Je, mtu unaweza kupokea Ekaristi Takatifu bila kula kile kipande cha ngano?

Je, mtu unaweza kupokea Ekaristi Takatifu bila kula kile kipande cha ngano?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Mantiki ya swali langu inalengo la kufahamu, je, Ekaristi ni kitu ‘Spiritual’ au ni kitu ‘physical’? Meaning, mtu anaweza kupokea Ekaristi bila kula kile kioande cha mkate? Spiritually tu kwa kuamini?
 
Ngoja waje hapa. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji3][emoji3]
 
Baada ya Yesu kufufuka, alikutana na wanafunzi wake mara nyingi. Na katika kukutana kwao aliumega mkate, baada ya kupaa wanafunzi walikua na desturi ya kukutana mara kwa mara na kila wakikutana walifanya maadhimisho ya ekarist takatifu kwa kuumega mkate.

Physical action ni kuumega nabkuula
Spiritual action or sense or aim n ye maneno
Huu ni mwl wangu uliotolewa kwa ability yenu. Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mm.

Unastairi ya kuila ekarist kama unavyovigezo.
 
Vyote ni sawa, unaweza ukapanga foleni mkate ukaisha au kwa sababu nyingine yoyote ile wakakunyima, hapo unakuwa umekula kwa imani.
Padre ama mhudumu wa Ekaristi anapaswa kuhakikisha kila mmoja anapokea mkate (hata kama itakuwa punje) au divai ama vyote.

Ndio maana kuna muda humpasa kuivunjavunja ama kutoa divai. Tunapaswa kumpokea Kristu katika substance.

Sakramenti ni alama za wazi na zinazoonekana...
 
Hatuli kipande cha ngano, tunapokea mwili na damu ya Yesu Kristu katika umbo (substance) ya mkate na au divai. Japokuwa matunda yake ni ya kiroho; sharti ipokelewe katika umbo (substance) ya ama mkate ama divai ama vyote.
Nini kinatofautisha hii na ‘Symbolism’ za waganga wa jadi? Mfano, why akuambie ulete kuku mwekundu au mweupe au mweusi? Why? Asipokuwa wa rangi hizo inakuwaje? Au why mtu ale kipande cha ngano na sio kipande cha sembe? Why?
 
Padre ama mhudumu wa Ekaristi anapaswa kuhakikisha kila mmoja anapokea mkate (hata kama itakuwa punje) au divai ama vyote.

Ndiyo maana kuna muda humpasa kuivunjavunja ama kutoa divai. Tunapaswa kumpokea Kristu katika substance.

Sakramenti ni alama za wazi na zinazoonekana...
Anaeoka hivyo vipande vya ngano, akiwa ni mzinzi kwa mfano, inaathiri utendaji kazi wa hiyo dawa?

Maana kwa upande wa waganga wa jadi, unaambiwa ukioga hii dawa usivae viatu au vitu kama hivyo.., je .., kuna masharti katika upikaji wa hiyo dawa ya mkate?
 
Logically inatakiwa hata usipokula uwe umepokea...

Otherwise inakuwa ni kama masharti ya kiganga...na ile dhana ya kuabudu vitu itapata nafasi hapo...

Ngoja wataalamu waje.....
 
Logically inatakiwa hata usipokula uwe umepokea...

Otherwise inakuwa ni kama masharti ya kiganga...na ile dhana ya kuabudu vitu itapata nafasi hapo...

Ngoja wataalamu waje.....
Naona wewe kidooogo unaelewa ninachojaribu ku-inquire
 
Anaeoka hivyo vipande vya ngano, akiwa ni mzinzi kwa mfano, inaathiri utendaji kazi wa hiyo dawa?

Maana kwa upande wa waganga wa jadi, unaambiwa ukioga hii dawa usivae viatu au vitu kama hivyo.., je .., kuna masharti katika upikaji wa hiyo dawa ya mkate?

Ule mkate unakuwa wa kawaida Tu kabla haujaombewa na padre ili kuugeuza kuwa mkate na damu ya kristu.. Kwa hiyo hakuna uhusiano kati ya mtengezezaji na ule mkate maana hata padre ukimkuta nje ni mtumishi wa kawaida Ila anaposimama madhabahuni, husimama kwa niaba ya mamlaka ya mbingu anayoiwakilisha


Kuhusu uhusiano wa vitu physical na kiroho nadhani ungeanza kujiuliza kwa nini toka enzi mwanakondoo alichinjwa hekaluni ili kumuondoa mtu dhambi au kwa nini Kristu alifanywa mwanakondoo aliyetolewa kafara ili kuondoa dhambi za ulimwengu

Kuna nini kwenye damu katika utakaso, kwa nini vitu visingefanyika Tu kiroho vikaisha ??

Je, kwa nini zamani watu walipaka majivu na kuvaa magunia katika kuomba toba mfano wanaisrael kipindi cha malkia ehster na kivipi kanisa katholiki huanzisha kwaresma kwa kupaka watu majivu kama ishara ya kuomba toba, kuna siri gani ya hayo majivu??...


Nachomaanisha kila unachokiona ulimwenguni kina kusudi lake ndio maana hata hao waganga unaowasema hutumia mitishamba na manuizi katika kufanya vitu vyao kwa sababu kuna muingiliano na mtegemeano kati ya ulimwengu tunaouona kwa macho na wa kiroho..

Hii ni kwa elimu yangu ndogo Tu 🙏🙏
 
Mleta mada kama ww ni mkatoliki nenda kwenye parokia iliyo jirani nawe onana na padre au katekista atakujibu maswali yako yote kama unaishi mbali na parokia/kigango na huna nauli sema nitakutumia ili ujibiwe maswali yako kwa ufasaha.
 
Back
Top Bottom