Je, Mtoto aliyezaliwa nje ya Ndoa anafaa kuitwa Jina la ubini la Baba yake?

Je, Mtoto aliyezaliwa nje ya Ndoa anafaa kuitwa Jina la ubini la Baba yake?

Ahsante Kwa kutoa darsa labda wataelewa kuwa walichomezeshwa ni upuuzi wa kibinadamu na sio maagizo ya MUNGU

Kama unahisi kwenye maandiko matakatifu Kuna mawazo yakibinadamu ndani yake basi hata hili la watoto wakando limechukuliwa kibinadamu maana naamini Mungu hakumuumba mtu na kumruhusu Aishi Ili aitwe majina ya laaana. Majina na Mambo mnayoyapigania mkiamini ni maagizo ya Mungu mjue waliongeza wanadamu wenye mwili wa nyama na sio mwenyezi Mungu muumba wa mbingu, nchi na vitu vyote vilivyomo.

hapo ndipo mnapokua wagumu kuelewa aliokwambia mtoto wa nje ya ndoa analana ni nani au unajitungia mtoto wa nje ya ndoa anaheshima kama wanavyo heshimiwa binaadam wengine laana ni kwa wazazi wake walio vunja amri ya Allah
fungua masikio uelewe vizuri haya nikuambiayo.
1- Mwana mume amewekewa sheria na Allah atakapotaka kumuingilia mwanamke lazima kwanza amuowe.
2- Mwanamke naye akitaka kuingiliwa lazima aolewe kwanza.
3-Dume la mnyama linapotaka kupanda jike hakuna sheria ya kuona.
4- jike la mnyama linapotaka kupandwa hakuna sheria ya kuona.

N:B
KWA SHERIA HIYO YA NDOA ndio anayo halalisha mtoto anae patikana hapo awe wa Baba na mama kwa Binaadamu.

NA KWA SHERIA YA KUTOKUWEPO ndoa kwa wanyama ndio inayo halalasha mtoto anaye patakana awe wa MAMA TU.

HUTOONA HATA SIKU MOJA JOGOO AKARUDI NA VIFARANGA NYUMBANI AU MWENYE JOGOO AKADAI NAYE NI MUHUSIKA WA VIFARANGA WA JIKE LA JIRANI YAKE KWA KUA JOGOO WAKE ALIMSHUGULIKIA KWELIKWELI JIKE LILE
WALA DUME LANG'OMBE KURUDI NA NDAMA NYUMBANI.

Hilo ndio linalotokea kwa Binaadamu watakapo chupa sheria yao ya NDOA wakafuta sheria ya wanyama KUTOKUWEPO NDOA. basi mtoto anakua wa mama kama ilivyo kwa JAMII YOTE YA WANYAMA NDEGE N.K

QURA'AN 6:38
Wanyama walio ardhini na ndege warukao kwa mbawa zao ni umma kama mlivyonyinyi(binaadam) hutakuacha kuelewesha chochote kile katika hiki kitabu kisha kwa Mola wenu mtarudishwa.
 
Ingalikua mtoto huyo ana mkono wake au ushirika wake kwenye kuzaliwa hii nadharia ingekua sahihi , yeye hajahusika na chochote hawez kuadhibiwa , unapo muadhibu mtu asie na kosa una tofaut gani na muuaji? Mwizi? Mzulumati? Tofaut yenu n nini?

Huyo mtoto anahusikaje na hiyo dhambi hadi aadhibiwe? Hakuna mtoto asie wa halali , hakuna mtoto mwenye haki kuliko mwingine , huwez sema huyo mtoto sio halali kisa hajazaliwa ndani ya ndoa , hiyo nadharia sio sahihi

lakini pia, kwenye maelezo yako unaonyesha ubinafsi ulio pindikia , kwamba wote ni watoto wa baba mmoja , ndugu yenu ambae kazaliwa nje ya ndoa akipewa mali anawadhulumu nyie?? Roho ya wapi hii? Na kama baba asipokua na mali na huyo ndugu yenu wa nje akaamua ibeba familia kwa kuwatunza na kuwapa mali mtachukua hamchukui?

Nashukuru Kwa maoni yako chief na Una haki ya kufanya hivyo.

Ila sheria itasimama mahala pake ili haya mambo yafikie kipindi yakome kabisa.

Shukrani Kwa kuchangia.
 
Uislam haumbagui mtoto alie zaliwa nje ya ndoa nyiyi ndio meelewa vibaya huyu mtoto kwanza hana dhambi yeyote kwa kuzaliwa nje ya ndoa pili huyo mtoto mamalaka juu yake yote yako umamani/ujombani kwake ndio wajibikaji wa kila shida ya huyo kijana kisheria. wewe ulompa mimba bint sio baba wewe ni Mzinifu. kwa hiyo mmekutana wazinifu wa wili nyie ndio haramu yule mtoto ni halali.na kama utamuhudumia kwa chochote kile utakua unatoa sadaka tu kama utoavyo sadaka kwa watoto au watu wengine.
Shukrani Kwa kutia neno mkuu maana naona watu hawataki kuelewa uhalisia WA mambo Ila wanasukumwa na hisia tu
 
hapo ndipo mnapokua wagumu kuelewa aliokwambia mtoto wa nje ya ndoa analana ni nani au unajitungia mtoto wa nje ya ndoa anaheshima kama wanavyo heshimiwa binaadam wengine laana ni kwa wazazi wake walio vunja amri ya Allah
fungua masikio uelewe vizuri haya nikuambiayo.
1- Mwana mume amewekewa sheria na Allah atakapotaka kumuingilia mwanamke lazima kwanza amuowe.
2- Mwanamke naye akitaka kuingiliwa lazima aolewe kwanza.
3-Dume la mnyama linapotaka kupanda jike hakuna sheria ya kuona.
4- jike la mnyama linapotaka kupandwa hakuna sheria ya kuona.

N:B
KWA SHERIA HIYO YA NDOA ndio anayo halalisha mtoto anae patikana hapo awe wa Baba na mama kwa Binaadamu.

NA KWA SHERIA YA KUTOKUWEPO ndoa kwa wanyama ndio inayo halalasha mtoto anaye patakana awe wa MAMA TU.

HUTOONA HATA SIKU MOJA JOGOO AKARUDI NA VIFARANGA NYUMBANI AU MWENYE JOGOO AKADAI NAYE NI MUHUSIKA WA VIFARANGA WA JIKE LA JIRANI YAKE KWA KUA JOGOO WAKE ALIMSHUGULIKIA KWELIKWELI JIKE LILE
WALA DUME LANG'OMBE KURUDI NA NDAMA NYUMBANI.

Hilo ndio linalotokea kwa Binaadamu watakapo chupa sheria yao ya NDOA wakafuta sheria ya wanyama KUTOKUWEPO NDOA. basi mtoto anakua wa mama kama ilivyo kwa JAMII YOTE YA WANYAMA NDEGE N.K

QURA'AN 6:38
Wanyama walio ardhini na ndege warukao kwa mbawa zao ni umma kama mlivyonyinyi(binaadam) hutakuacha kuelewesha chochote kile katika hiki kitabu kisha kwa Mola wenu mtarudishwa.
Mashallah chief

Asantumu Kwa kujazia maarifa hapa
 
Nashukuru Kwa maoni yako chief na Una haki ya kufanya hivyo.

Ila sheria itasimama mahala pake ili haya mambo yafikie kipindi yakome kabisa.

Shukrani Kwa kuchangia.
Sheria iliyojaa mapungufu top to bottom ni sheria?? Ni tamanadun na taratibu za kiarabu za hovyo

Mambo yakome?? yanakoma vipi wakat watendaj hawaathiriki na chochote hapo , au huyo mtoto n mtendaji?? Manake yeye ndie muathirika na sio wazazi
 
Kwa mujibu wa imani ya kiislamu mtoto ambaye amezaliwa nje ya ndoa hatambuliki Kwa mujibu wa Sheria kama mtoto wa Baba husika.

Kwasababu kizazi au uzao WA familia unatakiwa upatikane ndani ya ndoa ya kisheria au ndoa iliyofungwa Kwa misingi ya Dini,na nje ya hapo huyo ni mtoto wa zinaa ambaye kisheria anatambulika kama mtoto wa mama aliye mzaa Tu.

Ingawa kikawaida atafahamika kama mtoto wa Baba Fulani lkn kidini huyo Baba hatambuliki na hivyo kuna haki Fulani ambazo Baba hawezi kumfanyia mtoto wake.

Moja wapo ni huyo mtoto hafai kuitwa Jina la ubini WA Baba yake,Hilo Jambo ni haramu Sana na Mungu ameshalikemea tayari, ingawa Kwa bahati mbaya Sana Kwa kutojua wengi wamewapa majina ya ubini wao hao watoto wa nje ya ndoa.

Na lingine ni kumuozesha kwenye ndoa, Baba Hana haki ya kumuozesha binti yake WA nje ya ndoa Kwa mumewe kwani ndoa hiyo ni batili na haifai kabisa.

Lingine huyo mtoto hawezi kumrithi Baba yake kwasababu kisheria huyo mtoto sio WA huyo Baba,Bali Baba anaweza kumpa sehemu ya Mali huyo mtoto,lkn mara Tu huyo Baba anapokufa basi huyo mtoto Hana haki ya Kurithi chochote.

Lakini sio vibaya huyo Baba kumhudumia huyo kijana Kwa malezi na mahitaji mbali mbali maadam Tu yeye ndiye sababu ya kuja Hicho kiumbe hapa duniani.

Na mtoto ambaye Hana Baba kisheria anaweza kuitwa Kwa jina la mama yake, Kwa mfano ETUGRUL BEY ASHA au Kwa jina la ubini Kwa upande wa mama yake.

Kubwa ni kutambua uzao mzuri ambao hata kizazi chako kinaweza pata haki stahiki ni kizazi ambacho kinatokana na ndoa takatifu ambayo IPO Kwa mujibu wa Sheria.

Na hata wale ambao wanafunga ndoa za kiserikali basi watambue kidini Hicho kizazi Chao hakitambuliki na Sheria za Dini Kwa maana Baba Hana watoto hapo Ila watoto ni WA mama.

Ni hayo Tu!

Kazakh destroyer
Msonjo
Nurain
adriz
professional Driver
baby zu
Mnathibitisha vipi kama mtoto ni zao la ndoa? Nauliza hivi kwani hakuna uhakika (guarantee) kuwa kweli watoto wote ni wa mume na mke fulani. Na haki zao zikoje?
 
SHAHAWA za DICKSON/JUMA unataka ziitwe jina la mama? kweli WA ASIA wamewaroga ninyi kisa kanzu ambazo hata gest wanaenda nazo.
 
Mpaka leo naeleza waarabu hawana akili mnabisha.

Waarabu wameleta dini lakini wanaangalia penye asali.

Ukiwa nacho wewe ni mwarabu mwenzao ukiwa kapuku wewe ni ahaya zina kuusu
Sijakusoma Mkuu..

Kwamba matako yako ni mekundu?
 
Sheria iliyojaa mapungufu top to bottom ni sheria?? Ni tamanadun na taratibu za kiarabu za hovyo

Mambo yakome?? yanakoma vipi wakat watendaj hawaathiriki na chochote hapo , au huyo mtoto n mtendaji?? Manake yeye ndie muathirika na sio wazazi

Nilitamani huu mjadala na wewe ungeisha kwasababu huwa Nina kanuni moja ambayo ni kwamba

Ikifikia kipindi hatuelewani au hatufikii muafaka au tunapishana kimitazamo au kila mtu anasimamia misimamo yake basi ni Bora KUKUBALIANA KUTOKUKUBALIANA

Ila nitachangia jambo hili,unaposema kuwa watendaji hawaathiriki sio kweli,anayefuata sheria na kuamini juu ya sheria ya Allah huathirika Sana.

Kitendo cha mtoto wako WA zinaa kutompa Jina la ubini wako ni adhabu tosha kabisa,maana kutochukua ubini wako ni kama unamiliki gari halafu huna Kadi au kiwanja na huna Hati,maana ni kwamba Mda wowote chochote kinaweza kutokea

Kitendo cha wewe kutorithiana na huyo mtoto ni adhabu tosha kwako wewe Baba.

Kitendo cha kukosa haki ya kuozesha kama ni mtoto WA kike ni adhabu tosha maana itabidi umtafute sheikh amuozeshe Kwa niaba yako.

Sasa mtu mwenye akili timamu next time hawezi fanya upuuzi huo tena.

Nitakuwa tena sina la ziada kujadiliana na wewe,naogopa tusije kuvunjiana heshima.

Shukrani.
 
SHAHAWA za DICKSON/JUMA unataka ziitwe jina la mama? kweli WA ASIA wamewaroga ninyi kisa kanzu ambazo hata gest wanaenda nazo.
Huo ni mtazamo wako na maoni yako na Una haki ya kufanya hivyo

Ingawa

Upo mbali na uhalisia
 
Mnathibitisha vipi kama mtoto ni zao la ndoa? Nauliza hivi kwani hakuna uhakika (guarantee) kuwa kweli watoto wote ni wa mume na mke fulani. Na haki zao zikoje?

Hili unalo uliza limeshajibiwa katika komenti zilizo pita lkn nitajibu Kwa ufupi.

Iko hivi...

Ndoa ndio kidhibitisho chako wewe kuwa huyo mtoto ni wako kisheria, ndio inakupa umiliki halali WA hao watoto wako kwasababu mwenye shamba ndio mwenye mazao yake.

Hata kama akitokea jirani akalima shambani kwako bado mwenye mazao ni wewe, kwahiyo hata ikatokea ukazini na mke WA mtu na ukazaa nae,huyo mtoto ni WA mume husika.

Ni Sawa na wewe ukizaa nje ya ndoa basi huyo mtoto wa zinaa sio wako kwakuwa hauna nasabu naye kutokana na kutokuwa na ndoa Kati yenu.
 
Iko hivi...

Ndoa ndio kidhibitisho chako wewe kuwa huyo mtoto ni wako kisheria, ndio inakupa umiliki halali WA hao watoto wako kwasababu mwenye shamba ndio mwenye mazao yake.
Kwenye ndoa ya Mutah utajuaje mtoto ni wako , na ukichukulia unaweza maliza siku tatu zako kidume kingine kikaoa siku tatu tena
 
Kwenye ndoa ya Mutah utajuaje mtoto ni wako , na ukichukulia unaweza maliza siku tatu zako kidume kingine kikaoa siku tatu tena
Hizo zilikuwa na mushkeli ndio maana zilifutiliwa mbali, naamini waliofuatia kuzifanya walikuwa na mapungufu mengi

Na

Kuna kauli zinasema kuwa hizo ndoa hazikuwepo.
 
Hizo zilikuwa na mushkeli ndio maana zilifutiliwa mbali, naamini waliofuatia kuzifanya walikuwa na mapungufu mengi

Na

Kuna kauli zinasema kuwa hizo ndoa hazikuwepo.
Hakuna ushahidi zilifutwa , Muhammad kafa zilikiwa zinaendelea ,

Unataka kusema Allah anaweza leta ndoa ambayo Ina mushkeli? Embu rekebisha kauli
 
Hakuna ushahidi zilifutwa , Muhammad kafa zilikiwa zinaendelea ,

Unataka kusema Allah anaweza leta ndoa ambayo Ina mushkeli? Embu rekebisha kauli
Je unajua makusudio ya kuletwa zile ndoa?
 
Rekebisha kwanza kauli Yako kumzulia Allah kaleta ndoa yenye mushkeli,

Kazi ya kumpinga Allah niachie mimi
Mushkeli kwa watekelezaji WA ndoa hizo na sio Allah azza WA jallah
 
Back
Top Bottom