Je, mtu unaweza kupokea Ekaristi Takatifu bila kula kile kipande cha ngano?

Nini kinatofautisha hii na ‘Symbolism’ za waganga wa jadi? Mfano, why akuambie ulete kuku mwekundu au mweupe au mweusi? Why? Asipokuwa wa rangi hizo inakuwaje? Au why mtu ale kipande cha ngano na sio kipande cha sembe? Why?
Sijui kuhusu waganga wa jadi; kwa Wakatoliki tunatimiza agizo la Yesu Kristu - kumkumbuka kila tukutanapo kama Kanisa.

1 Wakorintho 11:23-26
Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, "Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu." na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, "Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu." Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.

Kwa kuwa Kristu alifanya hivyo kwa mkate (ngano), basi nasi tunafanya vivyo hivyo. Jambo la msingi kuzingatia hapa ni kuwa hatupokei kipande cha ngano, bali twampokea Kristu Bwana wetu katika maumbo ya mkate na mvinyo.
 
Anaeoka hivyo vipande vya ngano, akiwa ni mzinzi kwa mfano, inaathiri utendaji kazi wa hiyo dawa?

Maana kwa upande wa waganga wa jadi, unaambiwa ukioga hii dawa usivae viatu au vitu kama hivyo.., je .., kuna masharti katika upikaji wa hiyo dawa ya mkate?
Agano ni kati yetu na Kristu Yesu; siyo kati yetu na ngano ama aliyeoka mkate ama mtu au kitu kingine kiwacho chote.
 
Nini kinatofautisha hii na ‘Symbolism’ za waganga wa jadi? Mfano, why akuambie ulete kuku mwekundu au mweupe au mweusi? Why? Asipokuwa wa rangi hizo inakuwaje? Au why mtu ale kipande cha ngano na sio kipande cha sembe? Why?
Yesu alitumia mkate na divai kugeuza kuwa mwili na damu yake. Ndicho lifanyacho ichoo.

Hakutumia sembe na soda au juice ila mkate na divai so kanisa linafanya na kutumia kilekile kilichofanywa na Yesu.

Afu kuna mengi zaidi ya kula tu ule unaoita mkate na kunywa ile divai, kama "ishara ya ushirika na waumini wenzako na Yesu mwenyewe, ishara umoja na waumini wenzako unaounganishwa na huo mwili na damu ya kristo kupitiamkate na divai) ndio maana haiwezekani kuassume tu kuwa umekunywa mwili na damu ya Yesu bila kuvila ivyo physically
 
Sijui kuhusu waganga wa jadi; kwa Wakatoliki tunatimiza agizo la Yesu Kristu - kumkumbuka kila tukutanapo kama Kanisa.

1 Wakorintho 11:23-26
Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, "Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu." na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, "Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu." Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.

Kwa kuwa Kristu alifanya hivyo kwa mkate (ngano), basi nasi tunafanya vivyo hivyo. Jambo la msingi kuzingatia hapa ni kuwa hatupokei kipande cha ngano, bali twampokea Kristu Bwana wetu katika maumbo ya mkate na mvinyo.
Kama unachosema ni kweli, kwanini mnachagua with extreeme bias vile vya kumkumbuka? Kwanini hatumkumbuki katika maisha yake ya 18yrs to 30yrs? Lengo lenu ni nini?
 
Kumbuka Yesu alianza kazi yake ya ukombozi at 30 age.

UkiTafuta vitabu vyenye mambo ya mapokeo na kujisomea, maisha ya Yesu at 18yrs na utoto wake utayakuta huko mambo mengi tuu. Hayo kanisa halina haja ya kuyatilia maanani wala kuyafanyia kumbukumbu, sababu hayana msaada wowote kwa muumini kuupata uzima wa milele, ndio maana hata kwenye bible hayapo, yangekuwa na msaada ungeyaona kwenye biblia.

Zaidi hilo la mkate na divai kuwa mwili na damu ya yesu (mwili na damu yake) yesu mwenyewe, alilisisitizia kwa maneno "fanyeni ivi kwa ukumbusho wangu" ndio maana linakumbukwa na kufanywa hadi leo.
 
Aisee
Hizi dini zimetufanya kuwa wajinga sana…
Eti unakula mwili wa bwana…
Uchuro na Ulozi huu….
Ni kwa jicho la kiimani tu ndio unaweza kusadiki. Maana hata wayahudi wenyewe hawakumwelewa na walimsumbua sana kuwa tunawezaje kula mwili wake na kunywa damu yake mtu huyu. Walimwona ni kama mwendawazimu ivii. Nafikiri ingekuwa ni leo angeitwa mchawi mkubwa sana kwamba yaani tule mwili wake na tunywe damu yake huo si uchawi aiseee.

Lakini mwisho wa siku alikuja kueleweka vizuri tu na kwanza wanafunzi wake mwenyewe na ndicho kinachofanywa mpaka leo na kanisa.
 
Vyote ni sawa, unaweza ukapanga foleni mkate ukaisha au kwa sababu nyingine yoyote ile wakakunyima, hapo unakuwa umekula kwa imani.
Kunyimwa kivipi mkuu hebu fafanua.

Sababu mbaka unapanga foleni maanayake umekidhi vigezo, kwanini unyimwe.
Nakama hujakidhi vigezo unakuwa hustahili sio kunyimwa.
 
Kumbuka Yesu alianza kazi yake ya ukombozi at 30 age.

UkiTafuta vitabu vyenye mambo ya mapokeo na kujisomea, maisha ya Yesu at 18yrs na utoto wake utayakuta huko mambo mengi tuu. Hayo kanisa halina haja ya kuyatilia maanani wala kuyafanyia kumbukumbu, sababu hayana msaada wowote kwa muumini kuupata uzima wa milele, ndio maana hata kwenye bible hayapo, yangekuwa na msaada ungeyaona kwenye biblia.

Zaidi hilo la mkate na divai kuwa mwili na damu ya yesu (mwili na damu yake) yesu mwenyewe, alilisisitizia kwa maneno "fanyeni ivi kwa ukumbusho wangu" ndio maana linakumbukwa na kufanywa hadi leo.
Naomba kukupinga hapo unaposema maisha ya yesu between 18yrs na 30yrs hayana maana yeyote. Kwamba katika kipindi hicho maisha yake hayakuwa na cha kuigwa kama mfano kwetu?
Inamaana unataka kusema matendo yake katika umri huo si ya kupigiwa mfano kabisa, na hatupaswi kumkumbuka? Ila tuendelee tu kulishwa ngano na pombe kali kwa kisingizio cha kumkumbuka?

Alifunga ndoa lini na alifunga na nani? Tusije tukawa tunakula nyama na kunywa damu ya mzinzi bila kufahamu..? Maana umri huo wa 18-30 majaribu ni mengi sana

Halafu hili suala la kula nyama za watu / mtu na kunywa damu za watu, mbona limekaa kichawi chawi sanaaa.., ushirikina mwingi mno kwenye mambo ya kula nyama za watu.., kwanini mnafanya shirki kwa kisingizio cha kukumbukana?!
 
Kama yapi?
Nyie mlioandika biblia ndio mtuambie, unaniuliza mimi?! Serioulsy..

Lakini huu ustaarabu wa kula nyama ya mungu na kunywa damu ya mungu nyie inawaingia vipi akilini? Kumbuka, Yesu ni mungu...
 
Sasa wewe hutaki kula nyama unataka unywe damu tu, umekuwa simba?
 
Naomba kukupinga hapo unaposema maisha ya yesu between 18yrs na 30yrs hayana maana yeyote. Kwamba katika kipindi hicho maisha yake hayakuwa na cha kuigwa kama mfano kwetu?
Inamaana unataka kusema matendo yake katika umri huo si ya kupigiwa mfano kabisa, na hatupaswi kumkumbuka? Ila tuendelee tu kulishwa ngano na pombe kali kwa kisingizio cha kumkumbuka?

Alifunga ndoa lini na alifunga na nani? Tusije tukawa tunakula nyama na kunywa damu ya mzinzi bila kufahamu..? Maana umri huo wa 18-30 majaribu ni mengi sana

Halafu hili suala la kula nyama za watu / mtu na kunywa damu za watu, mbona limekaa kichawi chawi sanaaa.., ushirikina mwingi mno kwenye mambo ya kula nyama za watu.., kwanini mnafanya shirki kwa kisingizio cha kukumbukana?!
Yohane 20: 30-31.

30: Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki.

31: Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.

mkuu hata kwa logic ya kawaida tu ni kitabu kikubwa kiasi gani chaweza kutengenezwa kwa kuandika kila kitu alichofanya na kupitia muhusika (Yesu) toka anazaliwa mpaka anakufa (at 33yrs).

pia kuna shida kadhaa na ugumu wa kufanya hilo.

1: utunzaji wa kumbukumbu wa matendo yote ya muhusika toka anazaliwa mpaka kufa, sembuse kwa technology zilizokuwepo zama za Yesu ?, afu kabla hajaanza kazi yake at 30yrs hakuna aliyekuwa na muda nae wala kumtilia maanani, maana walielewa ni mtu wa kawaida tu asiye na maajabu yeyote (mwana wa seremala). Alipoanza kazi yake Kuna sehemu wanamshangaa kabisa huyu si mwana wa seremala hata ndugu zake si tunaishi nao hapa, na mambo kama hayo nk. Katika mazingira kama hayo utunzaji wa kumbukumbu wa yote yaliyofanywa na muhusika enzi za utoto na ujana wake ni suala gumu mkuu.

2: mengi ya yaliopo ni masimulizi tuu yaliochambuliwa kwa kuzingatia standards fulani basi hata wewe unaweza tafuta na kujifunza, lakini hayawezi kuingia kwenye "maandiko matakatifu" wala "mapokeo matakatifu" mapokeo matakatifu na maandiko matakatifu yanastandards zake pia, sio chochote tu kilichoandikwa kuhusu Yesu kitaingia kwenye biblia.

kwahiyo ni ngumu sana kuelewa na kuwa hakika kuwa hiki kweli ni halisi hakuna uongo wowote, au ni mambo ya kutunga tuu. Hivyo yanabaki kama mapokeo tuu basi
 
Nyie mlioandika biblia ndio mtuambie, unaniuliza mimi?! Serioulsy..

Lakini huu ustaarabu wa kula nyama ya mungu na kunywa damu ya mungu nyie inawaingia vipi akilini? Kumbuka, Yesu ni mungu...
Wewe ndio unatakiwa uyataje hapa hayo mambo unayoona ni lazima yakakumbukwa pia.

Afu una mambo mengi mara ndoa mara umungu wa Yesu.
 
Yohane 20: 30-31.

30: Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki.

31: Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.

mkuu hata kwa logic ya kawaida tu ni kitabu kikubwa kiasi gani chaweza kutengenezwa kwa kuandika kila kitu alichofanya na kupitia muhusika (Yesu) toka anazaliwa mpaka anakufa (at 33yrs).

pia kuna shida kadhaa na ugumu wa kufanya hilo.

1: utunzaji wa kumbukumbu wa matendo yote ya muhusika toka anazaliwa mpaka kufa, sembuse kwa technology zilizokuwepo zama za Yesu ?, afu kabla hajaanza kazi yake at 30yrs hakuna aliyekuwa na muda nae wala kumtilia maanani, maana walielewa ni mtu wa kawaida tu asiye na maajabu yeyote (mwana wa seremala). Alipoanza kazi yake Kuna sehemu wanamshangaa kabisa huyu si mwana wa seremala hata ndugu zake si tunaishi nao hapa, na mambo kama hayo nk. Katika mazingira kama hayo utunzaji wa kumbukumbu wa yote yaliyofanywa na muhusika enzi za utoto na ujana wake ni suala gumu mkuu.

2: mengi ya yaliopo ni masimulizi tuu yaliochambuliwa kwa kuzingatia standards fulani basi hata wewe unaweza tafuta na kujifunza, lakini hayawezi kuingia kwenye "maandiko matakatifu" wala "mapokeo matakatifu" mapokeo matakatifu na maandiko matakatifu yanastandards zake pia, sio chochote tu kilichoandikwa kuhusu Yesu kitaingia kwenye biblia.

kwahiyo ni ngumu sana kuelewa na kuwa hakika kuwa hiki kweli ni halisi hakuna uongo wowote, au ni mambo ya kutunga tuu. Hivyo yanabaki kama mapokeo tuu basi
Conveniently, kipindi cha hadi miaka 12 maisha ya Yesu kimeandikwa kwenye biblia, alipoingia balehe tu, kuanzia miaka 13, hakuna chochote juu yake , how convinient?! Baada ya miaka 30 hatuambiwa ana wake wangapi wala watotot wangapi, na kuanzia miaka 13 hadi 30 hakuna chochote kinachofahamika juu ya maisha yake, how convinient? Tutajuaje kama tunakula nyama ya mzinzi? Maana miaka 13 hadi 30 vishawishi ni vingi mno, alifunga ndoa lini , wapi na nani? Na aliacha watoto wangapi? Msijisahaulishe, maana alitahiriwa kabisa. Na hadi leo hatujui ni kwanini mungu alitahiriwa, total confusion, why mnatuchanganya hivi?! Why?!
 
Wewe ndio unatakiwa uyataje hapa hayo mambo unayoona ni lazima yakakumbukwa pia.

Afu una mambo mengi mara ndoa mara umungu wa Yesu.
Mambo ya kuanzia balehe yake, miaka 13 hadi miaka 30, hayo ndio tunataka tuyajue na kuyakumbuka pia
 
Back
Top Bottom