Je, Mtoto aliyezaliwa nje ya Ndoa anafaa kuitwa Jina la ubini la Baba yake?

Mkuu umeleta hoja ya msingi Sana lakini mambo mengine ni ya kimungu zaidi.

Kwa mfano huko zamani waislamu walikuwa wamepewa ruhusa ya kuwaoa wanawake ambao walipewa Kitabu,hapa inamaanisha umma ambazo zilishushiwa sheria na Mungu Kwa mfano wakristo na wengineo Bila kuwasilimisha au kuwabadili Dini kwasababu walikuwa enzi hizo wanamwamini Mungu Mmoja tofauti na wakristo WA siku hizi.

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba Mwenyezi Mungu anahekima zake ambazo Kwa akili ya binadamu haiwezi kutambua
 
Ndo maana wengine wanakuwa wapagani. mungu gani katili hivi anaadhibu watoto ambao hawakuomba wazaliwe na wazinzi?
Mkuu Mungu sio katili Ila hayo ndio matokeo ya kwenda kinyume na sheria zake.

Lau tungekuwa watiifu na kufuata muongozo wake haya yote yasingetokea

Na kwakila Jambo Lina fundisho ndani yake, ambao hawajafanya huo upuuzi watajifunza kutoka Kwa walikosea
 
Reactions: Tsh
Umesema sahihi,ninavyojua Mimi ni ndoa ya kikristo ndio inatambulika endapo mke na mume WA Imani Yao watabadili Dini na kuwa waislamu hawatalazimika kuoana tena
 
Kwahiyo kujaaliwa na Mwenyezi Mungu ndio upo sahihi?

Unazungumziaje majambazi na wauza unga mbona wanafanikiwa sana je wamejaaliwa na Mungu au wanapendwa na Mungu?
 
Sawa, ila ikinitokea mm itabidi anielewe tu maana siwezi telekeza damu yangu. Mm huwa naamini mtt ni zawadi kutoka kwa MUNGU. Sasa akiruhusu nikaipata hiyo zawadi katikati ya makosa yangu ya uzinifu ajue tu atabeba jina langu, urithi nitamwandikia na nitamuunganisha na dada na kaka zake wa ndani ya ndoa.
 
Sasa mtoto anakuaje hana baba aisee. Na vipi mtoto akipatikana kabla ya ndoa na mkaoana mkiwa na huyo mtoto bado atakua hana baba??
Nikupe mfano mmoja ISA mwana WA Mariam hakuwa na Baba na ndio maana ameitwa Kwa jina la mama yake

Akipatikana kabla ya ndoa hukumu itabakia pale pale hata Kama utakuja kumuoa mama yake,maadam Tu alizaliwa nje ya ndoa hiyo ndoa ya baadae hailalishi makosa ya awali
 
Hahaha najua si unamvimbia Mungu usijali we Vimba Tu IPO siku paap huyu hapa ndo utakujua hujui
 
Unajua nini,kuna amri kumi za Mungu lakini binadamu wa kisasa hakuna hata moja katimiza afu huyo huyo anakuja kuleta fafanuz nyingiii....mi huwa naangalia tu na kujisemea ...Hiiiii
😁😁😁 Kpnz changu naona unapagawa Tu, ndio mambo ya dunia hayo
 
Hahaha najua si unamvimbia Mungu usijali we Vimba Tu IPO siku paap huyu hapa ndo utakujua hujui
MimI sifanyi maamuzi sababu naogopa. Najua sina nafasi mbele ya MUNGU ila still itabidi anielewe tu. Yatakuwa ni mazungumzo kati ya MUNGU na aliyemuumba kwa mfano wake kuhusu baraka ya uzao aliompa.
 
Hizi dini za kizushi ndio chanzo cha migogoro, umasikini, ujinga, ugaidi na ubaguzi.

Uislam ni ujinga, ukristo ndio hovyo kabisa.

Mungu wa kwel hayupo kwenye dini.

Uislam ni tawi la ukristo wa warumi wa kale, haya yote ni magenge ya wahuni wa kizungu yanayofanya kazi kuwagawa waafrika na mijinga ya kule nchi za uarabuni isiyopenda kufikili zaidi ya kuwaza udini.

Uislam haukuanzishwa na ishamail, maana ishmail hakuwa muarabu wala hakuwa mzungu, kama ibrahimu akilkuwa mzungu na akazaa na binti wa kimisri(waafrika weusi) mnazan kunawezekana kutokea mwarabu hapo? Zaid ya Afrocast ama chotara asili ya uzungu(israel).

Biblia na quran zimeleta uharibifu kwa fikra duniano, hivyo ni vitabu vinavyoongoza kwa ugaidi dunia nzima kwa kificho..
 
Maelezo yako nimeyapata lkn hakuna kauli ya itayochukua nafasi dhiki ya Allah na Mtume

Nimesahau ni Sura gani lkn IPO haya ndani ya Qur'an juu ya hili swala na hivyo Jambo halina hitilafu hata kidogo kwasababu ni kauli ya Allah
 
Nafikiri ingependeza zaidi ungeweka na source/reference
Ndio najaribu kujikumbusha SURAT AN-NISAAI hapa
Nimesahau hiyo Aya IPO katika Sura gani,lkn itapatikana Tu inshallah
 
Ila Dini sometimes inaleta UPUMBAVU Sana... yaani inakufanya unakuwa mjinga

Yaani mtoto wako mwenyewe,Damu yako, unakataa asichukue jina lako (Kwa kifupi Unamkataa), eti kwa sababu unamuamini Alah... Huu ni Upumbavu wa dini.

Huyu Alah wenu kwenye Hili Alichemka vibaya sana.
 
Ndoa ndio inakupa uhalali wa kumiliki zao linalopatikana .
Kwa mfano unaweza kwenda kujenga nyumba kwenye kiwanja ambayo ina hati ya jina la mtu mwingine ?
 
kwani wakati mnakatikiana hamkujua kama atapatikana mtoto? maaneenerr huu uzi umekaa kibaguzi sana sikubaliani na mashala ya majina sijui ubini wala nini mtu akizaliwa kazaliwa full stop haya mambo ya kulazimishana sijui ukoo sijui kabila sijui ubini ni uwendawazimu tu. kwani hata akiamua kujiiya mti ama jiwe si ni binadamu tu? tutumie akili sio kila kitu cha kushobokea by the way haya madini tumeletewa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…