu ya chama chake CCM ambapo uteuzi wake ulisifiwa kama mafanikio ya chama na taifa.

Kwa nini Diamond anapaswa kutostahiki:

  • Diamond Platnumz alishindwa kuonyesha kuguswa wala kutoa hadharani mshikamano wowote na wasanii wenzake kama Roma Mkatoliki, Nay wa Mitego na Idris Sultan ambao waliteswa na dikteta Magufuli.
  • Diamond Platnumz alichagua kulinda na kupanua masilahi yake binafsi ya kibiashara kwa kusifu na kutumia nguvu yake ya umaarufu kulainisha sura ya dikteta katili na washirika wake.
Tuzo za BET zimekuwa zikiheshimka na Waafrika wengi kwa utambuzi wake wa talanta za wasanii wa mfano. Tuzo hii ya kimataifa ambayo ilianzishwa mnamo 2018 imekuwa ikienda kwa wasanii ambao wamekuwa waangalifu sana na walisimama kwa haki kwa maisha ya Waafrika. Wote Davido (2018) na Burna Boy (2019 na 2020) wamekuwa mstari wa mbele kwenye maandamano ya #EndSARS wakitumia nguvu zao za nyota na umaarufu kutoa mwanga juu ya dhuluma na hata kulinda raia kutoka kwa ukatili wa polisi. Diamond Platnumz ni mpenda fursa mwenye ubinafsi, mchoyo na ni mwombaji radhi wa serikali kandamizi ambaye alichagua kwa makusudi kufumbia macho ukatili na kushirikiana, kusifu na kushirikiana na wanaokiuka haki za binadamu kama Paul Makonda na John Magufuli.

Tunaamini kwamba mara tu BET itakapothibitisha ukweli huu, itakuwa wazi kuwa Diamond Platnumz HAKustahili kutambuliwa yoyote katika


FOR ENGLISH AUDIENCE


BET - Disqualify Diamond Platnumz from BET AWARDS 2021 (for Best International Act)

Movement #ChangeTanzania started this petition to bet awards and 3 others

This is a call to BET Awards hosted and produced by Black Entertainment Television (BET) to disqualify Diamond Platnumz

Diamond Platnumz is a world-renowned Tanzania music artist who used his popularity and his talent to whitewash and deodorize the brutal repression of the late dictator John Magufuli and his regime. Diamond is also a close friend and business ally of Paul Makonda the former Governor of Dar -es-Salaam who has openly persecuted and cracked down on LGBTI people. Makonda has also been designated in 2020 by the US State Department for gross violations of human rights including cracking down on freedom of expression and association.

Context:
Tanzania has suffered brutal repression and roll back of democracy since 2016 when (late) President Magufuli ascended into power. His regime curtailed democratic freedoms, basic human rights and Tanzanians witnessed never-before experienced atrocities like enforced disappearances, bodies bound and gagged washing ashore the Indian ocean, mass illegal detention of opposition politicians, critics and businessmen, crackdown on independent media, intimidation of creative people including musicians, actors and comedians. A particularly shocking event has been the brutal gunning down of opposition legislator Tundu Lissu in broad daylight. Lissu survived with 16 bullets in his body to tell his story. He is currently living in exile in Brussels, Belgium.
In 2020, Magufuli ran for re-election under his party Chama cha Mapinduzi (CCM) . Mr Lissu risked his life and returned to run against Magufuli under his party’s ticket – CHADEMA. The election was marred with irregularities, violence including killing of innocent civilians by forces acting for or on behalf of the regime. In the immediate aftermath of the election, Magufuli and his henchmen arrested the leaders of the opposition party and threatened them with treason charges. Some opposition leaders saw family members killed. Today several opposition leaders live in exile, while hundreds still languish in jail on trumped up charges.
Magufuli was also a rabid COVID19 denier whose repeated refusal to follow internationally accepted guidelines on prevention and treatment of COVID19 resulted in many deaths that remain undocumented to date due to the refusal of the government to publish any figures related to COVID19 since May 2020.

Diamond Platnumz’s role:
In 2016, Diamond made Paul Makonda the Patron of his music label and media company called Wasafi. Makonda has used the Wasafi Festival for publicity and to sanitize his image. Also throughout the increased level of repression when fellow artists were imprisoned and abducted Diamond remained silent. In 2017, he deliberately released a single called “Acha Nikae Kimya” (Let me remain quiet) as a response to the increasing demand from the public to speak up and condemn the crackdowns. Diamond to-date has not condemned or spoken up on any of the atrocities committed.

Diamond Platnumz is a self-avowed CCM party member and was the lead musician for the CCM campaign in 2015 and 2020. In 2020 despite a huge outcry locally and internationally against Magufuli and his regime, Diamond endorsed this brutal dictator, dedicated a song to him (“Magufuli Baba Lao”) and several times took to stage with him during campaign. In October 2020 during the #EndSARS protest in Nigeria, Diamond tweeted solidarity with Nigeria but deliberately chose to remain quiet on the atrocities happening in Tanzania during the elections.
After the BET Awards 2021 nomination for best international act, Diamond took to the media and spoke disparagingly of activists, then paid a visit to his party’s headquarters CCM whereby his nomination was hailed as some sort of achievement for the party and the nation.

Why Diamond should be disqualified:
Diamond Platnumz has failed to show basic concern and publicly express any solidarity with his fellow artists like Roma Mkatoliki, Nay wa Mitego and Idris Sultan who suffered at the hand of the dictator Magufuli.
Diamond Platnumz chose to protect and expand his personal and business interest by praising and using his star power to soften the image of a brutal dictator and his collaborators.
BET awards have been always held in high esteem by many Africans for its recognition of talent of exemplary artists. The international act which was established in 2018 has consistently gone to artists who have been very conscientious and stood up for justice for African lives. Both Davido (2018) and Burna Boy (2019 and 2020) have been in the frontline at the #EndSARS protests using their star power and fame to shed light on injustice and even protect civilians from police brutality. Diamond Platnumz is a selfish, greedy opportunist and an apologist of a repressive regime who chose to deliberately turn a blind eye to atrocities and associate, praise and collaborate with renowned human rights violators like Paul Makonda and John Magufuli.

We believe that once BET independently verifies these facts, it will be clear that Diamond Platnumz does NOT deserve ANY recognition in these prestigious awards.
 
Under normal circumstances DOMO Asingeweza kutoa kauli yoyote kupinga uonevu kwenye ile awamu hata kama ungekuwa wewe asilani usingejaribu yani…as we speak angekua kesha potezwa vbaya sana..avune alichopanda ila hakua na namna
AJITOKEZE awaombe radhi wabongo
Hao waliompigia kura rais wa Ghana ni wachache walio sehemu ya kundi la wanafiki, hao siku zote wapo.

Tunazo roho mbaya siku zote.
Sio roho mbaya hata wao nao walikuwa wanamuona hana roho nzuri,ndio maana wakataka kumzuia asipate hiyo heshima haikuwa inamstahili,na ndivyo ilivyo kwa Diamond wanaona hastahili hiyo hishima kutokana na ushahidi walio utoa.
 
Back
Top Bottom