Je, mtu unaweza kupokea Ekaristi Takatifu bila kula kile kipande cha ngano?

Je, mtu unaweza kupokea Ekaristi Takatifu bila kula kile kipande cha ngano?

Comment yangu nilikujibu vizuri Tu lakini ukaamua kuipuuza, nahisi kuna majibu na nia zako binafsi unazoziamini

Ni biblia hiyo hiyo imeandika yesu alipofikishs umri wa miaka 12 alipotea hekaluni Ila Yusuph na Maria walimpata baadal akitoa hekima na maarifa kwa watu ambao walimshangaa kwa umri wake na kauli kubwa aliyoitoa ni kuwa "alikuwa kwenye nyumba ya baba yake".. Kwa hiyo usidhani Yesu alianza kuwa Yesu baada ya ubatizo maana ingekuws hivyo bhasi tungeoneshwa kama historia nyingine kwenye bible

Kingine Yesu alikuwa ni fundi seremala kama alivyokuwa baba yake Yusuph. Kingine pia usijisahaulishe Yesu alikuwa ni nafsi ya Mungu katika mwili wa binadamu. Kwa hiyo hakuwa kama Mimi na wewe kwa asilimia sote

Kingine biblia ni mkusanyiko wa vitabu ambavyo vilichambuliwa na kuwekwa pamoja ili kutoa dira ya kiimani kwa watumishi wake

Lakini haimaaanishi kuwa hakukuwa na vitabu au mapokeo ya kihistoria yaliyoachwa. Najua fika kama umeegemea katika biblia huwezi kuijua historia ya bikira mariamu mama wa Yesu Ila ipo, kuanzia utoto wake hadi kufikia point ya kumzaa Yesu katika mapokeo ya kihistoria ndio itakuwa historia ya Yesu kristu isijumuishwe

Halafu kama wewe ni mkristu utajus ya kuwa Mungu haangalii past yako katika jicho la kibinaadanu ndio maans Yesu alisema, hata dhambi zako ziwapo nyekundu kama damu Mimi nitazifamya kuwa nyeupe kuwa kama theluji

Kwa hiyo toba ipo kwa ajili hiyo kwa hiyo usiwe bitter na past za watu kinachoangaliwa ni usafi wao pale wanapookolewa. Ukisema hivyo bhasi utasema huwezi kusoma vitabu vya mtume paulo kwa sababu alikuwa muuaji wakati akiitwa sauli

Mfalme daudi, mussa, mfalme suleiman na wengine ambao waliteleza na kusamehewa. Brother kiufupi kuhukumu ni kazi isiyokuhusu
Wewe acha blablah, kama hujui ungana nami kuhoji, ni kwanini maandiko yote yame omitt maisha ya Yesu baada ya balaehe hadi alipofika miaka 30, why? Lengo lenu nini?!
 
Iwe kwenye biblia au otherwise, ni kwanini kipindi critical baada ya balehe hadi miaka 30 kimeondoloewa kwenye maandiko yote? Why? Lengo lenu ni nini?
Jibu nilichokuuliza acha blabla. Akati unahoji maswali yako ulifix kwenye biblia tuu, sasa iweje uniulize mimi reference za wewe za kutumia ?

Icho kipande Kimeondolewa kwani kiliwahi kuwemo ? Unaondoaje kitu ambacho hakipo wala hakikuwahi kuwepo ? Au hujui maana ya kuondoa ?
 
Wewe acha blablah, kama hujui ungana nami kuhoji, ni kwanini maandiko yote yame omitt maisha ya Yesu baada ya balaehe hadi alipofika miaka 30, why? Lengo lenu nini?!

Ujinga ni kutokujua kwa hiyo mjinga akielekezwa na akajua, ujinga humuisha Ila upumbavu ni foolishness na foolishness ni kipaji kama ilivyo urefu na ufupi.

Sio maneno yangu, ni Nyerere huyo mkuu 🙏🙏
 
You so said tunachagua baadhi ya mambo with extreme bias... Tueleze mambo yapi hayo tuliyoyabagua. Hiyo ni moja.

Pili; Yesu ni Mungu, hilo halina mabishano. Hatuli nyama ila mwili na damu yake. Tunapokula mwili wake tunakumbuka upendo wake usiomithilika hata akautoa mwili wake uteswe ili sisi tuokolewe.

Tunapokunywa damu yake tunakumbushwa thamani yetu ya wokovu. Hivyo, tunapokula mwili wake na kunywa damu yake tunakumbuka matukio mawili muhimu katika wokovu wetu - kifo na ufufuko wake - kama alivyotuagiza tumkumbuke mpaka atakaporudi.

Kupitia kupokea mwili na damu yake, tunapata uzima wa milele na tunaendelea kukumbushwa jinsi alivyotupenda na akajitoa kwetu mzimamzima, bila kujibakisha. Kuna upendo mkubwa zaidi ya huo?
Eti Yesu ni Mungu

Afu Mungu alitahiriwa 🤣🤣🤣🤣🤣

Sometimes kuna imani zinaondosha kabisa logical thinking.
 
Jibu nilichokuuliza acha blabla. Akati unahoji maswali yako ulifix kwenye biblia tuu, sasa iweje uniulize mimi reference za wewe za kutumia ?

Icho kipande Kimeondolewa kwani kiliwahi kuwemo ? Unaondoaje kitu ambacho hakipo wala hakikuwahi kuwepo ? Au hujui maana ya kuondoa ?
Niliposema biblia nilimaanisha maandiko in general, au hata movies, au hata hadithi za word of mouth, general namaanisha records hazisemi chochote, why?

Unaposema kitu hakijaondolewa unata kuniambia Yesu alizaliwa, akaishi hadi miaka 12 , halafu akafariki, kisha akafufuka baada ya 17yrs akiwa na miaka 30, halafu akaendelea kuishi hadi aliposulubiwa na kufariki tena? Au unamaanisha nini? Kwamba hakuishi between 12 and 30, hivyo hakuna kilichokuwa omitted?
 
Ujinga ni kutokujua kwa hiyo mjinga akielekezwa na akajua, ujinga humuisha Ila upumbavu ni foolishness na foolishness ni kipaji kama ilivyo urefu na ufupi.

Sio maneno yangu, ni Nyerere huyo mkuu 🙏🙏
Ngonjera hazitasaidia, hicho kichaka hakina majani, rudi tu huku, na ujibu hoja ya kwanini maisha yake baada ya balehe hadi miaka 30 hajaandikwa wala kuelezwa popote, alimuona nani? Alizaa watoto wanagapi? Au alienda kwenye hibernation kama yale madubu ya polar regions? Kwanini , why?!
 
Eti Yesu ni Mungu

Afu Mungu alitahiriwa 🤣🤣🤣🤣🤣

Sometimes kuna imani zinaondosha kabisa logical thinking.
Inabidi tukubali tu kwamba mungu alitahiriwa, tutafanyaje sasa ndugu yangu, ukiwahoji kama hivi wanakuwa wakali sana..
 
Soma biblia uone hivyo vifungu vya kuanzia kuzaiwa hadi miaka 12. Pia soma biblia uone hivyo vifungu vya kuanzia miaka 30 hadi kufariki kwake. Ika kuanzia miaka 13 hadi 30 hamna kitu, totally blank!!!!! Binadamu yeyote ambae hayuko biased, free thinking, an attached na hana maslahi binafsi, ni lazima atahoji, ni kwanini hakuna maelezo yeyote juu yake katika kipindi critical kama hicho cha maisha yake?!
Biblia haijaandika kila kitu kumhusu Kristu:
  • Inaelezea mazingira ya utungwaji mimba wake
  • Inaelezea mazingira ya kuzaliwa kwake na namna alivyofanyiwa mambo yote waliyopaswa kufanyiwa watoto wa Kiyahudi kama ilivyodesturi na sheria zao - kutahiriwa, kutolewa hekaluni, kusherehekea sikukuu ya Pasaka, n.k
  • Na imejikita zaidi kuelezea kazi aliyoifanya
Maana yake; Yesu alikua kama walivyokua Wayahudi wengine wote.
  • Mbona haujauliza mambo aliyoyafanya baada ya kutahiriwa?
  • Mbona haujahoji mambo aliyoyafanya baada ya kutolewa hekaluni?
  • Mbona haujataka kujua alifanya nini akiwa na miaka 3 ama 4 ama 8 ama 9, n.k?
Maana yake aliendelea kuishi maisha ya kawaida kabisa ambayo yalimuandaa kufanya kazi yake vema... Baadaye waandishi wakajikita katika kazi zake ambapo napo hawakuandika kila kitu, waliandika baadhi ya mambo kama anavyokiri Mtume Yohane.

Yohane 20:30-31
Basi kuna ishara nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki. Lakini hizi zimeandikwa, ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.

Yohana 21:25
Kuna mambo mengine mengi aliyoyafanya Yesu, ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa.
 
Niliposema biblia nilimaanisha maandiko in general, au hata movies, au hata hadithi za word of mouth, general namaanisha records hazisemi chochote, why?
Kajielimishe kuhusu maana ya bibilia ndio urudi hapa.
Unaposema kitu hakijaondolewa unata kuniambia Yesu alizaliwa, akaishi hadi miaka 12 , halafu akafariki, kisha akafufuka baada ya 17yrs akiwa na miaka 30, halafu akaendelea kuishi hadi aliposulubiwa na kufariki tena? Au unamaanisha nini? Kwamba hakuishi between
Kajielimishe kuhusu historia ya biblia na vitabu vyake ndio urudi hapa.
 
Ngonjera hazitasaidia, hicho kichaka hakina majani, rudi tu huku, na ujibu hoja ya kwanini maisha yake baada ya balehe hadi miaka 30 hajaandikwa wala kuelezwa popote, alimuona nani? Alizaa watoto wanagapi? Au alienda kwenye hibernation kama yale madubu ya polar regions? Kwanini , why?!
Huwa sifanyi arguments, nafanya discussion ONLY

Chochote unachotaka kujua nimeshakielezea kwa hiyo kuelewa ni jukumu lako, mwisho kabisa nimekuheshimu sana mkuu sio kwa sababu unastahili kwa reply zako Ila ni kwa principles zangu binafsi, naomba ukae kwenye hiyo line 🙏🙏🙏
 
Kwanini lazima nile ndio iwe ekaristi? Kwani hiyo ni dawa inayofanya kazi ‘physically’ kama panadol? Au ni kitu spiritual?
Mbona tumeshakujibu - alisema fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.

Luka 14:22-24
Nao walipokuwa wakila, alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa, akasema, "Twaeni; huu ndio mwili wangu." Akatwaa kikombe, akashukuru, akawapa; wakakinywea wote akawaambia, "Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi.

Yeye alifanya hivyo physically, na kwa kuwa tunafanya kama yeye, then inapaswa kufanyika physically. Ukifanya metaphysically hiyo itakuwa ni wewe, yeye hakufanya hivyo na agano ni kufanya kama yeye.
 
Eti Yesu ni Mungu

Afu Mungu alitahiriwa 🤣🤣🤣🤣🤣

Sometimes kuna imani zinaondosha kabisa logical thinking.
Yesu ni Mungu.

Aliamua kuchukua mwili wa kibinadamu ili aje kuishi nasi na kutuokoa.

Hivyo ni Mungu kweli, na kwa kuuchukua mwili wa kibinadamu alifanyika binadamu kweli.

Kwahiyo kama binadamu mwenye mwili na aliyezaliwa katika jamii ya Wayahudi alifuata desturi zote zilizo njema, maana yeye ndiye wema wenyewe.

Hivyo Yesu alitahiriwa, kutahiriwa hakukumuondolea Umungu bali alituonesha namna Mungu hufuata utaratibu mwema.
 
Niliposema biblia nilimaanisha maandiko in general, au hata movies, au hata hadithi za word of mouth, general namaanisha records hazisemi chochote, why?

Unaposema kitu hakijaondolewa unata kuniambia Yesu alizaliwa, akaishi hadi miaka 12 , halafu akafariki, kisha akafufuka baada ya 17yrs akiwa na miaka 30, halafu akaendelea kuishi hadi aliposulubiwa na kufariki tena? Au unamaanisha nini? Kwamba hakuishi between 12 and 30, hivyo hakuna kilichokuwa omitted?
Angalia movie ya "The Young Messiah" imeonesha jinsi alivyokua kama Wayahudi wengine wote, itakuonesha vitu vingine pia ambavyo alivipitia na kuvitenda katika makuzi yake kwa mujibu wa Mapokeo Matakatifu.

Vipi kuhusu ya adult Messiah, kipindi yuko wa moto kabisa, 18+ years, movie yake mnaiachia lini?
 
Naona wewe kidooogo unaelewa ninachojaribu ku-inquire
Wewe ni mkristo? Kama jibu ni ndiyo, je unaenda kanisani? Kama jibu ni ndiyo, kwa nini unaenda physically na usiende spirituality? Kwa nini watu wasiabudu spiritituality tu wakiwa nyumbani?
 
Logically inatakiwa hata usipokula uwe umepokea...

Otherwise inakuwa ni kama masharti ya kiganga...na ile dhana ya kuabudu vitu itapata nafasi hapo...

Ngoja wataalamu waje.....
Logic ya wapi? Ya kutunga wewe? Kama ni hivyo basi binadamu kwenye kuabudu tusingepaswa kufanya matendo yoyote kwa miili yetu. Tungepaswa kufanya mambo kwa kutumia imani na fikra basi!
 
Back
Top Bottom