Je, mtu huyu nimfungulie kesi ya aina gani?

Halafu umemuachia shemeji akupangie mali zako na watoto wako, hivi shemeji ameingiaje hapo?
Kile kikao cha kifamilia sijui hata kilifikiaje hitimisho hilo,labda waliangalia ukaribu wake na familia yangu,yule mtu tulikuwa tunamuamini na nilimtumia kwa kazi nyingi tu mkuu
 
Hongera kwa kupigania haki yako mkuu,mimi kingine kilichonipa changamoto ni umbali kutoka eneo langu la kazi,maana ni mkoa tofauti,nimekuja hapa wakati huu kwa kuwa angalau kwa sasa naweza kulishughulikia hilo,nina muda kidogo wa mapumziko,shukrani sana mkuu
 
Siyo watu wote wanajua Mambo ya Mirathi na taratibu zake, wengine ndiyo hadi waafiwe ndiyo labda wanaweza kuanza kujua Mambo hayo tena kwa kuelekezwa na watu wanaojua utaratibu wa Mirathi!!
Kweli,kuna mtu hapo kaingiza hii issue yangu na ukosefu wa elimu ya shule!! Kumbe kuna hadi wasomi wabobevu wa masuala mengine hawajui issue tofauti na walichosomea,kuna mzee mmoja ni rafiki yangu na ni msomi wa haja,nilimwomba ushauri juu ya jambo hili akaniambia hajui lolote kuhusu mambo ya mirathi,kawaida sana
 
Asante,ila umenitisha,nitapambana mkuu,asante sana
 
Mkuu Equation x wazazi wa mke wangu walishafariki mke wangu akiwa mdogo sana,akalelewa na shemeji yake.
Nafasi ya mzazi, itumiwe na shemeji aliyemsomesha na kumlea, na muweke makubaliano ya kunufaika kwa watoto na wao kupitia mali za marehemu; hawa ndugu wengine hawana maamuzi kwenye hilo.

Kama ni mtu wa ibada, ita wazee wa kanisa/msikiti, mwenyekiti wa mtaa na mfikie maamuzi; kikao kianze kwa sala. Hawa ndugu wengine watakuwa ni mashuhuda tu, na hawatakiwi kumiliki chochote.
 
Asante sana mkuu,kuna mdau hapa ameniunganisha na mwanasheria mmoja,nimempigia simu tukaongea kidogo,amenieleza hivi hivi kama ulivyoeleza hapa,tena kumbe naye alikuwa anasoma thread hii,au ndiyo wewe mkuu?shukrani sana,umenitia moyo sana
 
Asante sana mkuu,kuna mdau hapa ameniunganisha na mwanasheria mmoja,nimempigia simu tukaongea kidogo,amenieleza hivi hivi kama ulivyoeleza hapa,tena kumbe naye alikuwa anasoma thread hii,au ndiyo wewe mkuu?shukrani sana,umenitia moyo sana
hapana sio Mimi# Ila IAM a lawyer too
 
hapo sijaelewa msimamizi wa mirathi anachaguliwa vipi wakati mme bado yuko hai,
hiyo ndoa ipo kisheria ama ilikuwa sogea tuishi?
 
Ondoa shaka mkuu,huyo jamaa hata help ya kunilogea labda aje kuniomba,nadhani ni njaa tu zinamsukuma kufanya hivyo,ndugu zake wa kuzaliwa wamemwita na kumtaka mara kadhaa aachane na Mali za watu,sasa hivi amewa block wote,hakuna kitu ataachiwa mkuu,nitaleta mrejesho hapa,wadau hapa wamenipa nguvu na are ya kupigania haki yangu kwa mustakabali wa familia yangu,nipo njiani sasa hivi,nimeanza rasmi.
 
Ww ni mtu mzima,kwa nini ulishindwa kushinikiza ili uwe msimamizi wa.mirathi.Kama kweli una haki katika mali hizo mkatae huyo msimamizi.Wanasheria watakusaidia zaidi
...Hakuwa Hata na Haja ya Kuchaguwa Mtu Mwingine awe Msimamizi wa Mali za Mkeo wakati wewe Upo hai!
Ulibugi. Tafuta Wakili Mzuri umueleze A to Z.
Wanakuchezea hao...[emoji35]
 
Ndg yangu wala usijali,siyo kosa kabisa Mtu kuchelewa kujua Mambo na taratibu za Mirathi japokua zipo kwenye vitabu vya Sheria zetu na ndiyo maana tuna Wana Sheria Kama vile tulivyo na ma Dr kwa ajili ya watu Wagonjwa! Na Mara nyingi Mambo ya Mirathi yanakuja Kama kuna Mali za Marehemu zenye mgogoro ndiyo huwa linaangaliwa swala zima la Mirathi na taratibu zake!!
 
hapo sijaelewa msimamizi wa mirathi anachaguliwa vipi wakati mme bado yuko hai,
hiyo ndoa ipo kisheria ama ilikuwa sogea tuishi?
Ndoa ya kanisani,na vyeti vyote viwili ninavyo,sasa nimejua kuwa kumbe ni hitaji la kisheria ukoo au familia kukaa kikao baada ya mazishi na kumpendekeza msimamizi wa mirathi,na anaweza kuwa yeyote mwenye uchungu na Mali za marehemu,tatizo lililojitokeza hapa ni tamaa,asante mkuu
 
Ndugu umezaa nae watoto wawili ina maana hizo mali ni za hao watoto wenu wawili ila msimamizi mkuu ilitakiwa ubaki wewe hata kwa mali alizo zichuma kabla kwa sababu ana watoto. Ungekua hujazaa nae hata kama pia sheria ina kutambua kua una haki lakini ki ustaarabu ungewaachua ndugu zake, as long unezaa nae hizo mali ulitakiwa uzisimamie kwa manufaa ya hao watoto. Ninacho kiona mimi hapo maregemu anaonekana ndo alikua bread winner of the familiy na bado alikutawala wewe na huo udhaifu umeendelea nao mpaka baada ya mke kufariki. Nini cha kufanya kama ulisign huo waraka wa kumteua huyo msimamizi wa mirathi ambalo wengi wamekuambia ni kosa kubwa ulifanya. Unapaswa kutafuta mwanasheria akusimamie kwamba huna imani na msimamizi wa mirathi ainisha haya matendo aliyo kwisha kuyatenda. nafasi hiyo ipo na una haki kwa kiasi kikubwa sana
 
Pole sana Mkuu na msiba.na maswahibu unayopitia kwa sasa.

Sijaweza kusoma comment zote ila kama kutakuwa na comment ambayo imesema nitakayokueleza basi naungana nayo.

Haya twende kazi,

Nitaeleza kazi za msimamizi wa mirathi kwa ufupi sana ili upime je anazifanya huyo msimamizi wa mirathi ya marehemu mkeo

Kazi kuu ya msimamizi wa mirathi ni kutambua na kukusanya mali za marehemu na kisha kuzigawa kwa warithi wake, ndani ya miezi 6. Sasa swali ni je huyo msimamizi wa mirathi amezitambua na kuzikusanya mali za marehemu mkeo?, baada ya kuzitambua na kuzikusanya amezigawa kwa warithi wa hizo mali?. Je, amefuata muda uliowekwa na sheria yaani miezi 6?. (Majibu unayo ila nitaeleza chakufanya ikiwa ni tofauti)

Sasa jambo gani ufanye ikiwa hajafuata muongozo wa sheria.

Hapa unatakiwa kwenda kufungua pingamizi dhidi ya msimamizi wa mirathi ukiitaka mahakama itengue/ifute uteuzi wake kwa kuwa hawezi kukusanya na kugawa mali z marehemu na pia amekuwa mharibifu/mpotevu wa mali za marehemu na zaidi ya yote amejinufaisha yeye binafsi.

Sasa kabla ya kufanya yote haya kuna jambo unatakiwa uwe na uhakika nalo kwa 100% ambalo ni Je, huyu shemeji yako aliteuliwa na Mahakama kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu mkeo?, au mliishia kwenye kikao cha familia/ndugu?.

Kama alipeleka maombi ya kuteuliwa Mahakamani basi sasa hapo unatakiwa kuomba mahakama itengue/ifute uteuzi wake. Kama hakuwahi kupeleka maombi ya kuteuliwa Mahakamani na mahakama.ikayakubali maombi yake basi huyo sio msimamizi wa mirathi kwakuwa ni Mahakama pekee yenye uwezo wa kuteua msimamizi wa mirathi na mahakama hiyo ni Mahakama ya Mwanzo au ahakama Kuu na sio ahakama nyingine zilizosalia.

Sasa kama hakuwahi kupeleka ombi Mahakamani, wewe sasa unatakiwa kupeleka maombi ya kuteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu mkeo Mahakamani. Hapa utatakiwa kuwa na muhuktasari wa kikao cha familia kukupendekeza kama msimamizi wa mirathi ikiwa mkeo hakuacha wosia.

Ikiwa ni ngumu kuitisha hicho kikao wewe nenda mahakama ya mwanzo fungua hivyo hivyo ombi la kuteuliwa kisha ieleze ahakama kwanini.hakuna muhuktasari wa kikao na hapo utaeleza kuwa aliyependekezwa hajafungua mirathi na anapoteza mali za marehemu ambapo hata marehemu asingezipoteza hivyo. (Shawishi Mahakama ila chunga usiwe unalalamika).

Kuna swala la wosia, kama mkeo aliacha wosia basi fuateni wosia unasema nini na hapa ni lazima bado kufungua mirathi mahakamani ila uzuri hapa hamtakuwa na sababu ya kikao cha kumteua msimamizi wa mirathi sababu tayari katajwa na wosia.

Mimi ni haya tu kwa sasa naamini utapata mwanga wakutosha kujua ufanye nini, ukiwa na maswali usisitekuuliza. Naweza nikachelewa kujibu ila nitakujibu tu.

Karibu.
 
Asante mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…