Je, matatizo ya Mwanamke ni fursa kwa baadhi ya Wanaume?

Kuna binti mmoja kaingia mjini Dar juzi kati kwenye interview na kampuni flani, ila ndani ya masaa 72 ameshamkubalia MD, HR na wadau wengine... wawili wameshamla. Hii ni hatari kwa afya, wadada na nyie ni tatizo, msichana ana umbo zuri na muonekano mzuri, ana kiingereza kizuri ila sasa......
Duh noma ataliwa na kutupwa akija mrembo mpya
 
Kumsaidia mtu kwa moyo mmoja, kunahitaji upeo mkubwa wa kiakili na kisaikolojia , unao wasema ni ile aina ya wanaume ambao hawajakomaa kihisia.
Ni kweli
Wanaelelewa kuwa wakati mtu yupo kwenye matatizo , uwezo wake wa kufanya maamuzi sahihi huwa ni mdogo sana.

Kwahiyo issue hapo ni kukosekana kwa ubinadamu tu.
Na kweli mtu akiwa na changamoto ni nadra kuamua sawa sawa
 
Ndio maisha ya viumbe vyote katika kila nyanja ya maisha, kimsingi tatizo/hitaji la kiumbe kimoja ni fursa kwa kingine ndio ecosystem inabalance!

Kwa mfano watu wasingeugua, wahudumiaji wangekulaje, wasigeharibikiwa na nyenzo zao mbalimbali mafundi wangepataje? Kila anayetatua tatizo/hitaji anapata return, yani ni mwendo wa nipe nikupe, usingetaka chumba hata huyo mzee usingemjua, na yeye asingehitaji pesa wala asingekujua nknk
 
Kuna jirani yangu alikosa pesa ya chumvi sh 500 tu nikampatia nayeye akanipatia just imagine chumvi tuu mtu anavua nguo nilivomaliza nikamwambia wewe ni zero brain
Sio wewe na yeye ni ma zero brain tupu?
 
Ndio maisha ya viumbe vyote katika kila nyanja ya maisha, kimsingi tatizo/hitaji la kiumbe kimoja ni fursa kwa kingine ndio ecosystem inabalance!

Kwa mfano watu wasingeugua, wahudumiaji wangekulaje, wasigeharibikiwa na nyenzo zao mbalimbali mafundi wangepataje? Kila anayetatua tatizo/hitaji anapata return, yani ni mwendo wa nipe nikupe, usingetaka chumba hata huyo mzee usingemjua, na yeye asingehitaji pesa wala usingemjua nknk
Nipe nikupe nimejikuta nacheka 😅
Utawapa wa ngapi sasa🙌
 
Ndivyo ilivyo. Kuna wengine wanasema moja kwa moja na kuna wengine wanavizia kiwiziwizi.
 
Hey guys,

Kuna jambo nimekuwa nikijiuliza kuhusu utafutaji wa kazi na fursa mbalimbali kati ya mwanaume na mwanamke.

Mara nyingi naona kuna tofauti kubwa sana.

Mwanaume anaweza kwenda kutafuta kazi au kujifunza kitu fulani, na majibu anayopata huwa ni mawili tu: kazi ipo au haipo.

Mambo yanakuwa ya moja kwa moja.

Changamoto kubwa naiona kwa baadhi ya wanawake, hasa wanapokutana na HR au manager ambaye ni mwanaume.

Badala ya mazungumzo kubaki kwenye kazi au fursa husika, mara nyingine mtu huanza kutengeneza mazingira ya mazoea, stori za karibu, na hatimaye kutongoza.

Niseme wazi, si ofisi zote ziko hivyo, si sehemu zote unaweza kukutana na hali hii, na si wanaume wote wana tabia hiyo(msisitizo).

Lakini ni jambo ambalo linaonekana kujirudia mara kwa mara kiasi cha kuibua maswali.

Najaribu kujiuliza, hawa wanaume wa aina hii huwa wana shida gani?🤔

Kwa nini umtengenezee ugumu mtu anayehitaji kazi au fursa mpaka ahisi kuna masharti ya ziada?
Kwa nini msaada au uwajibikaji uwe na matarajio ya malipo ya kimapenzi?😞

Mfano, mimi binafsi nilikuwa nimepanga nyumba kwa mmiliki ambaye ni mwanaume, ana familia na ni mtu ana ndoa.

Siku moja niliona mambo yangu hayajakaa sawa kifedha, hivyo nikampigia simu kabla hata muda wa kodi haujaisha nikamwambia.

"
Shikamoo mzee, najua tarehe ya kodi imekaribia lakini naona mambo yangu hayaja tik vizuri ikifika ukaona kimya naomba unipe muda kidogo kwa sababu hali yangu bado haijakaa sawa.

Akanijibu kwa upole sana na kuniambia watu wa aina yangu ni waaminifu na makini.

Nikasema sawa, labda ni mtu mwenye uelewa.
Lakini ilipofika muda wa kodi na kuona bado sijalipa, akanipigia simu tena na kusema.

Binti, nimekaa nikafikiria nikakuonea huruma.
Naweza nikakuacha ukae hapo hata miezi sita bila kulipa, au nikakupa sehemu nyingine kwa sababu nina nyumba nyingi🤔

Nikadhani labda ananisaidia kwa ubinadamu.
Kumbe baada ya hapo akaanza kusema jinsi anavyonipenda na maneno mengine mengi ya kimapenzi ( longo longo nyigi in Sugu voice).

Nikajiuliza, inawezekanaje mtu aanze kunipenda mara tu baada ya kujua nina shida? Noma sana.

Nilielewa haraka anachotaka, nikamwambia asijali nitatafuta namna ya kulipa, na kweli nililipa kama nilivyoahidi.

Sasa huwa najiuliza, tatizo huwa ni nini kwa baadhi ya wanaume kutaka kutumia matatizo ya wanawake kama fursa ya kupata mahusiano ya kimapenzi? Kwa nini wakiona mwanamke yuko kwenye hali ngumu, badala ya kusaidia kwa ubinadamu, wao huona huo kama mwanya wa kutimiza matamanio yao?

Au ni matumizi mabaya ya mamlaka na nafasi walizonazo?
Wewe unaonaje? Umewahi kushuhudia au kukutana na hali kama hii? 🤔💭

ShesRise_1 🖐
Umepewa bure
Toa bure
 
Nipe nikupe nimejikuta nacheka 😅
Utawapa wa ngapi sasa🙌

Haimaniishi umpe uchi, namaanisha generally kila kiumbe kinatoa kitu kupata kitu, huwezi kwenda kwa mama ntilie kula kama huna pesa, huwezi kwenda kwa mwalimu km huhitaji kufundishwa na kadhalika ni mwendo wa nipe nyanya nikupe kitunguu ndio nature inabalance...
 
Nje ya mada.

Mwanaume ukishakuwa na hela, wanawake woote wanakuona Kwa jicho la fursa pekee hivyo ngoma ni bila bila tu.
 
Haimaniishi umpe uchi, namaanisha generally kila kiumbe kinatoa kitu kupata kitu, huwezi kwenda kwa mama ntilie kula kama huna pesa, huwezi kwenda kwa mwalimu km huhitaji kufundishwa na kadhalika ni mwendo wa nipe nyanya nikupe kitunguu ndio nature inabalance...
Oooh sawa nimejibu hivyo maana tunaongelea rushwa ya ngono

Upo sahihi
 
Back
Top Bottom