Je, Mbowe kufutiwa kesi kabla ya mkutano wa wadau wa demokrasia na vyama vya siasa?

Ndio hapo sasa, ushahidi wa kuunga unga ule hautokani mkono mrefu au macho mengi ya serikali, ni wa kupika ofisini.
Huyo anayesema mkono mrefu ni upi huo? Mkono mrefu wa Kingai, Mahita, Jumanne, Goodluck kusafiri kutoka kituo chao cha kazi Arusha, kwenda kukamata watu Moshi, Tabora na Mwanza, huku polisi wa maeneo hayo hawahusishwi?

Cc mwananyaso
 
Rais Samia angepata credit kubwa sana kama angefuta hiyo kesi kabla ya kujadiliwa E.U.

Lakini ata akiifuta sasa itaonekana tu ni shinikizo la kimataifa.

Lazima aifute kesi ili dunia ya wawekezaji na demokrasia impokee,na sasa tunaihitaji dunia zaidi kuliko muda wote.

Mwisho wa yote mshindi atakuwa ni Mbowe maana kapewa political mileage kubwa sana na sasa hatoshikika tena.
 
Ukweli unaujua Chadema ni maarufu na muhimu kukiko hizo takataka zingine.
Mbowe sio meza wala viti vya kikao hicho, kusema Chdema ni maarufu na vingine ni takataka ni lazima ujue kikao hicho kimeandaliwa chini ya uongozi wa Zitto ambaye ni mwanachama nje ya hiyo Chadema.
 
Acha kushabikia watu kunyanyaswa kwa tuhuma za kijinga .Kila Mtanzania ana haki bila kijali yupo chama gani ,kuwa na moyo wa kibinadamu ,Mbowe kuwa mahabusu hakutakufanya wewe uwe tajili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jeshi haliendani na kasi ya mama na limejikita katika mambo ya kisiasa kinyume na katiba.Ni kulifumua loote.
Wao CCM pamoja na huyo mama, wanapenda jeshi la polisi linalojihusisha na siasa kwa sababu linawalinda wao dhidi ya vyama vingine vya siasa. Vyama vingine vya siasa vikitaka kufanya siasa, jeshi la polisi linatoa mkong'oto, hapo CCM wanapumua vizuri. Atalifumuaje jeshi kama hilo?
 
Apo ndio mama anashauriwa vibaya na akina Kingai.
 
CHADEMA hawatakubali kushiriki uozo huo kwa kuwa ni chama makini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…