Je, mtu huyu nimfungulie kesi ya aina gani?

Kuna wakat unakuwa na akili kuna wakat unakuwa ovyo sana
 
Umefafanua vyema sana mkuu, Ningependa kujua je, wosia unaokubalika lazima uwe na vigezo vipi?
 
Nakazia swali maana hata mimi nimeshindwa kuelewa huyo mke umeishi nae muda gani na kama mmebahatika kupata watoto hao watoto wana umri gani?

Hizo mali anazosimamia shemeji yako zina jina la mkeo,lako au majina yenu wote wawili na kama jina la mkeo kwa sababu gani na wewe ulikuwepo?
 
Mkuu UMUGHAKA ni mke wangu wa ndoa kabisa,ndoa ya kanisani,na vyeti via ndoa ninavyo,tumejaaliwa watoto wawili,wote wapo shule na vyeti vyao vya kuzaliwa ninavyo,mke wangu tulimzika nyumbani kwangu,hapa hapa ninapoishi sasa.
Mkuu huyo Mkeo alikuwa kabila gani kwanza
 
hapo sijaelewa msimamizi wa mirathi anachaguliwa vipi wakati mme bado yuko hai,
hiyo ndoa ipo kisheria ama ilikuwa sogea tuishi?
Swala la Nani awe msimamizi wa Mirathi ni swala la makubaliano ndani ya familia hasa hasa wale ambo ni warithi halali wakubaliane na waampe baraka zao Kama msimamizi wa Mirathi ya Marehemu,hata Jirani anaweza kua msimamizi wenu mradi tu mkubaliane kwa pamoja!!!
 
Asipotumia huu ushauri wako basi atakua hana shida. Angalizo pia hapa tumesikia ya upande mmoja usikute jamaa ni mfujaji wa mali pia ni mlevi ana wake wengine huko sijui michepuko ambayo itaathiri welfare ya watoto na mpaka muda huu watoto nani anaishi nao usikute baada ya wife kufariki jamaa alijitoa kwenye jukukumu la malezi wanaume tunakuwaga wrpesi sana kujiondoa kwenyr malezi hili linaweza kumuathiri. UMEMPA USHAUR BOMBA TENA WAKISHERIA.
 
Sawa kabisa mkuu,naomba kwanza unieleweshe jambo moja zaidi,mtu aliyeteuliwa na familia kusimamia mirathi anapaswa kwenda kuthibitishwa na mahakama,nimeambiwa kwa ndoa ya kikristo ni mahakama ya wilaya tu,lakini pia mtu huyo atapaswa kwenda na vielelezo kadhaa,vikiwemo muhtasari wa kikao cha familia,hati ya kifo,barua ya kiongozi wa serikali wa eneo alilokuwa akiishi marehemu na kiapo,sasa hati ya kifo ninayo mimi,na hakuwahi kunitaka nimpatie kwa sababu yoyote,mwenyekiti wa mtaa tunaoishi pia ameniambia kuwa hakuna mtu aliyemwendea kutaka barua yoyote kuhusiana na mirathi ya mke wangu,huyu mwenyekiti ni mtu wa karibu na familia yangu sana,ila nyumba na viwanja vyenye utata vipo kwenye mitaa tofauti tofauti,sasa je kuna uwezekano wa huyo ndugu kupata hati nyingine ya kifo tofauti na ile niliyonayo?na je nikitaka kuonana na kiongozi wa mtaa nitapaswa kwenda kwa huyu wa hapa tunapoishi au kule ambapo ndipo penye hizo Mali? Hata hivyo ni takribani miezi kumi na moja imeshapita toka mke wangu alipofariki,na kwa maelezo yako ya kisheria ni wazi kuwa alipaswa awe ameshafunga jalada la mirathi,kitu ambacho hajafanya hadi muda huu,na sidhani kama alikwenda mahakamani.
 
Umefafanua vyema sana mkuu, Ningependa kujua je, wosia unaokubalika lazima uwe na vigezo vipi?
Kwenye wosia huwa kuna mitazamo tofauti tofauti sana ya upi ni wosia halali ila kwa ujumla wake ni kuwa, wosia uwe umeandikwa na marehemu, uwe una mashahidi kulingana na sheria inavyoelekeza, uwe uliandikwa wakati Marehemu akiwa kwenye hali nzuri kiakili, uwe umetunzwa sehemu isiyoweka mashaka juu ya uhalali wake.

Bado wosia huo utaje warithi na mali za marehemu, umtaje msimamizi, usibague mtoto yoyote wa marehemu ikitokea ukasema mtoto fulani asipewe urithi basi uweke na sababu ambazo za msingi ni kama mtoto hakumtunza mzazi wake huyo au kama alitaka kumuua/kumdhuru.

Sasa hayo yanaweza yakawepo au yasiwepo kwa ukamilifu wake na bado wosia ukawa halali, itategemea na mazingira.

Unaweza ukakuta maelekezo tu kwenye note book au diary ya marehemu yakageuka wosia. Uhalali wa wosia huwani vurugu mechi sana. Mfano mzuri wosia wa marehemu Regnald Mengi

Nadhani umepata picha Mkuu.
 
Nimepata naye watoto wawili,mmoja ana miaka 9 na mwingine 5,nimeishi na mke wangu kwa miaka 9,ni hivyo mkuu
 
Watoto ninaishi nao mimi,na kuhusu ufujaji na hayo mengine sina kabisa mkuu,ndiyo maana nimeweza kuwekeza vitega uchumi na kuilea familia yangu vyema kabisa mkuu,ushauri nimeuzingatia na nitaufanyia kazi haraka, asante
 
Asante sana brother umenipa elimu ya bure. God bless You
 
Hapa nitakujibu kwa vipengele Mkuu.

1. Mahakama yakufunglia.shauri la mirathi ni aidha Mahakama ya mwanzo au Mahakama Kuu, na hapa nakushauri ukafungue Mahakama ya Mwanzo, utaratibu sio mgumu.

2. Swala la vielelezo hapa inabidi kwabza uwe na uhakika 100% kama je, alifungua shauri la mirathi Mahakamani na kuteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi?.

3. Ili kufungua shauri la mirathi vielelzo vinavyotakiwa ni Cheti cha kifo, muhkasari wa kikao kumteua msimamizi, wosia kama upo, na nyaraka nyingine kadiri Mahakama itavyohitaji ikiwa ni pamoja na cheti cha ndoa, barua ya serikali ya mtaa

4. Kuhusu wapi utafungua shauri la mirathi ikiwa mali zipo sehemu tofauti tofauti, ni Mahakama iliyopo eneo alipofia marehemu.

Kama kuna ambacho sijagusa utanijulisha.
 
Asante,ila hujagusia kuhusu uwezekano wa yeye kupata hati nyingine ya kifo tofauti na hii niliyonayo,au kama anaweza kuthibitishwa na mahakama pasipo kupeleka hati hiyo,na pia nimeambiwa kuwa kwa ndoa za kiislamu na kimila mirathi inafunguliwa mahakama ya mwanzo,na kwa ndoa ya kikristo na ambapo thamani ya mirathi haizidi tsh 100,000,000 basi ni mahakama ya wilaya,au mahakama kuu ikiwa thamani ya Mali itazidi kiwango hicho,niweke sawa kwa hili pia mkuu,nashukuru mno brother.
 
Hujanielewa mkuu,nimesema siku hiyo ya mazishi ambayo ndiyo kikao kilikaa sikuwa sawa kiakili,hivyo sikuzingatia kuhusu habari ya mirathi
Pole sana. Na hii ndio shida mara nyingi hivi vikao vinafanyika siku ya mazishi jioni so unakuta bado umevurugwa na hapa wajanja ndio wanajipenyeza na kama wao ndio walikuwa wengi na wana tamaa ya mali lazima wakuzidi akili wakijua kufuatacho ITV.
 
Nafikiri huyo shemeji yako, hana nguvu yoyote kisheria kuzimiliki hizo mali maana mwenye mali alikuwa na familia, sasa atakaesimama kwenye mali hizo ni mumewe,ilikuaje mpaka shemeji aje kusimamia mirathi upande wa dada yake.?
 
Kuna harufu ya Jinai hapa Kama kweli atakua na form no IV ya usimamizi wa Mirathi! Forgery inanukia, endelea kuchimba huko Mahakamani ujuwe ukweli wote! Anafunguwaje Mirathi ya Marehemu bila ya Vielelezo muhimu vya Marehemu Kama vile hati ya kifo!!??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…