Je, Mtoto aliyezaliwa nje ya Ndoa anafaa kuitwa Jina la ubini la Baba yake?


Nafikiri ingependeza zaidi ungeweka na source/reference
Ndio najaribu kujikumbusha SURAT AN-NISAAI hapa
 
Kuzaa hovyo kunapoteza uwezo wa mzazi kutoa huduma, hii ndo sababu yenye maana ya katazo la usizae nje ya ndoa, nyingine zote ni ubatili.
Iyo ni moja ya sababu lkn pia kuendeleza ukoo,malezi,tabia,dini

Ivi unajisikiaje wewe ungekua unaambuwa umezaliwa nje ya ndoa?

Unadhani panya road wanatokea wapi wale?
 
Amezaliwa na ndoa au mama na baba? Na ninani anae staili kutoa ubini?.
 
Hii hoja ni kama uchafu wa jalalani..yaani mtoto wangu alafu watu waliokaa wakatunga sheria zao gandamizi na za ovyo niwasikilize..Yaani ukojoleee ndani halafu uje useme ni mtoto wa nje.

Mungu amesema endeni mkazaliane na sio kuoana.
Tatizo ninaliona Kwa baadhi yetu ni kwamba hatumuamini Mungu na tunaona hizi Dini zimetungwa na watu ambao wamejiamulia mambo Yao.

Kwa mtazamo huu bado kuna kazi kubwa ya kumjua Mungu na sishangai kuona watu wanachukulia mambo kirahisirahisi Tu.

Tunahitaji kumjua Mungu kwanza
 
leo damu yako mzee usisingizie dini
Mimi binafsi ni mhanga wa hili Jambo lakini namlea mwanangu vizuri Sana,ingawa sikupenda kabisa mwanangu WA kiume asichukue Jina la ubini wangu lkn sina namna kwakuwa namuamini Allah huyo mtoto ataitwa Kwa jina la ubini WA mama yake.

Kwangu Mimi neno la Mwenyezi Mungu lipo juu ya kila kitu.

Kwahiyo kama Baba natoa huduma zote stahiki.
 
Mkuu nje ya sheria ya Mungu ni wako hapo naomba tuelewane Kwanza

Lakini

Ikifuatwa sheria ya Mungu huyo mtoto hatambuliki kama ni wako na ndio maana kuna baadhi ya haki hastahili kuzipata

Huo ndio ukweli na utabakia kuwa hivyo daima dawamu
 
Ukimuoa huyo mwanamke uliyezaa naye kabla ya ndoa ina maana ni ruksa mwanao kutumia jina la ubini wako?
 
Kwann pia awe wa mama? Acha undezi,huyo mtoto anakosa gani? Hakuamua kujileta mwenyewe duniani bali ni hao wazazi wake so hastaili adhabu yoyote.Kama hizo dini zinatuelekeza hivyo basi haina maana ya kuwa na hiyo dini maana ni unyanyasaji
Hapa Kwa mtazamo wako unaona kuna adhabu gani Kwa huyo mtoto mkuu.

Kama malezi na kumpa huduma zote ni ruhsa, kama wasia unaweza kumuandikia ingawa hautakiwi kuzidi thelusi moja na nusu kama sijakosea.

Hapa lengo ni kuacha kuzaa ovyoo Kama wanyama na Bila utaratibu,mwanadamu amepewa hadhi kubwa na Mungu anastahili kuwa kwenye maadili mema
 
Ukimuoa huyo mwanamke uliyezaa naye kabla ya ndoa ina maana ni ruksa mwanao kutumia jina la ubini wako?
Sijui ulimaanisha nikimuoa baada ya kuzaa nae?

Kwa mfano huyu wangu natarajia kumuoa lakini kwakuwa mtoto alipatikana kabla ya ndoa Jina la ubini litakuwa la mama yake hakuna kitacho badilika
 
Mahitaji ya mtoto hayana uhusiano na uzinzi wetu. Nimeshazini nimezaa huyo mtoto ni halali yangu na atapata haki zote hata kama dini haitaki. Viongozi wa dini wanaruhusiwa kununa. Sitelekezi mtoto, ni vile haijanitokea tu nikazaa nje ya ndoa.
 
Sijui ulimaanisha nikimuoa baada ya kuzaa nae?

Kwa mfano huyu wangu natarajia kumuoa lakini kwakuwa mtoto alipatikana kabla ya ndoa Jina la ubini litakuwa la mama yake hakuna kitacho badilika
Kwa hiyo bado ndoa kwa huyo uliyezaa naye haitoi suluhu ?...huko ni kumuadhibu mtoto.
 
Iyo ni moja ya sababu lkn pia kuendeleza ukoo,malezi,tabia,dini

Ivi unajisikiaje wewe ungekua unaambuwa umezaliwa nje ya ndoa?

Unadhani panya road wanatokea wapi wale?
Nje ya ndoa hakuzuii mtoto kufundishwa na kukua akiwa na maadili iwapo Baba yake atamkubali mtoto na kupigana kufa kuhakisha anapata haki ya malezi.
 
Kwa mujibu wa Sheria ya mtoto ya 2009,moja kati ya haki za mtoto ni jina la ubini.Kwa Sheria za Tanzania hakuna mtoto haramu,kwa hiyo mtoto wa nje ya ndoa anastahiki sawa na mtoto wa ndani ya ndoa.
Mkuu hayo ni mambo ya sheria za jamhuri

Sheria za Dini ambazo ndio muhimu kuliko zote na ndio ambazo utakuja kuhojiwa siku ya hukumu zinasema hivyo
 
Kwa hiyo bado ndoa kwa huyo uliyezaa naye haitoi suluhu ?...huko ni kumuadhibu mtoto.
Mtoto haadhibiwi hata kidogo Ila ndio Hali halisi ilivyo

Kwenye hukumu za Mungu hakuna longo longo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…